Kioo Mpapaso
Hadi sasa, kuna maduka 13 ya Tigo zenye vioo mpapaso amabazo unaweza kutumia kuwasilisha maoni yako. Fuata maelekezo kati vifaa hivyo. Utahitajika kutoa namba yako ya simu ili mtu wa huduma kwa wateja aweze kukupata kwa taarifa zaidi. Maoni yako yatapokelewa na huduma kwa wateja ambao watashughulikia maoni yako ili kuweza kuboresha huduma zetu.
Tutumie SMS (ujumbe mfupi wa maneno)
Pia, unaweza kutoa maoni yako kwa kutumia namba maalum hasa kwa malalamiko kuhusu maduka yetu. Tuma maoni au malalamiko kwenda namba hii 0713 123 706 na mtu wa huduma atakujibu.
Mhudumu Mkuu
Jisikie huru kutoa maoni au malalamiko na mhudumu yoyote. Endapo mhudumu msaidizi hajatoa huduma ya kuridhisha, omba kuonana na mhudumu mkuu. Watakusaidia kwa kadili ya uwezo wao.
Tutumie barua pepe
Unaweza kututumia ujumbe kupitia barua pepe ifuatayo Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. na utajibiwa. Hakikisha unatoa maelezo kamili na sahihi juu ya malalamiko au mapongezi yako. Itahusisha jina la duka na mahali ilipo, jina la mtoa huduma na maelezo yakutosheleza juu ya malalamiko au mapongezi yako.
Tutafurahi kupata maoni zaidi kutoka kwako.