Bima Mkononi FAQs | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..


Bima Mkononi FAQs

Unaweza kujiunga na Bima Mkononi kwa kupiga *148*15# au fika duka lolote la Tigo kwa msaada zaidi. Pia unaweza kupiga simu huduma kwa wateja namba 0659 071001 bure kwa maelezo zaidi.

Unaweza kutibiwa hospitali yoyote Tanzania ambayo inalaza wagonjwa. Baada ya kulazwa, utahitajika kutuma madai yako ya fidia huku ukiambatanisha nyaraka muhimu. Kumbuka hii ni bima ya kulazwa tu, na haitoi fidia kwa matibabu ya kawaida ya afya bila ya kulazwa.

Huhitaji kitambulisho kwa ajili ya Bima hii, namba yako ya simu ndio kitambulisho cha uanachama. Hivyo, pindi unapofanya madai ni muhimu kutaja namba yako ya simu iliyosajiliwa kwani malipo ya fidia yatatumwa kwenye namba hiyo.

Huduma yetu inalenga kufidia kwa kiasi kipato ambacho mteja angeweza kupata endapo angekuwa mzima akifanya shughuli au majukumu yake ya kiuchumi, hivyo ndio maana tumelenga kwenye kipengele cha maradhi yanayopelekea kulazwa pekee.

Tuna bima za aina tatu.

  1. Bima ya Ajali Binafsi - inakulinda iwapo utapata ulemavu wa kudumu au kifo kutokana na ajali
  2. Bima ya Maisha - inakulinda wewe na mtegemezi wako, iwapo mmoja wenu atapata umauti
  3. Bima ya Kulazwa - inakulinda kwa kufidia gharama iwapo utaumwa na kulazwa hospitali.

Unapojisajili na kufanya malipo, muda wa kusubiri kabla ya kuweza kudai fidia ni:

Bima Mkononi ya Maisha - siku 30.

Bima Mkononi ya Ajali Binafsi - Siku 1 tu.

Bima Mkononi ya Kulazwa - siku 30 baada ya kujiunga. Lakini kwa maradhi ambayo tayari mgonjwa anayo kabla ya kujiunga au magonjwa sugu, muda wa kusubiri ni miezi 6. Kwa madai ya uzazi/kujifungua, muda wa kusubiri ni miezi 9.

Bima Mkononi ya kulazwa imeandaliwa kutoa fidia kutokana na matibabu ya kulazwa. Iwapo haujalazwa katika kipindi chote cha bima, hakuna fidia itakayotolewa. Bima hii ni ulinzi kwako iwapo utapatwa tatizo na kulazwa au kupata ulemavu au kupoteza uhai.

Bima za Ajali na Maisha ni za mtu mmoja mmoja, isipokuwa mtu mwengine anaweza kupata fidia kutokana na Bima yako pindi unapomuandikisha kama mtegemezi. Ila Bima ya Kulazwa inaruhusu kuongeza watoto hadi 5 wenye umri wa miaka kati ya 1 na 17, kama sehemu ya nyongeza ya bima kuu ya mtu mzima.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo