Ikichukuliwa kama teknolojia nzuri ya hivi karibuni kwenye sekta Ya mawasiliano duniani isiyo na dosari katika kuifikia huduma ya intaneti, teknolojia ya 4G LTE ina kasi takribani mara tano ikilinganishwa na teknolojia ya 3G ambayo inatumiwa na watoaji wengine wahuduma hiyo kwenye sokola Tanzania.
Akizungumza kwenye mahoajiano maalum na vyombo vya habari kwenye ofisi za Tigo mjini Moshi pempezoni mwa uzinduzi rasmi wa mbio za kila mwaka za masafa za Kilimanjaro Marathon, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha alisema kusambazwa kwa mtandao wa 4G kunafanyika ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo wa kuwapatia wateja wake huduma ya hali ya juu duniani ili kuwawezesha kuendesha maisha ya kidijitali.
“Mpango wa kupanua mtandao wa Tigo wa 4G hadi Moshi kwa mara nyingine umeonesha sio tu kwamba Tigo inaongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye soko, bali pia kujikita kwake Kuongeza kufikiwa kwa intaneti kwa Watanzania wengi kadri iwezekanavyo,” alisemaWanyancha na kubainisha kuwa kuwa lengo kubwa la kampuni hiyo ya simu ni kuhakikisha huduma hiyo inaenean nchi nzima ifikapo mwishoni mwa mwaka huu2016.
Akizungumzia mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo Tigo ni mdhamini mwenza, Wanyancha alisema kwamba kama kampuni ya maisha ya kidijitali Tigo imeamua Kuwaunga mkono wanamichezo waume kwa wake hapa nchini ili kuwasaidia kufikia malengoyao ya muda mrefu katika maisha.
Wanyancha alihitimisha kuwa tangu mwaka jana Tigo ilishawekeza dola milioni 120 kwa mwaka kwenye upanuzi wa mtandao wake pamoja na kuboresha maeneo ya mitandao ya 4G na 3G na mkongo wamawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadiya kufikiwa kwa huduma kwa wateja nchi nzima.