Akiongea katika mkutano na waandishi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, alimtangaza mshindi huyo wa mwezi kuwa ni Omar Ahmed Bwenda (27) mfanyabiashara na mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Amesema kupitia promosheni hii iliyoandaliwa na Tigo kwa ajili ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuiunga mkono kwa kununua bidhaa na kutumia huduma zake imewawezesha pia wateja 28 kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila siku na wateja wanne kujishindia milioni 1,000,000/- kwa mwezi.
Kupitia promosheni hii itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu washiriki wataendelea kujishindia zawadi za fedha taslimu kila siku, kwa wiki na kwa mwezi. Ili kushiriki kinachotakiwa ni kutuma neno SOKA kwenda namba 15670 au tembelea tovuti ya www.tigosports.co.tz na kujibu maswali kuhusiana na michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri.
“Natoa wito kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo kuendelea kuchangamkia na kushiriki promosheni hii ya SOKA la AFRIKA ili waweze kujishindia zawadi, na kadri wanatavyoshiriki na kujibu maswali ndivyo watakavyokuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata ushindi na kuongeza kuwa na kuongeza kusema kuwa hadi kufikia mwisho wa promosheni hii, zaidi ya wateja 100 watajishindia zawadi ya pesa taslimu.”
Mashindano ya promosheni ya SOKA LA AFRICA ni sehemu ya jitihada za Kampuni ya Tigo kuwashukuru wateja wake kwa kutumia bidhaa na huduma za Kampuni.
Pia promosheni hii ni sehemu ya ubunifu ambao umelenga kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wateja.
Mwisho
About Tigo:
Tigo Tanzania is Tanzania's leading digital lifestyle telecommunications company. Tigo started its operations in Tanzania in 1995. Through its distinctive and diverse product portfolio in voice, SMS, high-speed internet and mobile financial services, Tigo has pioneered digital innovations such as the first Smartphone in Swahili, Free Facebook in Swahili, TigoPesa App, Tigo Mobile App as well as the first East African cross-border mobile money transfer with currency conversion.
For further information visit: www.tigo.co.tz or contact:
Woinde Shisael – Corporate Communications Manager
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.