Ndio, huduma zote muhimu za Tigo Pesa zinapatikana kama ilivyo kwenye Tigo Pesa ya kawaida. Kama vile
Ndio, utatumia namba ya siri ile ile unayotumiaga ukipiga *150*01#.
Ndio,unaweza kutumia ukiwa mtandao wowote, unahitaji tu kuhakikisha namba yako ya Tigo ipo kwenye simu yako wakati wa usajili. Baada ya hapo unaweza kutumia Tigo Pesa App ukiwa mtandao wowote.
Mteja ataweza kupata App hiyo kwenye App store au tembele tovuti yetu ya Tigo kupata jinsi ya kupakua.
Link inapatika kwenye meseji tunazotumia wateja au kwenye tovuti yetu ya Tigo. Au tembelea App Store yako kupakua App ya Tigo Pesa.
Inachukua dakika chache na pia inategemea na Intaneti yako.
Hapana makato ni yale yale kama ya kawaida ya Tigo Pesa.
Makato ni ya kawaida kama ya kudownload App nyingine.
Kama itatokea unapata tatizo angalia kama umeunganishwa na Intaneti au wasiliana na huduma kwa wateja kwa msaada zaidi.
Unahitaji Intaneti na simu ya yenye IOS au Android namba yako ya Tigo iliyosajiliwa Tigo Pesa
Wasiliana na huduma kwa wateja kwa msaada zaidi na utaweza kuendelea kuitumia huduma kwenye simu nyingine kama kawaida na pesa zako zitakuwa salama maana kila muamala unahitaji namba ya siri.
Hapana, pesa zako zitakuwa salama, mtu atahitaji namba yako ya siri kutumia Tigo Pesa yako. Ndio maana ni muhimu kutomwambia mtu yoyote namba yako ya siri.
Unaweza kutembele tovuti yetu ya Tigo na kuangalia ni simu gani zinaweza kukubali APP hii.
Unaweza kureseti PIN yako kwa kupiga simu Huduma kwa wateja au kutembelea ofisi zetu za Tigo.
Ndio,unaweza kutumia App hii kokote Tanzania, unahitaji tu kuwa na Internet, WiFi/Data na vile vile unaweza kutumia mahali popote ulimwenguni , kama kawaida unahitaji internet kuweza kutumia APP hii.
Application ipo katika lugha mbili, English na Kiswahili kumwezesha mteja kuweza kutumia huduma hii kwa lugha ambayo yuko vizuri nayo.
Ndio, inawezekana kuzihifadhi kumbukumbu namba kila mwisho wa muamala wako
App hii ina usalama wa kisasa kukulinda wewe kama mteja, lakini tunapenda kukumbusha umuhimu wa kutompa mtu PIN yako ya Tigo Pesa na kujua kuwa Wafanyakazi wa Tigo hawatohitaji namba yako ya Siri kwa matumizi yoyote.
Ndio utaweza tumia Tigo Pesa ya zamani na Application.
Ndio unaweza kuweka hii application kwenye simu nyingi na utaweza kuitumia kwenye zote kwa wakati mmoja, na utaweza kuangalia simu zote ambazo umesijali kwenye Application, na vile vile unaweza kuzitoa na kubaki na moja. Hakikisha tu namba yako ya Tigo unayotaka kutumia ipo ndani ya simu yako wakati wa usajili
A. Watumiaji wa Android
B.Mtumiaji wa IOS
Hakimiliki © 2019 - Tigo Tanzania