Madawati kwa shule za umma | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..
 Binafsi

Sekta ya elimu nchini Tanzania imekuwa inakuwa kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kiwango cha jumla cha kuandikisha watoto shule ya msingi kimepanda kwa asilimia 94, ongezeko hilo la kasi  linatokana na kufutwa kwa ada za shule ya msingi mwaka 2001  pamoja na maelekezo kutokana kwa serikali ambayo yaliagiza watoto wote walio na umri wa kuanza shule  wawe wameandikishwa kwa ajili ya kuanza elimu hiyo.

Mafanikio hayo  yamesababisha kuwepo kwa changamoto kadhaa  ikiwemo uhaba wa madawati. “Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania inahitaji madawati milioni 3.3 kwa ajili ya shule za msingi wakati madawati yaliyopo ni milioni 1.8. hivyo kuwepo kwa uhaba wa madawati milioni 1.5” alisema  aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Changamoto hiyo imelazimu kuchukuliwa kwa hatua  za makususdi, hivyo serikali ya awamu ya tano  chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli imeshaonesha nia yake ya kuwanyanyua  wanafunzi wote kutoka kukaa sakafuni  kwa kuwezesha kila darasa kuwa na madawati na hivyo kuboresha ubora wa elimu.

Katika kuunga mkono maamuzi hayo magumu ya Rais na wakati huo huo kuchangia katika  Lengo Endelevu ya Maendeleo namba 4 ambalo linayataka mataifa yote la kuhakikisha  elimu jumuishi na bora kwa wote pamoja na kukuza kuliko endelevu, Tigo ilijikita katika mradi uliofahamika kama Madawati kwa Shule za Umma. Mwaka 2015 peke yake tulitoa msaada wa madawati 2,000 kwa shule tofauti za msingi na hivyo kunufaisha wanafunzi 6,000 nchini kote. Mkakati huu uliendelea mwaka 2016 bega kwa bega na msimu wa tamasha la Tigo FIESTA 2016 ambapo madawati 5,700 yalitolewa kama msaada nchi nzima  kabla ya mwisho wa mwaka na hivyo kuwanyanyua  toka sakafuni zaidi ya watoto 17,000.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo