Bustisha | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..


 Bustisha

Bustisha:

Bustisha ni huduma ya mkopo wa Kifedha inayokuwezesha kukamilisha miamala yako ya Tigo Pesa ikiwa hauna fedha za kutosha kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa. Wateja wote wa Tigo Pesa wanastahili kupata huduma hii, lakini watalazimika kwanza kujisajili na kukubali kutumia huduma kupitia menyu ya Tigo Pesa au kwenye App ya Tigo Pesa.

Baada ya muamala kushindikana, mteja aliyejisajili atapokea taarifa ya kikomo cha Bustisha wanachotakiwa kuongezewa ili kukamilisha muamala huo, na ombi la idhini yake ya kutumia huduma hii. Baada ya mteja kukubali, muamala utakamilika na fedha zitatumwa moja kwa moja kwa mlengwa. Mteja akikataa, muamala utakataliwa na mteja atapewa taarifa ya kutokuwa na salio la kutosha.

Mteja anatarajiwa kurejesha pesa aliyoongezewa baada ya kuweka au kupokea pesa kwenye akaunti yake ya Tigo Pesa.


Muundo Wa Gharama:

Kuna aina mbili za gharama itayotozwa kwa mteja anayetumia huduma ya Butisha.

1. Riba ya mara moja:

Riba hii inatozwa kila wakati unapochukua mkopo wa Bustisha kulingana na viwango vilivyooneshwa hapa chini:

Viwango/Siku Riba ya mara moja
1-1000 5.70%
1001-3000 6.00%
3001 - 4000 6.20%
4001 - 10000 6.90%
10001 - 20000 6.20%
20001 - 30000 5.70%
30001 - 40000 5.00%
40001 - 50000 4.50%

2. Riba ya kila siku:

Hii ni riba ya kila siku ambayo mteja atatakiwa kulipia kila siku itayopita bila kurudisha kiasi cha Bustisha aliopewa. Riba hii itaendelea kulimbikizwa kila siku mteja akikosa kulipa deni la Bustisha hadi siku ya 16 ambapo Riba itapunguzwa hadi siku ya 30. Baada ya Siku ya 30, Kiasi kilichosalia hakitahususha Riba yoyote ya ziada.

Riba inatozwa kulingana na viwango na idadi ya siku kama vilivyooneshwa hapa chini:

Viwango/Siku

VIWANGO VYA RIBA

Siku ya Mkopo

Siku 2' - 5

Siku 6' - 10

Siku 11' - 15

Baada ya siku 16

5.30%

6.80%

10.30%

14.30%

15.80%

 1001 - 3000

5.60%

7.10%

10.60%

14.60%

16.10%

 3001 - 4000

5.80%

7.30%

10.80%

14.80%

16.30%

 4001 - 10000

6.50%

8.00%

11.50%

15.50%

17.00%

10001 – 20000

5.80%

7.30%

10.80%

14.80%

16.30%

20001 – 30000

5.30%

6.80%

10.30%

14.30%

15.80%

30001 – 40000

4.60%

6.10%

9.60%

13.60%

15.10%

40001 – 50000

4.20%

6.00%

9.00%

13.20%

15.00%

Muongozo Wa Utumiaji Kwa USSD:

Jinsi ya Kujiunga

•         Piga *150*01#

•         Chagua 7 Huduma za Kifedha

•         Chagua 4 Mikopo

•         Chagua 2 Bustisha

•         Kubali Vigezo na Masharti

•         Ingiza namba ya siri Kuthibitisha

Kuangalia Kiwango cha Bustisha

•         Piga *150*01#

•         Chagua 7 Huduma za Kifedha

•         Chagua 4 Mikopo

•         Chagua 2 Bustisha

•         Chagua 2 Kiwango cha Bustisha

•         Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Kulipa Deni Kamili

