Hifadhi Biashara | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..


 Hifadhi Biashara

Hifadhi Biashara:

Hifadhi Biashara ni bima ndogo iliyoundwa ili kulinda maisha ya wafanyabiashara wadogo nchini Tanzania kutokana na hatari/majanga yanayoweza kutokea katika shughuli zao za kila siku.

Kumekuwa na majanga mengi ya masoko kuungua moto, mafuriko na mengine mengi hivyo kusababisha hasara kwa wafanya Biashara wengi sana katika miji mbalimbali nchini Tanzania.

Mara nyingi Bima huitaji kujaza fomu ili kuweza kufanya malipo mbalimbali ya Bima husika ambayo mara nyingi kiasi cha bima huwa gharama ukilinganisha na Bima ya Hifadhi Biashara. Mteja atatakiwa kuwa na namba yake ya Tigo Pesa tuu na kiasi cha elfu sabe tuu (7,000) kufurahia bima hii kwa kulinda bima yako dhidi ya Uharibifu wa mali, Wizi, Kushindwa kulipa kodi, Uporaji wa fedha na rambirambi.

Bima hii ya Hifadhi Biashara imeundwa kwa ajili ya wafanya Biashara, wanaomiliki biashara ndogo ndogo na za kati kama vile wakala wa Tigo Pesa, vinyozi, wafanyabiashara wa soko, saluni, maduka ya mboga, bucha, mafundi cherehani, na wafanyabiashara wengine wadogo au wauzaji reja reja.

Fidia na Viwango Vyake :

 1. Uharibifu wa mali hadi million Tano (5,000,000)
 2. Uporaji wa fedha hadi laki mbili na nusu (250,000)
 3. Wizi hadi million moja (1,000,000)
 4. Rambirambi hadi million moja (1,000,000)
 5. Kushindwa kulipa kodi hadi million moja (1,000,000)

Huduma hii inagharimu kiasi gani?

Hifadhi Biashara hugarimu hadi TZS 84,000 kwa mwaka ambapo mteja anaweza kuchagua kulipa kwa muda tofauti kama;

 1. TZS 7,000 kwa mwezi
 2. TZS 21,000 kwa miezi mitatu
 3. TZS 42,000 kwa miezi sita
 4. TZS 84,000 kwa mwaka mmoja

Muongozo wa Utumiaji Kwa USSD.

1. Jinsi ya Kununua Bima ya Hifadhi Biashara:

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua 7: Huduma za Kifedha
 3. Chagua 3: Bima
 4. Chagua 3: Hifadhi Biashara
 5. Chagua 1: Nunua bima
 6. Soma na Kagua maelezo ya Bima, Kisha chagua 1 kuendelea
 7. Andika jina la Biashara/ Mmiliki wa Bima
 8. Andika namba ya simu ya Mrithi Wako
 9. Chagua aina ya malipo
 10. Andika namba ya siri ya Tigo Pesa kukamilisha muamala

2. Jinsi ya Kufungua madai:

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua 7: Huduma za Kifedha
 3. Chagua 3: Bima
 4. Chagua 3: Hifadhi Biashara
 5. Select 2: Madai
 6. Chagua madai kama Mmiliki au kama Mrithi
 7. Fuata maelekezo husika kuendelea

3. Jinsi ya Kuangalia Uhai wa Bima:

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua 7: Huduma za Kifedha
 3. Chagua 3: Bima
 4. Chagua 3: Hifadhi Biashara
 5. Chagua 3: Kuangalia uhai wa Bima
 6. Fuata maelekezo husika.

4. Jinsi ya Kununua Upya:

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua 7: Huduma za Kifedha
 3. Chagua 3: Bima
 4. Chagua 3: Hifadhi Biashara
 5. Chagua 3: Kununua Upya
 6. Fuata maelekezo husika.


Maswali na Majibu:

  Hifadhi Biashara ni nini?

Hifadhi Biashara ni bidhaa ya bima ambayo imeundwa kulinda wafanyabiashara wadogo na familia zao nchini Tanzania..

  Nani anaweza kununua Bima hii ya Hifadhi Biashara?

Wafanyabiashara wadogo na wakati   wanaweza kuchagua kununua Bima hii ya Hifadhi Biashara kwa Tigo Pesa.

  Je ni kwa namna gani mfanyabiashara anaweza kununua Bima ya Hifadhi Biashara kwa Tigo Pesa?

Mfanyabiashara anaweza kununua kupitia menu ya Tigo Pesa (*150*01# )

 • Chagua 7: Huduma za Kifedha
 • Chagua 3: Bima
 • Chagua 3: Hifadhi Biashara
 • Chagua 1: Nunua Bima
 • Soma na Kagua maelezo ya Bima, Kisha chagua 1 kuendelea
 • Andika jina la Biashara/ Mmiliki wa Bima
 • Andika namba ya simu ya Mrithi Wako
 • Chagua aina ya malipo
 • Andika namba ya siri ya Tigo Pesa kukamilisha muamala.

Kiasi cha malipo ulichochagua kitakatwa kutoka kwa akaunti yako ya Tigo Pesa na  malipo yakishakamilika mteja atatumiwa taarifa zako za bima na viwango vya bima yako. 

  Je, unahitaji nyaraka zozote ili kujiunga na bima hii ya Hifadhi Biashara?

Hapana,  Hauitaji nyaraka zozote kujiunga na Bima ya Hifadhi Biashara. Unachotakiwa ni namba yako ya simu iliyosajiliwa na huduma ya  Tigo Pesa.

  Hifadhi Biashara inafidia nini?
 • Uharibifu wa Mali: Kwa madai dhidi ya moto, mlipuko, mafuriko, tetemeko la ardhi, matendo ya Mungu, ghasia na mgomo nk.
 • Wizi: Ikiwa bidhaa zako zimeibwa katika eneo lako la kazi..
 • Kodi: Kwa gharama ya kodi hadi siku 10 kufuatia madai ya uharibifu wa mali
 • Upotevu wa Pesa: Kwa pesa zilizoibiwa katika eneo lako la kazi au zilizoporwa
 • Gharama ya mazishi: Katika tukio la kifo tutafidia gharama za mazishi.
  Fidia zina kiwango gani?
 • Uharibifu wa mali: Tunafidia hadi TZS 5,000,000
 • Wizi: Tunafidia hadi TZS 1,000,000
 • Kodi: Tunafidia hadi TZS 1,000,000
 • Upotevu wa pesa: Tunafidia hadi TZS 250,000
 • Gharama za mazishi: Tunafidia hadi TZS 1,000,000
  Hifadhi Biashara inagharimu kiasi gani na unalipaje?

Unaweza kuchagua aina ya malipo ya kwanza kama inavyoonyeshwa hapa chini kwa kununua moja kwa moja kupitia Tigo Pesa USSD yako

 • Unaweza kulipia TZS 7,000 kwa mwezi
 • Unaweza kulipia TZS 21,000 kwa miezi mitatu
 • Unaweza kulipia TZS 42,000 kwa miezi sita
 • Unaweza kulipia TZS 84,000 kwa mwaka.
  Je, ni kwa wakati gani ambapo nitaondolewa kwenye Bima ya Hifadhi Biashara?

Utaondolewa kwenye bima ya Hifadhi Biashara kama hujafanya upya malipo yako baada ya muda wa ziada wa siku 15, baada ya Bima yako kuisha muda wake.

  Je, ni nini kitatokea ikiwa mtu atanunua bima ya Hifadhi Biashara baada ya muda wa ziada kuisha?

Yafuatayo yatatokea;

 • Bima yako itafutwa kabisa na
 • Utahitajika kujisajili upya kama mteja mpya na kufuata utaratibu wa kujiunga
  Je nini kitatokea, iwapo mfanyabiashara atanunua Bima baada ya muda wake wa ziada kuisha ?

Bima yako  ya zamani itapotezwa na mteja lazima ajiasajili ili anunue bima mpya ya hifadhi biashara.

  Je naweza kujitoa kwenye bima ya Hifadhi Biashara ? Na kwa muda gani ?

Ndio, Unaweza kujitoa kwenye bima ya Hifadhi Biashara muda wowote kwa kuwasilana na wakala kwa wateja  0677066696/7. Ingawa , kwa wateja   wenye bima, itawabidi wasubiri siku 30 hadi bima itakapoisha kwasababu kiasi kilicholipwa hakiwezi kurudishwi. 

  Je nawezaje kufungua madai ?

Unafanya maombi kupitia menu  ya Tigo Pesa (*150*01#) na kisha fuata maelekezo yafuatayo

 • Chagua 7: Huduma za Kifedha
 • Chagua 3: Bima
 • Chagua 3: Hifadhi Biashara
 • Select 2: Madai
 • Chagua madai (1) kama Mmiliki au (2) kama Mrithi kisha fuata maelekezo husika kuendelea.
  Je mteja atasubiri muda gani hadi madai yake yakamilike ?

Madai yote halali yatakamilishwa ndani  ya masaa 72/ siku 3 baada ya uhakiki kufanyika. Kama taarifa zaidi zitahitajika timu ya Hifadhi Biashara itawasiliana na mfanyabiashara ndani ya masaa 72.

  Ni kwa jinsi gani mteja atapokea malipo baada ya kufungua madai?

Madai na malipo yote yatafanyika moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa.

  Ni nani atapokea Rambirambi au Gharama za mwisho endapo mfanyabiashara atafariki?

Mrithi ambae mfanyabiashara alimsajili kwenye Bima ya Hifadhi Biashara ndie atakae pokea malipo ya rambirambi endapo mfanya atapoteza maisha.

  Mfanyabiashara atatakiwa kufanya nini akipatwa na janga?

Inashauriwa, mfanyabiashara akipata janga anatakiwa atoe taarifa Ndani ya masaa 24  kwa Hifadhi Biashara ili kuruhusu kukusanya taarifa Zaidi, Piga *150*01# >> Huduma za Kifedha (7)>>Bima (3) >>Madai(2) na kisha fuata maelekezo.

  Je! Ni wapi nitapata msaada kuhusiana na madai na malalamiko ya Hifadhi Biashara ?

Kwa maswala zaidi kuhusu madai na malalamiko ya Hifadhi Biashara, tafadhali piga Hifadhi Biashara namba 0677066697, barua pepe: Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona., tovuti www.hifadhibiashara.co.tz

  Je ni wapi nitapata msaada kuhusiana na huduma za Tigo?

Tafadhali, Piga 100 kuwasiliana na Huduma Kwa Wateja kwa masuala  ya Tigo kwa msaada zaidi. 

Maana ya maneno na msamiati uliotumika kwenye Hati yako ya Bima

Mahali popo ambapo maneno na msamiati ufuatao umetumika kwenye Hati yako ya Bima, yatakuwa na maana kama ifuatavyo:

 

“kipindi cha mwaka”

Maana yake ni kipindi cha miezi 12 mfululizo kama inavyooneshwa katika mpango wako. Kipindi cha kwanza cha mwaka huanza tarehe ya kuanza kwa bima yako hadi tarehe ya marekebisho iliyooneshwa kwenye mpango wako.

“unyang’anyi wa kutumia

silaha”

inamaanisha uchukuliwaji haramu wa pesa kutoka katika umiliki wako unaofanywa kwa kutumia nguvu au vitisho vya silaha za moto.

“wizi wa kuvunja”

inamaanisha uporaji wa mali yako unaofanywa na mtu anayevunja na kuingia kwenye jengo lililo na biashara yako, akiacha kila dalili za uvunjaji huo.

“biashara”

inamaanisha uhalisia au maelezo ya biashara yako kama yanavyoonekana kwenye mpango wako.

“madai”

inamaanisha ombi lolote linaloletwa kwetu ili kukulipa kutokana na hasara au uharibifu uliotokea.

“yaliyomo”

inamaanisha chochote kilichomo kwenye biashara yako katika eneo lenye vihatarishi. Yaliyomo ni pamoja na vifaa vya ofisi, hisa, vifaa vya biashara, zana, mashine na vifaa vya kielektroni.

 

 

“vifaa vya kielektroni”

inamaanisha vifaa vya kielektroni au mashine mfano kompyuta na na kompyuta mpakato.

“moto”

inamaanisha uharibifu unaosababishwa na moto.

 “tarehe ya kuanza”

inamaanisha tarehe ambayo bima yako inaanza.

“mashine”

inamaanisha mfumo au kitendeakazi pamoja na chanzo chake cha nishati na vifaa saidizi.

“eneo lenye vihatarishi”

inamaanisha eneo la nyumba ambapo biashara yako ipo na / au inapofanyika.

“Mpango”

inamaanisha hati iliyo na maelezo maalumu ya bima iliyokatwa.

“bidhaa”

inamaanisha bidhaa unazoziuza kwa wateja wako

“wewe/lako”

 

“sisi/yetu”

“gharama za mazishi”

 

inamaanisha majina yaliyooneshwa kwenye mpango yaani jina lako au jina la biashara yako.

inamaanisha Sanlam Tanzania General Insurance Limited

inamaanisha gharama za mazishi kutokana na kifo cha ajali na cha kawaida cha mtu mwenye Bima.

 

 

 

Hati yako ya bima

Hati yako ya bima ina vigezo na masharti yote ambayo ni sehemu ya mkataba wako wa bima na sisi. Tunaridhia kulipa hasara zako ilimradi tu ukidhi masharti yote ya hati yako ya bima na hasara au uharibifu uliosababishwa na mojawapo ya matukio yaliyokatiwa bima.

Hati yako ya bima inatokana na ukubali wako wa ofa yetu kupitia Huduma zetu za Mawasiliano ya Ujumbe Mfupi Kati ya Simu na Progamu tumizi (USSD), Mpango wako, vigezo na masharti yetu, mawasiliano yetu kwako na mabadiliko yoyote tuliyokubaliana kwa maandishi.

 

Kulipia kinga ya bima yako

Unatakiwa utulipe kiasi cha pesa kinachojulikana kama ada kwa kila mwezi ambayo itapokelewa kwa idhini yako kutoka kwenye Tigo Mobile Wallet yako. Ikiwa hutalipa malipo kabla ya tarehe ya malipo, tutakupa kipindi cha matazamio cha siku 15 na ikiwa tutakuwa hatujapokea malipo hayo ifikapo mwisho wa siku ya 15, tutaifuta hati yako ya bima.

Madai

Ikiwa bidhaa za biashara yako zimeharibiwa au kuibiwa, unaweza kuleta madai. Iwapo jambo lolote litatokea katika zile bidhaa za biashara yako, ni shurti uwasiliane nasi ili kutufahamisha. Ni shurti uisome hati yako ya bima kwa uangalifu sana ili uelewe ni lini tutaridhia madai.

 

Kukatia Bima ya Bidhaa, Pango, Fedha, Wizi

Mali iliyokatiwa bima

Mali iliyowekewa bima ni bidhaa katika biashara yako au ile unayohusika nayo katika eneo hatarishi kama inavyoonekana katika mpango wako. Tutakulipa fidia ya madai yoyote yanayosababishwa na tukio kama hilo hadi jumla ya kiasi cha bima kilichooneshwa kwenye mpango wako.

 

Matukio yaliyokatiwa bima

Tutakulipa fidia ikiwa bidhaa zilizoko kwenye bima yako zimepotea au kuharibiwa na majanga ya moto; umeme au radi; mlipuko; dhoruba, upepo, maji, mvua ya mawe au theluji; tetemeko la ardhi; athari kwenye magari, ndege au kuangukiwa na vipuli vyake hadi kiasi chote cha bima iliyooneshwa kwenye mpango wako. Aidha, tutakulipa fidia dhidi ya hasara au uharibifu wa mali iliyokatiwa bima kutokana na moto na/au mlipuko ambao umetokea wakati wa kusafirishwa kwenda au kutoka kwenye eneo hatarishi.

Tutakulipa fidia ya kodi ya pango inayotokana na hatari zozote zilizoainishwa katika "Matukio yaliyokatiwa Bima" kwa kipindi chote kama inavyooneshwa kwenye mpango wako.

Tutakulipa fidia kutokana na hasara au uharibifu unaosababishwa na wizi wa kuvunja kutoka kwenye majengo yako hadi kiasi cha bima iliyooneshwa kwenye mpango wako.

Tutakulipa fidia kwa hasara au uharibifu wa pesa kutoka kwenye majengo yako uliosababishwa na wizi wa kutumia silaha na wakati wa kusafirishwa kwenda au kutoka benki hadi kiasi chote cha bima iliyooneshwa katika mpango wako.

 

Visivyokatiwa bima

Hatutakulipa fidia dhidi ya hasara au uharibifu unaosababishwa na mchakato wowote ambao hutumia au kuhusika na maji au kuchakaa au kukwanguka taratibu; ukungu, kutu au kulika.

 

Bima ya Gharama za Mazishi 

Matukio yaliyokatiwa Bima

Tutakulipia gharama za mazishi zinazosababishwa na kifo cha ajali au cha kawaida hadi kiasi cha bima iliyoonyeshwa kwenye mpango wako. Kifo cha ajali inamaanisha kifo kinachotokana na jeraha la mwili ambalo linasababishwa moja kwa moja na vurugu na janga linaloonekana.

 

Yasiyokatiwa Bima  

Hatutalipa fidia pale ambapo kifo kimesababishwa na vitendo vyako mwenyewe moja kwa moja au siyo moja kwa moja.

 

Vigezo na Masharti ya Hati yako ya Bima

Tunatoa kinga chini ya hati yako ya bima kulingana na vigezo na masharti yafuatayo:

 

Shurti uwe mwangalifu

Ni shurti uwe mwangalifu kadiri iwezekanavyo ili kuzuia au kupunguza hasara, uharibifu, kifo, kuumia au deni na usitende kwa uzembe.

 

Ubatilishaji

Unaweza kubatilisha hati yako ya bima wakati wowote. Tunaweza kubatilisha hati ya bima hii kwa kukupatia taarifa ya maandishi ndani ya siku 30 kupitia anwani yako ya posta kama inavyooneshwa kwenye mpango wako au kwa njia nyingine yoyote ya mawasiliano.

 

Madai

Endapo tutabadilisha au kukarabati mali yako, tutajitahidi kukupatia kilekile ulichokuwa nacho hapo kabla, japo inaweza isiwe hivyo wakati wote. Tunaweza kumtumia mgavi au mrekebishaji yeyote tutakayemchagua sisi ikiwa tutakarabati au kubadilisha mali yako. Kabla ya kumaliza au kukamilisha malipo ya madai yoyote, tunaweza kukutaka usaini makubaliano ya hasara.

 

Namna ya kudai

Ni shurti utuambie haraka iwezekanavyo kuhusiana na jambo lolote lililotokea ambalo linaweza kusababisha madai na kutuambia kuhusiana na bima nyingine yoyote ambayo unaweza kuwa nayo.

Ni shurti utupatie maelezo kamili ya kile kilichotokea ndani ya siku 30 tangu kitokee. Ni shurti pia utupatie hati zote ambazo tunaweza kuzihitaji. Ni shurti utuarifu mara moja kwa maandishi ikiwa unamjua mtu yeyote anayekudai au ambaye anataka kufungulia mashtaka.

Ni shurti uripoti kituo cha polisi ndani ya saa 48 kuhusiana na wizi wowote wa kutumia nguvu au kitendo cha jinai. Utalazimika kutia saini hati ya kiapo katika kituo cha polisi na kutoa maelezo kamili kuhusiana na uharibifu, hasara au wizi. Ni shurti pia polisi wakupatie namba ya kesi yako.

Usimwahidi kitu chochote mtu yeyote baada ya tukio kutokea. Ni shurti uwasiliane nasi haraka iwezekanavyo ili tukusaidie kuhusu madai yako.

Ni shurti utuambie haraka iwezekanavyo kuhusiana na jambo lolote lililotokea ambalo linaweza kusababisha madai na kutuambia kuhusiana na bima nyingine yoyote uliyo nayo.

Ni shurti utupatie maelezo kamili ya kile kilichotokea ndani ya siku 30 tangu kitokee. Ni shurti pia utupatie hati zote ambazo tunaweza kuzihitaji.

Ni shurti utuarifu mara moja kwa maandishi ikiwa unamjua mtu yeyote anayekudai au ambaye anataka kufungulia mashtaka.

Ni shurti uripoti kituo cha polisi ndani ya saa 48 kuhusiana na wizi wowote wa kutumia nguvu au kitendo cha jinai. Utalazimika kutia saini hati ya kiapo katika kituo cha polisi na kutoa maelezo kamili kuhusiana na uharibifu, hasara au wizi. Ni shurti pia polisi wakupatie namba ya kesi yako.

Usimwahidi kitu chochote mtu yeyote baada ya tukio kutokea. Ni shurti uwasiliane nasi haraka iwezekanavyo ili tukusaidie kuhusu madai yako.

 

Haki zetu baada ya jambo fulani kutokea na hitaji lako la madai

Ni shurti uturuhusu kutembelea majengo yako ili kutusaidia kushughulikia madai yako. Tunaweza kuhitaji kuchukua mali iliyoharibiwa ili kuifanyia ukarabati au kuipeleka kwa mtu ili kuamua kama inatengenezeka. Itaendelea kuwa mali yako hadi pale tutakapokulipa. Ni shurti uendelee kuilinda mali yako hadi pale tutakapoiondoa.

Ni shurti utupatie taarifa zote na msaada tunaouhitaji ili tuweze kushughulikia matengenezo, utetezi au ulipaji wa madai na kuyafanya kwa jina lako.

Tunaweza kuamua kutoenda mahakamani au kujadiliana na wakili wa mtu fulani. Ikiwa tutaamua jambo hili, tunaweza kukulipa kiasi ambacho tunadhani unastahili. Ikiwa mtu mwingine atakubali kiasi kidogo zaidi, tutakulipa kiasi hicho kama malipo ya mwisho.

 

Ni shurti utueleze ukweli

Lazima kila wakati utupatie taarifa ambayo ni kweli, sahihi na kamilifu kulingana na uelewa wako. Hakikisha kuwa hakuna kitu chochote kinachokosekana. Ikiwa hutatoa taarifa ya kweli, sahihi na kamilifu, tunaweza kubatilisha hati yako ya bima na kukataa kukulipa madai. Hupaswi kufanya udanganyifu au kuleta madai ya ulaghai.

Kama utafanya udanganyifu au kuwasilisha madai ambayo ni ya udanganyifu kwa njia yoyote ile, tutakufungulia mashtaka polisi, kubatilisha hati yako ya bima na kutolipa madai hayo. Hatutakurudishia malipo yoyote ya ada ambazo ulishalipia.

 

Ukomo wa Muda

Ikiwa tutakataa madai yako kwa maandishi, au ikiwa hukubaliani na kiasi cha madai ambayo yametolewa kwa maandishi, unaweza kutuandikia barua ndani ya siku 15 tangu tarehe ya mwisho ulipowasiliana nasi.

Ikiwa bado tutakataa madai yako au kubishania kiwango cha madai yako licha ya uwakilishaji wako wa maandishi, unaweza kufungua shauri la kisheria dhidi yetu ndani ya miezi 6 tangu tarehe tulipokuandikia kukataa uwasilishaji wako.

Hatulazimiki kulipa madai baada ya miezi 12 tangu tarehe ya tukio ambalo limesababisha madai hayo, isipokuwa kama madai hayo yalikuwa yanasubiri hatua ya mahakama au usuluhishi; au kwa kiwango ambacho ni stahiki yako kisheria.

 

Hakuna ada zitakazorejeshwa ikiwa kiasi chote cha bima kitakuwa kimelipwa kwa madai yoyote

Ikiwa tumekulipa madai kwa kiasi chote kinachopaswa kulipwa kwa ajili ya tukio au kifaa, hatutarudisha malipo yoyote ya ada kwa muda uliobaki wa kipindi cha bima yako kwa tukio hilo au kifaa hicho.

 

Kurejeshwa kwa bima iliyokatwa

Kiasi cha bima iliyokatwa kama kinavyoonekana katika Mpango wako hakitapunguzwa na kiasi cha madai yoyote isipokuwa kama imeelezewa vingine.

 

Bima nyingine

Ikiwa madai yanalipwa chini ya hati hii ya bima na chini ya hati ya bima nyingine yoyote, tutalipa tu sehemu ya madai yanayotuhusu.

 

Taarifa muhimu unazopaswa kutueleza

Ni shurti wewe utuambie mara moja endapo kuna mabadiliko yoyote kwa mfano ikiwa umehamisha biashara yako kwenda kwenye eneo jipya au ikiwa umeanzisha biashara mpya. Ikiwa hutatuambia kuhusu mabadiliko yoyote, tunaweza kubatilisha hati ya bima hiyo au kuzuia malipo ya madai yoyote ambayo yametokea baada ya mabadiliko.

Neno "wewe" linajumuisha mtu yeyote anayetenda kwa niaba yako.

 

Mamlaka na Fedha

Bima hii iko chini ya mamlaka ya mahakama za Jamhuri ya Tanzania. Fidia yote itafanywa kwa fedha ya Shilingi ya Tanzania.

 

Mtu anayetenda kwa niaba yako

Utapoteza haki yako ya kupokea fidia ikiwa mtu anayetenda kwa niaba yako hafuati kanuni na masharti ya hati hii ya bima.

Yasiyojumuishwa kwenye hati yako ya bima

Hatutashughulikia hasara, uharibifu au jukumu lolote la kisheria ambalo linasababishwa na au ni matokeo au linahusiana na yoyote kati ya haya yafuatayo:

 

Ghasia, Vita, vitendo vya kisiasa, machafuko ya kijamii, ugaidi au vitendo vyovyote vya aina hii

Ghasia za wananchi, vurugu za wafanyakazi, vurumai, mgomo, kufungiwa nje au machafuko ya kijamii au mapigano au shughuli yoyote ambayo imetambuliwa au kuelezwa kuleta yoyote kati ya mambo yaliyotajwa hapo juu. Vita, uvamizi, uvamizi wa adui wa kigeni, uadui au shughuli kama vita (iwe vita imetangazwa au la), au vita vya wenyewe kwa wenyewe. Uasi, uasi wa jeshi au matumizi ya nguvu, sheria za kijeshi au hali ya kuzingirwa, au tukio lingine lolote au sababu ambayo huamua kutangazwa au kutunzwa kwa sheria za kijeshi au hali ya kuzingirwa, uasi au mapinduzi. Kitendo chochote au jaribio (iwe ni kwa niaba ya shirika, taasisi, mtu au kikundi cha watu) iliyohesabiwa au kuelekezwa kupindua au kushawishi nchi au serikali yoyote, serikali ya jimbo, mtaa au mamlaka za kikabila kwa nguvu au kwa njia ya woga, ugaidi au vurugu.

Kitendo chochote au jaribio lililoandaliwa au kuelekezwa kusababisha hasara au uharibifu wa kuendeleza kusudi, lengo au sababu yoyote ya kisiasa, au kuleta mabadiliko yoyote ya kijamii au kiuchumi, au kupinga hali yoyote au serikali, au mamlaka yoyote ya mkoa, ya jimbo au ya kabila, au kwa kusudi la kuibua hofu kwa umma, au sehemu yoyote ile.

Kitendo cha mamlaka yoyote iliyoanzishwa kisheria katika kudhibiti, kuzuia, kukandamiza au kwa njia yoyote ile kushughulikia tukio lolote ambalo linahusiana na ghasia, vita, vurugu za kisiasa au machafuko ya umma.

Kitendo chochote cha ugaidi. Kitendo cha kigaidi kinamaanisha matumizi au tishio la vurugu kwa sababu za kisiasa, kidini, kibinafsi au kiitikadi. Hii inaweza kujumuisha au isijumuishe tendo ambalo ni hatarishi kwa maisha ya binadamu. Kinaweza kufanywa na mtu yeyote au kikundi cha watu, kutenda kazi peke yao, kwa niaba ya au na shirika au serikali yoyote. Ni pamoja na kitendo chochote kilichofanywa kwa kusudi la kushawishi serikali yoyote au kusababisha hofu kwa umma.

Ikiwa tutasema kwamba madai fulani hayalipwi kwa sababu zozote zilizotajwa hapo juu, ni shurti uthibitishe kuwa madai hayo yamekatiwa bima chini ya hati yako ya bima.

 

Matukio ambayo hutokea kwa sababu ya uharibifu usio na bima kisheria

Tukio lolote ambalo mfuko umeanzishwa chini ya Sheria ya Bima na Fidia ya Uharibifu wa Kivita (Na. 85 ya 1976) ya Jamhuri ya Tanzania.

 

Zana za kinyuklia

Vifaa vya silaha za nyuklia, mionzi au uchafuzi wa unururifu kutoka kwenye nishati yoyote ya nyuklia, au kutokana na taka yoyote ya nyuklia, au kutokana na mwako wa nishati ya nyuklia ambao unajumuisha mchakato wowote wa utupaji wa nyuklia unaojitosheleza wenyewe.

 

Upotevu wa Kompyuta

Kushindwa au kufeli kwa kompyuta yoyote:

kuitambua tarehe yoyote kama tarehe sahihi au tarehe ya kweli ya kalenda, au kwa usahihi au ipasavyo kuitambua, kudanganya, kufafanua, kuchakata, kuhifadhi, kupokea au kuwa na mwitikio wa data au taarifa yoyote, au kutekeleza amri yoyote au maagizo, kuhusu au kuhusiana na tarehe yoyote kama hiyo; au

kupokea, kutunza, kuhifadhi au kuchakata taarifa yoyote au msimbo wowote kama matokeo ya utekelezaji wa maelekezo yoyote ambayo yamewekwa kwenye programu ya kompyuta yoyote, ikiwa ni amri ambayo inasababisha upotevu wa data au kutoweza kupokea, kutunza, kuhifadhi au kuchakata kwa usahihi data kama hii kulingana na au kuhusiana na tarehe yoyote kama hiyo; au

kupokea, kutunza, kuhifadhi au kuchakata taarifa yoyote au msimbo kwa sababu ya makosa ya programu, kuingia kimakosa au kufutwa kwa sheria au kuharibika kwa data na / au programu; au

kupokea, kutunza, kuhifadhi au kuchakata data yoyote kama matokeo ya kitendo cha virusi vya kompyuta yoyote, au msimbo mwingine unaoharibu, au usioruhusiwa au maelekezo ikiwa ni pamoja na kitu kinachoingia na kuharibu programu (Trojan horse), wakati au virusi au msimbo wowote mwingine wenye kuharibu mawasiliano au programu au mwingiliano.

Kompyuta inamaanisha kompyuta yoyote, vifaa vya kuchakata data, maikrochipu, saketi iliyounganishwa au kifaa kama hicho  katika kompyuta au vifaa visivyo vya kompyuta au programu yoyote ya kompyuta, vifaa, mfumo wa uendeshaji au vifaa vyovyote vya kompyuta au vifaa vya kielektroni na habari au data ya kielektroni au vingine vinavyohifadhiwa ndani au juu ya yoyote ya hayo hapo juu, iwe mali yako au la.

 

Utaifishaji

Utaifishaji, utekaji nyara, uporaji, ukamataji, uharibifu wa makusudi, upotezaji, kiambatisho, kumtia ndani, kumtia nguvuni au kuhifadhi au hatua yoyote kama hiyo au michakato yoyote na agizo lolote la mahakama, mila, polisi, vitengo vya kuzuia uhalifu, au mamlaka iliyowekwa kisheria au maofisa.

 

Hasara isiyo ya moja kwa moja

Hasara inayoandamana na au ya moja kwa moja ya namna yoyote ile, isipokuwa pale ambapo fidia yetu inahusiana na mwingiliano wa biashara au bima ya hasara.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo