Akitangaza vifurushi vya Mega Mix kwa waandishi wa habari Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev alivielezea vifurushi hivyo kama "hatua moja mbele ya mabadiliko katika soko inayotoa vifurushi sahihi zaidi: ikiwa ni suluhisho kwa watumiaji wote wa data ndani ya sekta yamawasiliano ya simu nchini Tanzania."
Shavkat aliongeza, "Wateja wetu hivi sasa wana uhuru wa kuchagua kutoka katika simu zao kifurushi chochote wanachokitaka kikiwa na dakika za ziada zitakazo wawezesha kuunganishwa na wapendwa wao wakati tunapoukaribisha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka."
Aliendelea kusema, "Kwa vifurushi vipya wateja wanaweza kuhabarishwa kwa wakati katika mtiririko wa kuunganishwa na wenzi wao na kuwa bega kwa bega na yanayotokea sehemu mbalimbaliduniani. Vifurushi hivi vipya vinaendelea kuonesha jinsi Tigo ilivyojikitakatika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali nainavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa pamoja na ubunifu kwa wateja wetu.
"Wateja wetu vilevile wanaweza kuzipata taarifa za kidunia, kutafuta kupitia Google, kusikiliza muziki, kuangalia video, kupakua na hata kutiririsha sinema. Hii ni kwa sababu tumeunda vifurushi hivi kwa kuzingatia mahitaji ya kipekee ya wateja wetu kwa kufanyauwepo urahisi katika kuchagua kutoka katika kifurushi kimoja kwenda kingine kutegemeana na hali ya kifedha ya wateja."
Aidha Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga alisema, "Kutokana na teknolojia ya 4G LTE kupatikana kwa hivi sasa katika miji 20 vifurushivya Mega Mix kunafungua enzi mpya za kufikia intaneti kusiko naushindani, ambako kutaondoa vikwazo na kuwawezesha watumiaji kuona mengi, kusikia zaidi na hatimaye kupata yaliyo mazuri katika maisha."
Mpinga aliongeza, "Mteja anachotakiwakukifanya ili kupata vifurushi vya Mega Mix ni kupiga *148*00# halafu chagua, Vifurushi vya intaneti."