•         Piga *150*01#

•         Chagua 7 Huduma za Kifedha

•         Chagua 4 Mikopo

•         Chagua 2 Bustisha

•         Chagua 1 Kulipa Deni

•         Chagua 1 Kulipa deni Kamili

•         Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Kulipa Deni Kiasi

•         Piga *150*01#

•         Chagua 7 Huduma za Kifedha

•         Chagua 4 Mikopo

•         Chagua 2 Bustisha

•         Chagua 1 Kulipa Deni

•         Chagua 1 Kulipa deni Kiasi

•         Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Kuangalia Kiasi Unachodaiwa

•         Piga *150*01#

•         Chagua 7 Huduma za Kifedha

•         Chagua 4 Mikopo

•         Chagua 2 Bustisha

•         Chagua 3 kiasi unachodaiwa

•         Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Jinsi ya Kujitoa

•         Piga *150*01#

•         Chagua 7 Huduma za Kifedha

•         Chagua 4 Mikopo

•         Chagua 2 Bustisha

•         Chagua 5 Kujitoa

•         Ingiza namba ya siri Kuthibitisha

•         Kisha fuata maelekezo.

Muongozo Wa Utumiaji Kwa kutumia Tigo Pesa App:

Jinsi ya Kujiunga

•         Fungua App ya Tigo Pesa

•         Chagua Huduma za Kifedha

•         Chagua Mikopo

•         Chagua Bustisha

•         Kubali Vigezo na Masharti

•         Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Kuangalia Kiwango cha Bustisha

•         Fungua App ya Tigo Pesa

•         Chagua Huduma za Kifedha

•         Chagua Mikopo

•         Chagua Bustisha

•         Chagua Kiwango cha Bustisha

•         Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Kulipa Deni

•         Fungua App ya Tigo Pesa

•         Chagua Huduma za Kifedha

•         Chagua Mikopo

•         Chagua Bustisha

•         Chagua Lipa Deni

•         Ingiza namba ya siri

•         Weka Kiasi

•         Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Kuangalia Kiasi Unachodaiwa

•         Fungua App ya Tigo Pesa

•         Chagua Huduma za Kifedha

•         Chagua Mikopo

•         Chagua Bustisha

•         Chagua Kiasi Unachodaiwa

•         Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Jinsi ya Kujitoa

•         Fungua App ya Tigo Pesa

•         Chagua Huduma za Kifedha

•         Chagua Mikopo

•         Chagua Bustisha

•         Chagua Kujitoa

•         Ingiza namba ya siri Kuthibitisha

•         Kisha fuata maelekezo.


Maswali na Majibu:

  Bustisha ni nini?

Hii ni huduma ya mkopo ambayo inayomuwezesha wateja wa Tigo Pesa kukamilisha miamala yao ya Tigo Pesa ikiwa hawana fedha za kutosha kwenye akaunti zao za Tigo Pesa. Baada ya kujiunga, Unachohitaji ni kufanya miamala ya Tigo Pesa na kama huna fedha za kutosha, Bustisha itaitakuongezea kiasi ulichopungukiwa.

  Ni kiasi gani cha chini na cha juu ninachoweza kuongezewa kwa kutumia BUSTISHA?

Viwango vya Bustisha ni kati ya TZS 1 - 50000, Wateja watatengewa viwango tofauti kulingana na utumiaji wao wa huduma za Tigo Pesa na urejeshaji wa madeni ya Bustisha kwa wakati.

  Nani anastahili kujiunga na huduma ya Bustisha?

Watumiaji wote wa Tigo Pesa kuanzia miezi 6 na kuendelea, wanastahili kufurahia huduma ya Bustisha, wanahitaji tu kujiunga na huduma kupitia menyu ya Tigo Pesa au kwa kupitia Tigo Pesa App.

  Je, ni miamala gani ya Tigo Pesa ninayoweza kukamilisha kwa kutumia huduma ya BUSTISHA?

Ukiwa na Bustisha sasa unaweza kukamilisha miamala ifuatayo ya Tigo Pesa hata bila fedha ya kutosha; Kutuma pesa kwenda mitandao yote, Malipo ya Bili, Malipo ya Serikali, Kununua Muda wa Maongezi, Malipo ya Wafanyabiashara (Lipa Kwa Simu), Malipo ya Master Pass.

  Je, nitajuaje taarifa zangu za Bustisha?

Piga *150*01#, chagua (7) huduma za kifedha, chagua (4) mikopo, chagua (2) Bustisha, hapo utaweza, kulipa deni lako, kuangalia kiwango chako cha Bustisha, kuangalia kiasi unachodaiwa, vigezo na masharti, au kujiondoa kwenye huduma. Utapokea SMS ya uthibitishaji yenye maelezo kwa kila chaguo.

Au

Fungua App ya Tigo Pesa, Chagua Huduma za Kifedha, Chagua Mikopo, Chagua Bustisha, hapo utaweza Kulipa Deni, Kuangalia Kiwango chako cha Bustisha, Kuangalia Kiasi unachodaiwa, vigezo na masharti, au kujiondoa kwenye huduma. Utapokea SMS ya uthibitishaji yenye maelezo kwa kila chaguo.

  Nitatozwa kiasi gani kwa kutumia Bustisha?

Kuna aina mbili za malipo kwa huduma za Bustisha, riba ya mara moja na riba ya kila siku. Tafadhali tembelea tovuti yetu www.tigo.co.tz kwa maelezo zaidi kuhusu gharama za Bustisha.

  Je, ninaweza kurudisha muamala na kurejesha pesa zangu ikiwa nilituma/kulipa kimakosa kutumia Bustisha?

Mchakato wa kubadilisha Tigo Pesa unatumika mradi tu mpokeaji hajatumia fedha hizo. Hata hivyo, gharama za Tigo Pesa, na Bustisha hazitorudishwa.

  Je, ni mara ngapi ninaweza kutumia huduma ya Bustisha?

Idadi ya miamala itategemea na kiwango chako cha Bustisha.

  Je, nitalipaje deni langu la ziada ya Bustisha?

Wateja wenye deni la BUSTISHA la zaidi ya siku 3 (saa 72) makato yatafanyika moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao za Tigo Pesa wanapoweka au kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa. Wale wenye deni la chini ya siku 3 (saa 72) wanaweza kulipa deni kwa hiari yao kwenye akaunti zao za Tigo Pesa.

  Je, ninaweza kulipa deni kiasi?

Ndio unaweza. Ni bora kulipa angalau sehemu ya deni pale unapoweza, kwa sababu hii itafanya ada yako ya Kuchelewa kwa malipo kuwa ndogo.

  Kwa nini siwezi kupata mkopo wa Bustisha?

Zifuatazo zaweza kuwa kati ya sababu:

  • Hujajisajili kwenye huduma ya Bustisha
  • Umemaliza kiwango chako cha Bustisha
  • Muamala wako umevuka kiwango cha Bustisha ulichopangiwa.
  • Muamala unaofanya hauwezi kukamilishwa na huduma ya Bustisha.
  Je! Ni vipi Naweza kupata msaada?

Tafadhali, Piga 100 kuwasiliana na Huduma Kwa Wateja kwa msaada zaidi.

  Je nini kitatokea endapo nimetumia Bustisha na muamala haujakamilika?

Iwapo mteja ametumia mkopo wa Bustisha kukamilisha muamala na huduma haikukamilika, muamala utarejeshwa na mkopo wa Bustisha hautakuwa umetumika. Mkopo wa Bustisha utaanza kutumika pindi tu utakapopokea huduma au muamala ambao haujakamilika utakapopatiwa ufumbuzi.

Vigezo na Masharti:

 

Bonyeza link  www.tigo.co.tz/sw/vigezo-na-masharti/bustisha

    Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

    Tafuta duka la Tigo