Dar es Salaam. Agosti 28, 2020. Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha mtanzania anaishi maishi ya kidigitali,Tigo,leo imeingia katika makubaliano na Kampuni ya usafirishaji ya Vigor Group ambayo inamiliki boti za ZanFast Ferries ili kuwawezesha wateja wake kununua tiketi kwa njia ya Tigo Pesa, hatua itakayoboresha huduma za ukataji tiketi kwa wateja wao.
Kampuni ya ZanFast Ferries ni moja ya watoa huduma za usafiri wa majini kati ya Zanzibar na Dar es Salaam zinazochangia katika urahisishaji wa huduma za usafiri kwa wenyeji na wageni.
Kaimu Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema “Tukiwa kama kampuni inayoongoza katika huduma za kidigitali Tanzania,tunafuraha kwa hatua hii kwani inaongeza thamani katika huduma zetu.Kwa sasa wateja wanaweza kununua tiketi kirahisi zaidi kwa Tigo Pesa mahali popote walipo.Tunawashauri wateja wetu kutumia huduma hii ili kuokoa muda na kulipa kwa urahisi zaidi,” alisema Pesha.
Ili kupata tiketi, mteja wa Tigo atatakiwa kupakua application ya ZanFast Ferries kisha nenda kata tiketi,chagua Tigo Pesa na fanya malipo.Baada ya kukamilisha malipo mteja atapokea ujumbe mfupi (SMS) pamoja na tiketi laini (e-ticket) itakayotumika siku ya safari.
“Tunaamini njia hii ni suluhu ya muda mrefu na itaboresha namna wateja wanavyopata huduma za usafiri hususan wasafiri wa ndani kwani kwa sasa hakuna haja ya kwenda tena katika ofisi bali ukiwa na simu yako tu unaweza kujihakikishai uhakika wa kupata usafiri,” alisema Pesha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Vigor Group, Abdallah Turky alieleza kufarijika na ushirikiano baina yao na Tigo Pesa kwani huduma ya Tigo Pesa ni huduma ya uhakika na rahisi kutumika mahali popote na kwamba itarahisisha upatikanaji wa huduma za usafiri kwa wateja wake.
“Ushirikiano baina yetu na Tigo Pesa umetanua wigo wa njia za malipo sanjari na App yetu ya ZanFast Ferries ambazo zinampa mteja uhuru wa kununua tiketi mahali popote alipo,” alisema Turky.
Aliongeza kuwa kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Tigo katika kuleta huduma na bidhaa za kidigitali ili kurahisisha malipo kwa wateja wake.
Wateja watakaofanya malipo kwa Tigo Pesa watatumia tiketi laini (e-ticket) badala ya tiketi za kawaida na watatakiwa kuwa nayo siku ya safari.
Kuhusu Tigo:
Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo ni kampuni inayoongoza katika utoaji wa huduma kidigitali hapa nchini.Tigo ilianza kutoa huduma zake mwaka 1995 ikiwa na huduma mbalimbali za sauti, jumbe (SMS), intaneti yenye spidi pamoja na huduma za kifedha.
Tigo imekuwa mstari wa mbele kuleta mapinduzi ya kidigitali ikiwamo kuanzisha huduma ya Simu janja (Smartphone) ya Kiswahili, Facebook ya bure, App ya Tigo Pesa na zaidi kuwa kampuni ya Kwanza kutoa huduma ya kutuma na kupokea pesa katika nchi za Afrika Mashariki.
Kwa Taarifa zaidi tembelea www.tigo.co.tz au Wasiliana na
Woinde Shisael-Meneja Mawasiliano
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Kuhusu Vigor Group:
Ikiwa na Makao yake makuu visiwani Zanzibar tangu mwaka 1980 ikijulikana kama Turkys Group of Companies, imeendelea kukuza huduma zake Tanzania bara na visiwani pamoja na Visiwa vya Comoro.Hivi karibuni, Kampuni hiyo imeweza kutanua wigo wa huduma katika sekat mbalimbali ikiwamo usafiri wa Anga,Utalii, Afya, Huduma za Fedha, usafiri wa majini, Mawasiliano pamoja na uzalishaji wa umeme ikilega kukidhi mahitaji ya watu wa rika zote nchini.