Bima Mkononi | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Bima Mkononi

Bima Mkononi - Bima Binafsi kwa Wateja wa Tigo Pesa

Upatikanaji wa bima ya maisha, hospitali na ajali imerahisishwa. Bima Mkononi inawawezesha wateja wa Tigo kujiunga na bima kiurahisi na kwa karaka kwa kupitia simu zao. Ukijiunga, furahia gharama moja pekee tu kwa watu wote walio kati ya umri wa miaka 18 - 65. Kujiunga inachukua dakika chache tu na unaweza kulipa kwa kupitia Tigo Pesa au kwa kulipa pesa taslimu kwenye kituo chochote cha Tigo huduma kwa wateja.


Jinsi ya kujiunga:

 1. Chagua bima unayohitaji, gharama na muda wa kudumu kati ya hizo zilizoorodheshwa hapo chini.
 2. Piga *148*15# na ufuate maelekezo

Tupigie simu bure huduma kwa wateja 0659 071 001 kwa maelezo zaidi, msaada na madai ya fidia.


Aina za Bima na Gharama:

 1. Bima Mkononi ya Kulazwa:

Fidia hadi Tsh 2,200,000

Bima Mkononi ya Kulazwa inakulinda wewe na Watoto mpaka watano kutokana na kulazwa, kwa kukulipa Tsh 40,000 kwa kila usiku mmoja kwa aliyelazwa, kufikia ukomo wa siku 55 au Tsh 2,200,000 kwa mwaka.

Bei ya Bima:

Huduma

Gharama

Kiwango cha Ulinzi

Mtu Mzima 1

TZS 1,500

Siku 30 au TSh 1,200,000

Mtu Mzima 1 + Mtoto 1

TZS 2,250

Siku 35 au TSh 1,400,000

Mtu Mzima 1 + Watoto 2

TZS 3,000

Siku 40 au TSh 1,600,000

Mtu Mzima 1 + Watoto 3

TZS 3,750

Siku 45 au TSh 1,800,000

Mtu Mzima 1 + Watoto 4

TZS 4,500

Siku 50 au TSh 2,000,000

Mtu Mzima 1 + Watoto 5

TZS 5,250

Siku 55 au TSh 2,200,000

Madai:

 • Utalipwa fidia baada ya kulazwa na kulipa gharama katika hospitali yoyote Tanzania inayolaza wagonjwa kwa siku isiyopungua moja.
 • Toa Taarifa ndani ya siku 120 baada ya kulazwa hospitali.
 • Malipo yatatumwa kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupokea nyaraka zifuatazo: Kitambulisho, Fomu ya Kulazwa – yaani discharge summary*, Cheti cha kuzaliwa cha mtoto iwapo mtoto amelazwa au barua ya serikali ya mtaa iwapo mtoto sio wa kumzaa.

*Ripoti ya daktarin na risiti yenye mchanganuo wa malipo itahitajika kwa mtu mzima au mtoto aliyelazwa kwa zaidi ya Siku 5.

Madai yasiyolipwa:

Majeraha ya kujitakia, kujiua, kujihusisha na vurugu, matumizi mabaya ya vilevi au matibabu yasiyo ya lazima, mfano: Upasuaji wa urembo.


2- Bima Mkononi ya Ajali Binafsi

Fidia hadi Tsh 3,000,000

Bima Mkononi ya Ajali Binafsi inakulinda na kifo, ulemavu wa kudumu na kulazwa hospitalini kutokana na ajali. Ukifikwa na umauti, mtegemezi wako atapokea Tsh 3,000,000.

Ikiwa utapata ulemavu wa kudumu, kiwango cha fidia kitategemea aina ya ulemavu. Ikiwa umelazwa kutokana na ajali, utapokea Tsh 30,000 kwa kila usiku ambao utalazwa hospitali.

Bei ya Bima:

Tsh 1,000 kwa mwezi

Madai:

 • Malipo yatatumwa kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupokea nyaraka zifuatazo: Kitambulisho, Cheti cha Kifo, au Ripoti ya daktari inayoonyesha sababu ya ulemavu. Ikiwa umelazwa, ambatanisha ripoti ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, kitambulisho na risiti.

Madai yasiyolipwa:

 • Majeraha ya kujitakia, kujiua, kujihusisha katika vita, matumizi mabaya ya vilevi au madawa ya kulevya
 • Matatizo ambayo tayari mdai anayo.
 • Matibabu yasiyo ya lazima yaliyochaguliwa na mgonjwa mfano upasuaji wa urembo.
 • Matibabu baada ya tukio (yasiyotokana moja kwa moja na ajali)

3- Bima Mkononi ya Maisha:

Fidia hadi TSh 1,000,000

Bima Mkononi ya Maisha inakulinda wewe na mtegemezi uliyemchagua. Ukifikwa na umauti, mtegemezi wako atapokea Tsh 1,000,000. Ikiwa mtegemezi wako atafariki utapokea TSh 500,000

Bei ya Bima:

TSh 1,500 kwa mwezi

Madai:

 • Toa taarifa ya madai ndani ya siku 90 baada ya kifo cha aliyechukuliwa bima
 • Malipo yatatumwa kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupokea nyaraka zifuatazo: Kitambulisho na Cheti cha kifo au Ripoti ya Daktari inayoonyesha sababu ya kifo au kibali cha mazishi.

