Tigo yazindua ofa mpya ya ‘Saizi Yako’ inayokidhi mahitaji binafsi ya kila mteja
- Ofa inapatikana kupitia menu za Tigo *147*00# na*148*00#
Dar es Salaam. 31 Mei, 2019. Wateja wa Tigo sasa wana kila sababu ya kufurahi baada ya uzinduzi wa ofa mpya ya ‘Saizi Yako’ inayolenga kuwapatia huduma za intaneti, muda wa maongezi na SMS kutokana na mahitaji mahususi ya kila mteja kwa gharama nafuu.
Ofa hii ya ‘Saizi Yako’ ni ya kipekee sana kwa sababu inawapatia wateja ambazo ni mahususi kwa kila mteja hivyo kuwaridhisha wateja wa sasa na wa baadaye wakiangalia gharama wanayoitumia kulinganisha na huduma wanayoipata. Ofa hii pia inapatikana kupitia menyu iliyorahisishwa ili wateja waweze kuipata na kuinunua kwa urahisi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa ofa hii kutoka makao makuu ya Tigo, Dar es Salaam, Afisa Biashara Mkuu wa Tigo, Tarik Boudiaf, alisema kwamba lengo la kampuni hiyo ni kutoa ofa bora, zenye mahitaji yote ya mteja sehemu moja, kwa gharama nafuu, na zitakazo kidhi mapendekezo na mahitaji ya wateja wao.
“Tumezingatia tabia, mahitaji na mienendo ya wateja wetu kwa miaka mingi sasa. Na kinachotufanya tuwe wabunifu ni kwamba tunatambua kwamba kila mteja wetu ni wa kipekee. Hivyo, tumeamua kubuni ofa hii ya ‘Saizi Yako’ ambayo ina mahitaji yote ya mteja sehemu moja na inayozingatia mahitaji yao mahususi. Sasa tunatoa fursa kwa wateja wetu kuweza kupata ofa za kipekee kwa kuzingatia matumizi yao ya kila siku na kwa gharama nafuu,” alisema Boudiaf.
Boudiaf pia alieleza kwamba, kama mteja anatumia muda wa maongezi zaidi kuliko intaneti na SMS, basi atapata kifurushi bora cha muda wa maongezi. Na mteja akitumia zaidi intanet kuliko muda wa maongezi na SMS, mteja huyo atazawadiwa kifurushi bora cha intanet. Utaratibu huo huo utafuatwa pia kwa ajili ya SMS.
“Tunaamini kwamba ‘Saizi Yako’ itaendana na mahitaji, bajeti na maisha ya wateja wetu. Kuwapatia ofa ambayo wataweza kupata kila wanachohitaji sehemu moja, kwa ajili yao, pia inamaanisha kwamba, sisi kama Tigo, tunatambua na kufanyia kazi mahitaji ya wateja wetu yanayobadilika kila siku. Uelewa wetu wa wateja pia unajenga mahusiano yetu nao na kuwafanya watuthamini zaidi,” aliongeza Boudiaf.
Kufurahia ofa maalumu ya ‘Saizi Yako’, wateja wanaweza wakapiga *147*00# au *148*00# kwa urahisi na kuchagua ‘Saizi Yako’. Ofa hii pia itapatakina katika Tigo Pesa APP hivi karibuni.
Mwisho.
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania ni kampuni ya mawasiliano inayoongoza kuwezesha maisha ya kidijitali nchini. Tigo ilianza kufanya kazi nchini mwaka 1995. Kupitia huduma zake mbali mbali na za kipekee za kupiga na kupokea simu, intanet ya kasi na kutuma na kupokea pesa, Tigo imeongoza katika ubunifu wa kidijitali kwa kuzindua simu janja ya kwanza ya Kiswahili, Facebook ya bure kwa Kiswahili, Tigo Pesa App, Tigo Mobile App, pamoja na mfumo wa kwanza wa kutuma na kupokea pesa katika kanda ya Afrika Mashariki wenye uwezo wa kubadilisha fedha za kigeni moja kwa moja.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na:
Woinde Shisael – Meneja Mawasiliano
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.