Home Internet Kutoka Tigo | Tigo Tanzania

 Home Internet Kutoka Tigo

Huduma ya Tigo Home Internet:

Huduma mpya ya Home Internet inayotolewa na mtandao wa Tigo ina kuwezesha kusimamia matumizi ya Router au Modem yako kwa kupitia simu yako ya kiganjani ya Tigo huku ukifuarahia spidi za hali ya juu za 4G+ kutoka Tigo, sifa hii inaifanya huduma hii kua ya kipekee, tofauti na ya kwanza nchini Tanzania.

Huduma hii mpya ya Tigo Home Internet itakuwezesha kufurahia kutumia Router au Modem yako katika mtazamo mwingine kabisa.

Ukiwa na Tigo Home Internet kupitia App ya Tigo Pesa utaweza kufanya yafuatayo:-

 1. Utaweza kutazama salio lako la MBs
 2. Utaweza kutazama salio lako la Dakika
 3. Utaweza kutazama salio lako la kuu (muda wa maongezi)
 4. Utaweza kununua vifurushi vya Home Internet kwa ajili ya Router / Modem yako au kumnunulia Rafiki.
 5. Kupokea ujumbe au taarifa inayohusu kifaa chako (Modem / Router) kupitia namba yako ya simu ya mkononi ya Tigo. 

Kinachofanya huduma hii kua ya kipekee, tofauti na ya kwanza nchini Tanzania ni ule uwezo wa kusimamia matumizi ya Router au Modem yako kwa kupitia simu yako ya kiganjani ya Tigo. Utaweza;-

 1. Kuangalia salio, kununua muda wa maongezi au kununua kifurushi cha internet pasipo kutoa SIMcard yako kwenye Router au Modem
 2. Hakuna haja ya kugeuza matumizi ya Simujanja yako kwa kuitumia kama Router au Modem kwa sababu utapata uwezo wa kusimamia matumizi ya Router au Modem yako kupitia namba yako ya simu ya mkononi ya Tigo
 • Utaweza kuona jinsi unavyotumia MBs zako na kununua vifurushi kiurahisi kabisa kupitia App ya Tigo Pesa. Hili limewezekana kutokana na maboresho tuliyoyafanya. 

Zaidi ya hapo, Tigo Home Internet inakuja na vifurushi nafuu vya wiki na mwezi.


Vifurushi vya Wiki na Mwezi vya Tigo Home Internet ni kama ifuatavyo:- 

Packages: 

Maelezo Wiki Mwezi
Standard Standard Plus Premium Standard Standard Plus Premium
Gharama TZS 15,000 TZS 25,000 TZS 35,000 TZS 50,000 TZS 85,000 TZS 120,000
Kifurushi cha Muda Wote GB12 GB20 GB30 GB30 GB50 GB100
Kifurushi cha Usiku X GB20 GB30 GB30 GB50 GB100
Dakika Mitandao yote X X X 150 300 400

 

Vigezo na Masharti:

 1. MBs za ziada za BURE za internet za kutumika usiku zitatumiwa kuanzia 00:00 hadi 05:59
 2. Kifurushi chako cha Home Internet kinapoisha mteja atahitajika kununua kifurushi kingine ili kuendelea kutumia huduma. MBS za BURE zilizotolewa kama bonasi zitaweza kutumika kati ya 00:00 usiku hadi 05:59 alfajiri tu.
 3. Vifurushi vya Home Internet ni kwa ajili ya wateja waliojiunga na Huduma ya Tigo Home Internet pekee.
 4. Kujiunga na huduma ya Tigo Home Internet tembelea duka la Tigo karibu yako 

Vifaa Vilivyopo:

Modem:

Router:

 


Tigo itawazawadia GB40 kwa kila mteja mpya atakaye nunua SimCARD  mpya pamoja na kifaa cha Tigo Modem  na vile vile GB100 kwa mteja yeyote mpya atakayenunua sim card mpya pamoja na kifaa cha Tigo Router.

Vifurushi vya kuanzia vya Tigo vitakua kama ifuatavyo:-

 1. Tigo SIM + Router + GB100 BURE zitumike ndani ya siku 30 kwa gharama ya Tsh250,000
 2. Tigo SIM + Modem + GB40 BUREE zitumike ndani ya siku 30 kwa gharama ya Tsh125,000

Kifaa cha Tigo Modem kina uwezo wa kuunganisha hadi vifaa 10 vinavyotumia internet wakati Tigo Router zina uwezo wa kuunganisha hadi vifaa 32 kwa wakati mmoja.

Pia Tigo imetenga watoa huduma mahususi kutoa msaada na huduma kwa wateja wetu wanaotumia Tigo Home Internet masaa 24 kila siku.

Maswali kuhusu Tigo Home Internet

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo