Home Internet kutoka Tigo FAQs | Tigo Tanzania


Home Internet kutoka Tigo FAQs

Ni Huduma mpya ya Intaneti kutoka Tigo inayokuwezesha kufurahia matumizi ya router / modem kwa namna ya  kipekee kabisa. Sasa utaweza kudhibiti matumizi yako ya Router na Modem kwa kutumia simu yako ya kiganjani huku ukifurahia mtandao wa 4G+ ukiwa na Tigo Home Internet.

Ukiwa na huduma ya Tigo Home Internet

 1. Hakuna haja ya kutoa Laini yako kutoka kwenye Router/Modem kwa ajili ya kuangalia salio la MBs au kuongeza salio
 2. Hakuna haja ya kugeuza matumizi ya Simujanja yako kwa kuitumia kama Router/Modem kwa sababu utapata uwezo wa kusimamia matumizi ya Router/Modem yako kupitia namba yako ya simu ya mkononi ya Tigo
 3. Utaweza kuona jinsi unavyotumia MBs zako na kununua vifurushi kiurahisi kabisa kupitia App ya Tigo Pesa.

Utahitaji vitu vifuatavyo;

 1. Laini ya Tigo kwenye simu yako
 2. Utahitaji laini nyingine ya Tigo kwa ajili ya kifaa chako cha Tigo Home Internet (Modem / Router)
 3. Utahitaji kifaa cha Tigo Home Internet yaani (Modem/Router)
 4. Uwe na akaunti iliyo hai ya TigoPesa
 5. Pakua App ya Tigo Pesa kutoka App Store au Play Store

Kama una laini ya Tigo unahitaji kujisajili na huduma ya Tigo Pesa kwa kupiga *150*01# na kisha ufuate maelekezo. Pia unaweza kutembelea duka la Tigo karibu yako.

Kama simu yako ni android utahitaji kuingia Google Play Store kupakua App yako ya Tigo Pesa. Kwa sasa App hii inapatikana kwa watumiaji wa simu za Android tu, na App kwa ajili ya simu za Iphone itaanza kupatikana hivi karibuni.

Ukijiunga na Tigo Home Internet utapata;

 1. Uwezo wa kutizama salio papo hapo: MBs na Dakika (ikiwa umejiunga na kifurushi kinachokupa na dakika pia).
 2. Uwezo wa kuangalia salio la muda wa maongezi (salio kuu)
 3. Kikomo cha vifurushi vyako ulivyojiunga
 4. Kununua kifurushi kwa ajili ya Router au Modem yako
 5. Kununua kifurushi kwa ajili ya namba ingine ya Router/Modem (kwa mfano kumnunulia Rafiki)
 6. Kupokea ujumbe au taarifa inayohusu kifaa chako (Modem / Router) kupitia namba yako ya simu ya mkononi ya Tigo.

Kujiunga na huduma ya Tigo Home internet fika duka la Tigo karibu yako

Kujiunga na huduma ya Tigo Home internet fika duka la Tigo karibu yako kwa msaada zaidi.

Ndiyo, unaweza kutumia kifaa chako (Modem/Router) cha mtandao mwingine kujiunga na Tigo Home Internet ikiwa kifaa hicho hakijazuiwa / fungiwa kutumika mtandao mwingine. Kama kimefungiwa au kuzuiwa hutoweza kitumia kujiunga na Tigo Home Internet.

Unaweza kununua vifurushi kupitia;

 1. Kwa App ya Tigo Pesa: Chagua Tigo Mobile Shop
 2. Piga *147*00# kisha chagua Home Internet
 3. tigo.co.tz

Hapana, huduma hii itahitaji mteja kujiunga kila kifurushi chake kinapoisha na haina mpango wa kujirudi rudia (yaani auto renewal).

Ndiyo, kupitia huduma ya Tigo Home Internet utaweza kuwanunulia vifurushi vya Tigo Home Internet marafiki,ndugu na jamaa pia.

Unaweza kupata msaada zaidi kutoka duka lolote la Tigo karibu nawe au kupiga zimu bure kituo chetu cha huduma kwa wateja namba 100

Hapana, tuna vifurushi maalum kwa ajili ya Tigo Home Internet ambavyo vinapatikana kupitia

 1. App ya Tigo Pesa
 2. *147*00#
 3. tigo.co.tz

Hapana, vifurushi vya Tigo Home Internet ni kwa ajili ya matumizi ya vifaa vinavyo tumia huduma ya Tigo Home Internet yaani Router/Modem na si kwa ajili ya simu za mkononi.

 

Vifurushi vya Mwezi vya Home Internet kutoka Tigo vinakuja na Dakika ambazo unaweza kuzitumia kwa kuunganisha simu maalum ya mezani ambayo unaweza unaunganisha na Router yako.

Hapana, Dakika zilizopo kwenye vifurushi vya Home Internet unaweza kuzitumia kwa kuunganisha simu maalum ya mezani ambayo unaweza kuunganisha na Router yako.

Hapana, Dakika zilizopo kwenye vifurushi vya Home Internet unaweza kuzitumia kwa kuunganisha simu maalum ya mezani ambayo unaweza unaunganisha na Router yako.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo