Dar es Salaam, 24 Aprili, 2018.
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania inaungana na kampuni ya simu za mkononi ya TECNO kupanua wigo wa matumizi ya simu janja (smartphone) nchini pamoja na kuwapa wateja huduma bora zaidi za kidigitali, huku wakizundua simu mpya yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X.
TECNO Camon X imejazwa of ya 3GB intaneti bure kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo, ili kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata fursa ya kufurahia huduma za kipekee za kidigitali zinazopatikana kupitia mtandao ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G.
‘Tigo ipo katika kilele cha mageuzi ya kidigitali na ndio mtandao wa kwanza na pekee wa simu za mkononi nchini ambapo wateja wataweza kujipatia simu janja, za kisasa zaidi, zenye uwezo wa 4G za TECNO Camon X kupitia maduka yetu yote ya Tigo. Pia wateja wetu wana fursa ya kununua simu hizi janja za TECNO Camon X kwa njia ya kulipia kwa awamu kutoka kwa duka la simu la Tigo kwa kupiga *147*00#,’ Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alibainisha.
Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania Eric Mkomoya alisema ‘Tunafurahia ushirikiano huu utakaowezesha upatikanaji wa bidhaa murwa na ofa kabambe kwa Watanzania kupitia mtandao mkubwa, wa uhakika na ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G. Hii ni hatua kubwa ya ukuaji wa soko la simu nchini itakayowezesha wateja kupata simu janja ya kisasa zaidi ya TECNO Camon X kwa wakati ule ule ambapo simu hiyo inazinduliwa kote duniani”.
Umoh aliongeza kuwa, ‘Tigo inalenga kuongeza upatikanaji na matumizi ya zimu janja za kisasa nchini, huku tukihakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma bora zaidi za intaneti kupitia mtandao wetu mpana na uhakika zaidi nchini wa Tigo 4G. Ndio maana Tigo inatoa ofa ya 3GB intaneti bure kila mwezi kwa miezi sita kwa wateja wote watakaonunua simu janja ya TECNO Camon X.’
Simu inayotumia kadi mbili ya TECNO Camon X ina kioo cha kikubwa cha inchi 6, uwezo wa 3GB RAM, memori ya 16GB, camera ya mbele yenye uwezo wa 20MegaPixel (MP) na camera ya nyuma yenye uwezo wa 16 MP pamoja na uwezo wa kutambua sura. Simu hiyo pia inakuja na garantii ya miezi 13. Vyote hivi vinaifanya simu hii kuwa bora kwa mtumiaji anayehitaji simu bora. Simu janja ya TECNO Camon X itapatikana kwa bei ya TSH 449,999/- na inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini, katika duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00# na kwenye duka la mtandao la www.jumia.co.tz/tigo-shop.