Madai yasiyolipwa:

 • Majeraha ya kujitakia, kujiua, kujihusisha katika vita, matumizi mabaya ya vilevi au madawa ya kulevya.

 

Maswali ya Mara kwa Mara:

  Je, najiungaje kwenye huduma hii?

Unaweza kujiunga na Bima Mkononi kwa kupiga *148*15# au fika duka lolote la Tigo kwa msaada zaidi. Pia unaweza kupiga simu huduma kwa wateja namba 0659 071001 bure kwa maelezo zaidi.

  Naweza kutibiwa hospitali zipi/gani?

Unaweza kutibiwa hospitali yoyote Tanzania ambayo inalaza wagonjwa. Baada ya kulazwa, utahitajika kutuma madai yako ya fidia huku ukiambatanisha nyaraka muhimu. Kumbuka hii ni bima ya kulazwa tu, na haitoi fidia kwa matibabu ya kawaida ya afya bila ya kulazwa.

  Vipi kuhusu kitambulisho au kadi ya Bima?

Huhitaji kitambulisho kwa ajili ya Bima hii, namba yako ya simu ndio kitambulisho cha uanachama. Hivyo, pindi unapofanya madai ni muhimu kutaja namba yako ya simu iliyosajiliwa kwani malipo ya fidia yatatumwa kwenye namba hiyo.

  Mbona huduma ya kulazwa pekee?

Huduma yetu inalenga kufidia kwa kiasi kipato ambacho mteja angeweza kupata endapo angekuwa mzima akifanya shughuli au majukumu yake ya kiuchumi, hivyo ndio maana tumelenga kwenye kipengele cha maradhi yanayopelekea kulazwa pekee.

  Aina za Bima

Tuna bima za aina tatu.

 1. Bima ya Ajali Binafsi - inakulinda iwapo utapata ulemavu wa kudumu au kifo kutokana na ajali
 2. Bima ya Maisha - inakulinda wewe na mtegemezi wako, iwapo mmoja wenu atapata umauti
 3. Bima ya Kulazwa - inakulinda kwa kufidia gharama iwapo utaumwa na kulazwa hospitali.
  Muda wa kusubiri

Unapojisajili na kufanya malipo, muda wa kusubiri kabla ya kuweza kudai fidia ni:

Bima Mkononi ya Maisha - siku 30.

Bima Mkononi ya Ajali Binafsi - Siku 1 tu.

Bima Mkononi ya Kulazwa - siku 30 baada ya kujiunga. Lakini kwa maradhi ambayo tayari mgonjwa anayo kabla ya kujiunga au magonjwa sugu, muda wa kusubiri ni miezi 6. Kwa madai ya uzazi/kujifungua, muda wa kusubiri ni miezi 9.

  Nitapata fidia gani iwapo sitaumwa mwaka mzima?

Bima Mkononi ya kulazwa imeandaliwa kutoa fidia kutokana na matibabu ya kulazwa. Iwapo haujalazwa katika kipindi chote cha bima, hakuna fidia itakayotolewa. Bima hii ni ulinzi kwako iwapo utapatwa tatizo na kulazwa au kupata ulemavu au kupoteza uhai.

  Bima hii ni ya watu wangapi?

Bima za Ajali na Maisha ni za mtu mmoja mmoja, isipokuwa mtu mwengine anaweza kupata fidia kutokana na Bima yako pindi unapomuandikisha kama mtegemezi. Ila Bima ya Kulazwa inaruhusu kuongeza watoto hadi 5 wenye umri wa miaka kati ya 1 na 17, kama sehemu ya nyongeza ya bima kuu ya mtu mzima.

Vigezo na Masharti ( Bima Mkononi ya Kulazwa ):

 • Tarehe ya kuanza: Siku 30 baada ya kujisajili

 • Umri unaorushiwa (Watu Wazima): Miaka 18 - 64

 • Umri unaorushiwa (Watoto): Mwaka 1 – Miaka 17

 • Muda wa kusubiri ni miezi 6 kwa maradhi ambayo tayari mtumiaji anayo au magonjwa sugu.
 • Muda wa kusubiri ni miezi 9 kwa madai ya Uzazi/Kujifungua.

Vigezo na Masharti ( Bima Mkononi ya Ajali Binafsi ):

 • Tarehe ya kuanza: Siku moja baada ya kujisajili.
 • Umri unaorushiwa: Miaka 18 - 64

Vigezo na Masharti ( Bima Mkononi ya Maisha ):

 • Tarehe ya kuanza: Siku 30 baada ya kujisajili
 • Umri unaorushiwa: Miaka 18 - 64

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo