Msaada upo katika mwitiko kwa wito wa serikali kwa mashirika, watu binafsi na watu wenye mapenzi mema kwa ajili ya kusaiidia waathirika wa janga hilo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa mjini Bukoba, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya aliwafariji waathirika wa tetemekeo hilo na kuwahakikishia kuwa Tigo siku zote iko tayari kutoa msaada pindi unapohitajika na jamii.
“Tunaeleza masikitiko yetu kwa waathirika wa tetemeko la ardhi na tunawatakia wote waliojeruhiwa kupona haraka. Ni matumaini yetu kwamba hivi karibuni wote katika maeneo yaliyoathirika wataweza kupata ahueni kutokana athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuendelea na maisha kama kawaida,” alisema Maswanya.
Maswanya alithibitisha tena kujikita kwa kampuni hiyo ya simu katika kuungana na serikali pamoja na watu walio na mtazamo unaofanana katika kuisaidia jamii katika maeneo ambako Tigo inaendesha shughuli zake.
Maswanya aliongeza, “Ni matumaini yetu kwamba msaada huu utakuwa ni nyongeza katika misaada iliyotolewa na watu wenye mapenzi mema na utaenda mbali katika kuwasaidia waathirika kujenga upya maisha yao na kuendelea na maisha kama kawaida.”
Akiishukuru na Cloud media kwa mchango wao Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu alisema kuwa mchango huo unaongezeka katika misaada mingine kutoka kwa watu wenye mapenzi mema ndani ya nchi, ukanda wa Afrika Mashariki na wa kimataifa ambao wametoa kwa ukarimu ikiwa ni mwitiko wa kuunga mkono wito uliotolewa na serikali.
Aidha aliwahakikishia kuwa msaada huo utaenda moja kwa moja katika lengo ulimokusudiwa na kuwataka watu zaidi waendelee kujito kuwasaidia waathrika.