Michezo zaidi ya 800 inapatikana kupitia huduma hii ikiwemo michezo maarufu ambayo ni pamoja na Buddy Man, Cut the Robe, Zombie Run na Tokyo Drift.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “ Huduma hii mpya ya michezo inaifanya Tigo kuwa ya kwanza katikamitandao ya simu Tanzania kutoa jukwaa la michezo linaloweza kutumiwa na watu wengi ambapo wateja wa Tigo wanaweza kucheza michezo mbalimbali kulingana na chaguo lao kwa gharama wanayoimudu. Tigo imejikita kuendelea kusimamia maslahi ya wateja wake kwa kutoa bidhaa nyingine nyingi kwa ajili ya manufaa ya kuwa na simu za kisasa.”
“Tigo sasa ndio inaongoza katika upatikanaji wa huduma ya 4G LTE nchini, na kwa sasa huduma hii inapatikana katika miji mikubwa 12. Tunaamini kwamba wateja wetu watafaidika sana kutokana na intaneti yenye kasi zaidi itakayo wawezesha kupakua na kucheza michezo hii,” alisema Gutierrez.
Tigo Games ni huduma ambayo mteja akichajua kulipia mara moja, ataweza kuchagua michezoaipendayo na kuicheza atakavyo wakati wowote. Kuna VIP Club ambayo inampa mteja uamuzi wa kujiunga na kifurushi cha siku, wiki na hata mwezi; pia kinamruhusu mteja kupakua michezo bila kikomo.
Mteja ataweza kucheza michezo kwa mda wowote autakao bila makato yeyote. Malipo ya utumiaji wa data kadri mteja anaendelea kucheza ndio yatakayo hitajika. Uzinduzi wa VIP Games Club utakapofanyika, siku 7 za mwanzo wateja wataweza kufurahia huduma bure kwa kutembelea wovuti huu: http://burudani.tigo.co.tz/games
“Kuanzishwa kwa bidhaa hii kupo kwenye mikakati ya Tigo ya kuwapatia wateja wake bidhaa na huduma zilizo na ubora duniani ambazo zinawawezesha kufurahia kwa ujumla maisha ya kidijitali,” alisema Gutierrez.