Digital Changemakers | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..
 Binafsi

Mkakati wa kidijitali wa waleta mabadiliko unatambua na  kusaidia wajasiriamali kijamii wa ndani kwa masuluhisho ya ubunifu ambayo yanalenga kuibadilisha jamii  kwa kutumia programu/teknolojia za kidijitali. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 kama Tigo Reach for Change na baadae kubadilishwa kuwa Digital Changemakers mwaka 2014 tumeshaweza kuwavutia  na kuchagua masuluhisho muhimu  ambayo yamekuwa na matokeo chanya kwa watoto na jamii kwa jumla.

Tumewekeza kwa watu binafsi ambao wanavutia kwa matokeo, wanapenda na wana sifa za kiujasiriamali na kuwapatia programu muhimu zinazohitajika katika  ubunifu wa suluhisho la matatizo yanayoikabili jamii. Digital Changemakers wanapewa msaada wa fedha na ufundi kupitia kituo chetu cha mfano na wanaunganishwa na washauri na wataalamu wa Tigo katika kuwasaidia  na kuendeleza miradi yao. Ifuatayo hapa chini ni orodha ya Changemakers wetu ambao wameshaweza  kuleta mabadiliko kwa watoto 15,000 katika maeneo tofauti kupitia miradi yao.

CAROLYNE  EKYARISIIMA   - APPS & GIRLS

Akiwa amelenga kuziba pengo la kijinsia katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) nchini Tanzania, Carolyne  anaendesha programu yake ya Apps & Girls ambayo inahamasisha na  kuwezesha watoto wa kike walio na umri wa miaka 10 hadi 18 kujifunza kompyuta na kuanzisha ubunifu wa kidijitali. Kwa kuanzisha klabu maalumu katika mashule  na kupitia matukio ya kama vile warsha, maonesho, kuweka makambi na mashindano asasi hii inaunda viongozi wanawake  wa baadaye nchini Tanzania. Kwa taarifa zaidi tembelea: http://www.appsandgirls.com/

BRENDA SHUMA - GABRIELLA CENTRE

Akiwa amehitimu katika Chuo Kikuu cha Tumaini katika shahada ya therapia ya viungo, Brenda-Deborah Shuma ambaye muasisi wa kituo cha Gabriella Children Rehab amewekaza muda na elimu yake katika  kuwalea watoto walio na mtindio wa ubongo pamoja na uoni hafifu. Brenda alishafanya kazi na Kituo cha YWCA Children Rehabilitation, ambapo alishiriki katika kuunda na kuanzisha wiki ya programu ya kina ya therapia kwa watoto walio na ulemavu. Ni mapenzi haya pamoja na uzoefu uliomshawishi  kufungua kituo cha  Gabriella Children Rehab mjini Moshi Tanzania. Kwa taarifa zaidi tembelea: http://www.gabriellarehab.org

FARAJA NYALANDU - SHULE DIRECT

Faraja ni mwanasheria, mwenye mapennzi katika kuhamasisha na kushughulikia haki za kijamii za watu. Anapendelea  masuala yanayohusu haki za watoto, elimu bora, kuwezesha wanawake na haki za binadamu. Ni muasisi mwenza wa Shule Direct  ambao ni ujasiriamali jamii  ukijielekeza  kushughulikia  kukabili ukosefu wa  vitabu vya kutosha katika shule za sekondari kwa kukusanya mada nzuri kutoka kwa walimu wenye sifa  na kuzifanya  kupatikana bure  kupitia mtandao.asasi hivyo inatoa fursa kwa wanafunzi nchini Tanzania  kujifunza na kutambua umuhimu wao. Kwa taarifa zaidi: www.shuledirect.co.tz/

JOAN AVIT- GRAPHOGAME TANZANIA

Kujifunza kusoma ni jambo muhimu katika uelewa, ubora wa elimu na kutokomeza umasikini. Hata hivyo  takribani theluthi mbili ya watoto nchini Tanzania  hadi kufikia darasa la pili wanakuwa hawana uwezo wa kusoma! Joan Avit kupitia mradi wake  Graphogame Tanzania ameanzisha mbinu ya kufundisha kidijitali ambayo inatumia mchezo katika simu ya mkononi  na kufundisha watoto wadogo kusoma katika maeneo ya vijijini mkoani Kilimanjaro. Kwa taarifa zaidi: http://info.graphogame.com/

THADEI MSUMANJE - MAJENGO KIDSYOUTH & TECHNOLOGY SCHOOL

Thadei Msumanje anaamini kwamba teknolojia ni programu yenye nguvu katika maendeleo ambayo inaweza kutumiwa  kuendeleza elimu duniani, maisha pamoja na afya. Kupitia asasi yake ya Majengo Kids Youth & Tech School, analikabili tatizo hili kwa kuileta teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa watoto  ndani ya jumuiya za vijijini. Amejumuisha kujifunza  Tehama  na miundo mingine ya kujifunza  kama vile shule za awali kwa kuhakikisha kwamba faida za Tehama katika hatua za kujifunza  zinapatikana kwa watoto wote katika maeneo ya vijijini Tanzania.

INNOCENT J SULLE- My Little Travelling Library

Uhaba wa kupata mada za masomo na kukosekana kwa utamaduni imara wa kujisomea kumechangia kuwepo kwa duru endelevu ya kutokujua kusoma  miongoni mwa watoto nchini Tanzania. Watoto wanashindwa kupata vitabu wanavyovipenda  kuwepo kwa tabia duni ya kusoma  ambayo ni sababu kubwa inayochangia  ufanisi duni katika masomo  katika shule za msingi nchini. Dhana ya Innocent James ya “Maktaba Yangu Ndogo Inayotembea” inajenga mtandao wa maktaba ya simu, inayowaletea watoto vitabu katika maeneo ya vijijini. Kupitia kazi hii Innocent analenga   kuhamasisha utamaduni  wa kujisomea miongoni mwa kizazi cha watoto, kuongeza viwango cha kujua kusoma kujitegemea katika kujifunza.

LEKA TINGITANA - eAfya

Leka Tingitana ni mtaalamu wa teknolojia mwenye mapenzi ya kuunda masuluhisho ya kidijitali dhidi ya matatizo katika sekta ya afya. Kupitia kampuni yake ya LX Technological Solutions for Africa, Leka alianzisha jukwaa la mawasiliano ya simu za mkononi la eAfya kusaidia  kuunda mtandao wa Jumuia ya Afya ya Wafanyakazi (CHW) ambao wako mstari wa mbele katika kusaidia kutoa huduma ya afya kwa kina mama wajawazito na kinamama wachanga. Ubunifu huu utatoa mchango muhimu katika kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wachanga nchini Tanzania.

NEEMA SHOSHO – AFYA SLICES

Asasi ya Afya Slices  inatumia programu za kidijitali kutoa taarifa za lishe  zikiwalenga kinamama, walezi na watoaji wa huduma za afya. Akiwa na lengo la kupunguza kiwango cha vifo vya watoto na utapiamlo miongoni mwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano, jukwaa la Afya Slices linalenga kutoa taarifa  kuhusu kutumia  vyakula vya asili na wanavyovimudu katika kuboresha lishe ya mtoto. Neeema alianzisha vigezo tofauti katika kuwezesha wazazi na walezi kupata taarifa kuhusu umri wa watoto wao. Kupitia simu za mkononi watumiaji wanaweza  kuingia katika namba maalum za utambulisho ambazo zitawapatia taarifa sahihi za lishe  kwa vigezo wanavyokuwa wamevichagua.

EDWARD SIMON BIHAGA – UMOJA WA WAWEZESHAJI

 Edward ni mwanaharakati aliyepania kutokomeza ajira mbaya kwa watoto mkoani Kigoma nchini Tanzania na hata nje. Akitumia asasi yake ya Umoja wa Wawezeshaji, Edward anaziweka mada za kielimu kuhusu ajira za watoto kidijitali kwa ajili ya kuzisambaza  kupitia ujumbe mfupi wa maneno na hivyo kuibua uelewa  kuhusu ajira za watoto. Asasi yake pia  inapanga  kuokoa watoto  wanaotumikishwa kiutumwa na kuwawezesha wazazi wao kupitia shughuli za kiuchumi na kijamii ili kupunguza athari dhidi ya watoto kuondokana tena katika  ajira za kulazimishwa pamoja na kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu kupata elimu.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo