TAARIFA KWA UMMA:
Ndugu Mteja,
Tigo Tanzania tunapongeza juhudi za kitaifa zinazoendelea kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19. Tunachukua nafasi hii kuwahimiza wateja wetu kupunguza mikusanyiko ya aina yoyote.
Tunafatilia kwa ukaribu maagizo yaliyotolewa na Serikali ya Tanzania ili kuzuia usambaaji wa virusi vya ugonjwa huu. Lengo letu ni kuhakikisha tunaendelea kuwahudumia wateja wetu nchi nzima huku tukihakikisha usalama wa wafanyakazi wetu na jamii kwa ujumla unazingatiwa.
Tumeweka vifaa vyote vya usafi katika maduka yetu, hii ni katika kuchukua hatua za kiusalama kuhakikisha unakuwa salama wakati unaendelea kuhudumiwa. Zaidi ya hilo, katika maduka yetu yote tumeweka vimiminika vitakatishi (sanitizer) ili kuweka mikono yako safi.
Tunawahamisha wateja wetu wote waendeleae kutumia mifumo yetu ya kidijitali ikiwamo kituo chetu cha huduma kwa wateja, WhatsApp, Facebook, Twitter na Instagram kwaajili ya kupata huduma zetu.
Pia, tunaomba kila mtu atumie Tigo Pesa na mifumo mengine ya malipo ya kimtandao nchi nzima kwaajili ya kupunguza athari za kusambaza virusi baada ya kushika noti.
Tutaendelea kuwahabarisha kuhusu maendeleo yoyote yanayo husiana na huduma zetu na tahadhari tunazochukua kuhakikisha unaendelea kupata huduma zenye ubora katika kipindi hiki.
Kuwa na amani kwamba vitengo vyetu mbalimbali vipo tayari kutoa huduma iliyobora kwa wateja wetu wote.
Tigo Tanzania.