Dar es Salaam. 4 Juni, 2019. Wateja wa Tigo wanayo nafasi ya kujishindia safari ya kwenda Misri kushuhudia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 50 kupitia promosheni mpya inayojulikana kama SOKA LA AFRIKA.
Kupitia promosheni hiyo, wateja 10 wa Tigo wataweza kujishindia tiketi za kwenda kushuhudia mashindano haya makubwa barani Afrika, ambapo timu ya taifa, Taifa Stars nayo itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.
Ili wateja waweze kushiriki katika promosheni hii ya SOKA LA AFRIKA na kujipatia nafasi ya kuwa mamilionea pamoja na kushinda tiketi, watatakiwa kutuma neno SOKA kwenda 15670 au kutembelea tovuti ya www.tigosports.co.tz ili kuweza kujibu maswali yanayoihusu mashindano hayo yanayofanyika nchini Misri.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa SOKA LA AFRIKA, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa kampuni hiyo, David Umoh, alisema SOKA LA AFRIKA ipo mahususi kwa ajili ya kuwazawadia wateja waaminifu wa Tigo ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele kutumia bidhaa na huduma za kampuni hiyo katika kutumia huduma na bidhaa zetu.
“Tunaamini kwa kutumia mashindano haya, tunaweza kupata fursa nzuri kutoa habari, elimu na burudani kwa kutumia jukwaa la mawasiliano na michezo,” alisema Umoh.
Fainali za Mataifa ya Afrika, ni mashindano makubwa kuliko yote barani Afrika ambayo yanawaleta pamoja wachezaji wa Kiafrika wanaoshiriki ligi kubwa na zenye ushindani ndani na nje ya bara hili.
“Tunaamini itakuwa ni jambo zuri kwa wateja wetu kupata nafasi ya kwenda kushuhudia mashindano haya makubwa ikiwa ni pamoja na kushangilia timu yetu ya Taifa Stars itakayotuwakilisha. Tunawatakia kila kheri,” aliongeza Umoh.
Akizungumzia zawadi za fedha zitakazotolewa, Umoh alisema, “Zaidi ya wateja mia moja watashinda fedha kila siku, kila wiki na kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu.
Umoh aliwahimiza wateja wa Tigo kushiriki katika promosheni hiyo na kusema kuwa kadiri mteja anapojibu maswali, ndivyo anavyozidi kujiongezea pointi na nafasi kubwa zaidi ya kushinda tiketi kwenda Misri au mamilioni ya pesa.
Mwisho.
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania ni kampuni ya mawasiliano inayoongoza kuwezesha maisha ya kidijitali nchini. Tigo ilianza kufanya kazi nchini mwaka 1995. Kupitia huduma zake mbali mbali na za kipekee za kupiga na kupokea simu, intanet ya kasi na kutuma na kupokea pesa, Tigo imeongoza katika ubunifu wa kidijitali kwa kuzindua simu janja ya kwanza ya Kiswahili, Facebook ya bure kwa Kiswahili, Tigo Pesa App, Tigo Mobile App, pamoja na mfumo wa kwanza wa kutuma na kupokea pesa katika kanda ya Afrika Mashariki wenye uwezo wa kubadilisha fedha za kigeni moja kwa moja.
Woinde Shisael – Meneja Mawasiliano