Supa Nyota | Tigo Tanzania
 Binafsi

Vigezo na Masharti vya promosheni ya “SUPA NYOTA”

1. Vigezo na Masharti

a. Promosheni ya Supa Nyota ni kwa wateja wa Tigo wa malipo ya awali tu

b. Muda wa promosheni: 29 Septemba mpaka 24 Novemba 2018.

c. Kila mteja atakae rekodi wimbo wake kushiriki kwenye SupaNyota atahitaji kutafuta kura kuweza kushiriki kwenye shindano la SupaNyota. Mwenye pointi nyingi ataweza kuingia kwenye ushiriki wa SupaNyota kwa kila mkoa ambao Tamasha la Fiesta litafanyika. Kwa Kila wimbo Mteja akirekodi itagarimu shs 100 kwa wimbo na kwa Kila Kura ya ujumbe itagarimu shs 50.

WINNER SELECTION:

• Uchaguzi wa mshindi utatokana na kura atakazo pigiwa kwenye wimbo aliorekodi.

• Kwenye kila mkoa wa Fiesta kutakuwa na mshindi mmoja ambaye atapata nafasi ya kushiriki SupaNyota. Kura zinaweza kupigwa mpaka mwisho wa Tamasha la Fiesta kwa kila mkoa.

• Kuchagua washindi na kuwataarifu kutafanyika katika uwepo wa majaji wa kutoka Tigo na Clouds FM.

• Washiriki wote wa “SUPANYOTA - FIESTA-Star” watachaguliwa kutokana na idadi ya kura watakazo pigiwa kwenye nyimbo zao. Mshiriki mwenye kura nyingi atapata nafasi ya kushiriki katika kutafuta mshindi wa SupaNyota wa mkoa husika kutokana na kalenda ya Tigo Fiesta pia mshiriki atattangazwa kwenye tovuti www.tigofiesta.co.tz or www.tigo.co.tz

Jinsi ya Kushiriki na Kupiga Kura:

IVR:

a. Mshiriki ataweza rekodi wimbo wake wa ushiriki kwa kupiga BURE nambari 0901656568 kisha kuchagua lugha, atapata maelezo ya kufwata ili kuweza kurekodi atabonyeza namba 1, baada ya kurekodi na kuweka wimbo. Mshiriki atapata nambari ya ushiriki ambayo anaweza kutumia kupigiwa kura na Ndugu, Jamaa na Marafiki kupata kura nyingi Zaidi.

b. Kupiga kura piga nambari 0901656568 baada ya kuchagua lugha, mteja atafwata maelekezo ambayo yatamuelekeza jinsi ya kupiga kura.

Portal:

a. Mteja anaweza kujirekodi kwa kutembelea http://tigofiesta.co.tz, na kwenda kwenye menyu ya SUPANYOTA kuboneyza “Kurekodi Wimbo Wako”, Baada ya kujirekodi anaweza kuweka/kuhifadhi wimbo wake kwenye portal na pia naweza kuona wimbo wake kwenye menyu ya Kurekodi, post the song on Portal and he can see his song inside Kurekodi Menu, Mshiriki atapata nambari ya ushiriki ambayo anaweza kutumia kupigiwa kura na Ndugu, Jamaa na Marafiki kupata kura nyingi Zaidi.

b. Mteja anaweza kurekodi Nyimbo nyingi.

c. Marafiki na familia wanaweza kupiga KURA kupitia Portal http://tigofiesta.co.tz wakiingia kwenye menyu ya SUPANYOTA

Ujumbe wa SMS:

a. Marafiki na familia wanaweza kupiga KURA kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika KURA ikifwata na nambari ya mshiriki kwenda 15571, mfano: KURA 22334 kwenda 15571

Taarifa zinginezo:

a. Majina ya washindi,picha na video za washindi wa zawadi kupitia promosheni ya “Supa Nyota” watakuwa wakitangazwa kupitia vyombo vya habari.

b. Kwa kushiriki, mshindi anaipatia kampuni ya Tigo haki ya kumtangaza na kutumia jina, picha na video ya mhusika kama mshiriki na mshindi kwenye vyombo vya habari kwa kipindi chote cha promosheni hii.

c. Wafanyakazi wa kampuni za Tigo na Telecovas na familia zao hawaruhusiwi kushiriki kwenye promosheni hii.

d. Promosheni hii ni kwa ajili ya watanzania na wageni wenye vibali vya ukazi (residence permits) tu.

e. Majina ya washindi yatatangazwa kwenye vyombo vya habari vitakavyochaguliwa.

f. Namba na idadi za wateja walioshiriki promosheni hii yatakuwa katika taarifa na kumbukumbu za kampuni ya Tigo, Telecovas na clouds.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo