Uwajibikaji wa Kijamii | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Binafsi

 Ndani ya Tigo Tanzania lengo letu la uwajibikaji kwa jamii  ni kumwezesha kila  mtu binafsi  kupiga hatua  ndani ya maisha na kuyafurahia. Tunaamini katika hamasa hii  lakini  bado lengo la msingi litakuwa ni  kutambua  kupitia  matumizi ya programu za kidijitali katika kila nyanja ya maisha.

Kwa miaka kadhaa sasa tumekuwa ni kampuni iliyo na uwekezaji mkubwa wa amana  za kuendesha na sio tu  upatikanaji wa mawasiliano  bali pia  kuendelea kujenga mfumo imara wa kiikolojia ambao unaleta matumaini  ya teknolojia katika maisha  ndani ya jamii inakoendesha shughuli zake. Tumesimamia  miakakati kadhaa  kuanzia  kuziba pengo la umiliki wa simu za mkononi miongoni mwa wanawake, kuboresha  kuunganishwa kwa shule za umma kwa  kuzipatia  intaneti ya uhakika na kuwezesha mchakato wa usajili wa uzazi kwa kutumia simu za mkononi.

 MTAZAMO WETU KATIKA UWAJIBIKAJI KWA JAMII:

 Kipaumbele cha mkakati  katika uwekezaji wetu kijamii  ni kuangalia katika maeneo matatu ya kimaudhui ambayo ni  Kujumuishwa Kidijitali, Elimu na Ujasiriamali Kibiashara. Maudhui haya yanaelezea matamanio yetu ya kumwezesha kila mmoja  na teknolojia ya kidijitali wakati  tukiunda  thamani yenye ushirikiano  kwa wadau wetu  ambao kwa kutaja baadhi  ni pamoja na  wateja, jamii, serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari.

 Yafuatayo ni maelezo mafupi  kwa kila maudhui  yanavyomaanisha kwetu; 

Vipaumbele Kimkakati  Tunamaanisha nini  katika kipindi kirefu
Kujumuishwa Kidijitali Kuwezesha kufikia  na kutoa msukumo kuchukua na kutumia Teknolojia ya Habari na Mwasiliano miongoni mwa watu binafsi au makundi kama programu  ya kupiga hatua katika elimu, kuwezeshwa kiuchumi  na ustawi wa jamii.
Elimu Kubadilisha maisha ya wanafunzi vijana kupitia kuunganishwa  na  kujenga thamani kupitia  elimu. 
Ujasirimali kibiashara Kuwapatia vijana stadi za kujenga biashara wakati  wakiunda majukwaa kwa mtandao, kujifunza na kushirikiana. 

 

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo