KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Tigo Tanzania, leo imezindua huduma ya malipo iliyoboreshwa.
Huduma hiyo ya malipo awali ilitambulishwa mwaka 2014 kwa jina la 'Lipa Hapa kwa Tigo Pesa' ili kuwafanya wateja kununua bidhaa mbalimbali kwa njia ya kidijitali.
Kwa sasa huduma hiyo imepewa jina la 'Lipa kwa Simu' ambapo imekuja ikiwa imeboreshwa zaidi na kwamba mteja atatumia kufanya malipo mbalimbali bila kutumia namba za QR katika kupata huduma.
'Lipa kwa Simu' ni huduma ya kifedha ya kidijitali inayomfanya mfanyabiashara au taasisi kupokea fedha kutoka kwa wateja wanaotumia simu za mkononi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo Cha Fedha Cha Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema: “Soko la ndani lina sifa ya ukuaji mkubwa wa idadi ya watu, hususan vijana na viwango vya juu vya utumiaji wa data na mifumo ya kidijitali.
"Madhumuni yetu ni kutanua na kuboresha njia zote za malipo nchini Tanzania. Tunaamini, huduma mpya ya Lipa kwa Simu, itawapa wateja wote wa Tigo Pesa pamoja na watumiaji wengine wa pesa, uzoefu mkubwa wa malipo kwa kuwawezesha kufanya shughuli zao zote za malipo kwa njia salama na rahisi”.
“Pamoja na kuletwa kwa namba za QR na namba zingine katika Lipa kwa Simu tumejipanga kuleta ubunifu na usanifu kwa shughuli za Tigo Pesa.
"Kwa wafanyabiashara, tunaanzisha uzoefu wa ndani ambapo wataweza kusimamia ushuru wao wa malipo kupitia App ya Tigo Pesa, hii itaruhusu urahisi na udhibiti zaidi wa fedha za biashara," alisema.
Uzinduzi huu pia unaenda sambamba na promosheni ambayo itakua ni kwa ajili ya wateja wote wakipata ongezeko la fedha kila watakapotumia huduma ya 'Lipa Kwa Simu'.
Alisema huduma hiyo itakua inapatikana katika maeneo mbalimbali ikiwemo sokoni, sheli za mafuta, cinema, sehemu za vyakula, hotelini, wanapouza vinywaji, supermarket, maduka ya madawa na wanapouza vifaa vya ujenzi.
Alisema kuwa huduma hiyo itatumiwa na wateja wote wa Tigo Pesa na haina haja ya kujisajili.
Wateja wote wanatakiwa kufanya kifuatacho:
1.Bonyeza *150*01#
2.Chagua ‘5’ Lipa Kwa Simu, alafu
3.Chagua “1” kwa Tigo Pesa au unaweza kulipa kwa kutumia Tigo Pesa App na kufurahia huduma hiyo ambayo ni rahisi.
.......Mwisho....