Jaza Tukujaze Tena | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Jaza Tukujaze Tena

Jaza Tukujaze Tena:

Tigo inayofuraha kuzindua promosheni mpya ya Jaza Tukujaze Tena ambayo kila Mteja wa mtandao wa Tigo ni Mshindi. Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku 90.

Jaza Tukujaze Tena ni promosheni inalenga kuwazawadia wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuiamini Kampuni ya Tigo Tanzania kama mtandaobora kwa huduma za mawasiliano nchini. Kupitia promosheni hii Wateja watapata Zawadi za papo kwa hapo kama MBs za intaneti, dakika, au SMS kila wanapojiunga na kifurushi chochote kiwe cha siku, wiki au mwezi.

Pamoja na zawadi za hapo kwa hapo za bonasi za dakika, SMS au MBs za intaneti, watapata nafasi kuingia droo ya bahati ambayo kuna zaidi ya simu janja 1,200 zenye uwezo wa 4G kushindaniwa kwa kipindi chote cha siku 90 cha promosheni. Zawadi za Simu janja zitakazoshindaniwa ni pamoja na Samsung Note 20, ITEL T20 na Kitochi 4G. Simu hizi zitashindaniwa na wateja wetu pamoja na washirika wetu wa timu za mauzo - POS, Wakala, Freelancers, Team Leaders na Mawakala Wakuu wa Tigopesa. 

Wateja wetu wanaweza kununua vifurushi kupitia njia zetu mbalimbali za mauzo ambazo ni *147*00#, Tigopesa Apps na Tovuti yetu na moja kwa moja wataingia kwenye droo na kujishindia simu janja.


Muda wa Promosheni:

Promosheni ya Jaza Tukujaze Tena itaendeshwa kwa siku 90 kuanzia tarehe 23 Oktoba 2020. Promosheni hii itahusisha bahati nasibu ambayo wateja wataingia moja kwa moja kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia simu zenye uwezo wa 4G kila wanunuapo vifurushi.


Jinsi ya Kushiriki:

Wateja wa Tigo wa malipo ya kabla watashiriki kwenye promosheni hii kwa kununua vifurushi kupitia njia yoyote. Vifurushi vyote vya siku, wiki na mwezi vinaruhusiwa kwa promosheni hii na kifurushi chochote kati ya hivyo tajwa kitatoa tiketi ya bure ya kuingia kwenye bahati nasibu na kujishindia simu yenye kasi ya 4G.


Njia za Kujiunga Vifurushi:

 • Kwa USSD menyu *147*00# na *148*00#
 • Kupitia portal au tovuti yetu www.tigo.co.tz
 • Kupitia Tigopesa USSD *150*01# au Tigopesa App ambayo inaweza kupakiliwa kutoka Google Play Store HAPA au APP Store HAPA
 • Kupitia Wakala wetu wa Tigo Rusha.

Uchezeshwaji wa Bahati Nasibu na Mshindi Kuchaguliwa:

Jaza Tukujaze Tena promosheni itakuwa na droo 26 na itawazawadia Zaidi ya washindi 1200 simu zenye uwezo wa 4G na kipindi chote cha promosheni. Droo zitachezeshwa mara mbili kwa wiki, kila Jumatatu na Alhamisi.


Droo na Zawadi:

  • Wateja wote watakaonunua kifurushi (Siku, Wiki au Mwezi) watakuwa na nafasi ya kushiriki kwenye droo.
  • Kila kifurushi kitatoa nafasi 1(moja) ya kuingia kwenye bahati nasibu. Kujiunga kwa wingi kutaongeza nafasi Zaidi za ushindi kwenye droo.
  • Kila kifurushi kitakachonunuliwa bila kujali ni cha Siku, Wiki au Mwezi wala Dakika, SMS, Intaneti au Combo kwa siku husika kitakuwa na nafasi sawa kwenye droo ya bahati.

Kutakuwa na jumla ya washind 14(kumi na nne) kila siku. Ambapo washindi 7 (saba) watakaobahatika watajishindia simu aina ya Kitochi 4G Smart na wengine 7 (Saba) watajishindia simu ya Itel T20 yenye uwezo wa 4G.

Mteja atajishindia Zawadi mara moja tu kwa siku husika LAKINI atakuwa na nafasi ya kushiriki tena droo ya siku inayofuata kama atanunua kifurushi kwa siku hiyo. Hivyo mteja atajishindia Zawadi kwa siku ya kwanza na ya pili lakini hawezi shinda Zaidi ya mara moja katika droo moja.

Bahati Nasibu kwa Zawadi za KUNDI la 1 itafanyika kila Jumatatu na Alhamis. Kila siku ya Jumatatu zitafanyika droo kwa ajili ya washindi wa siku za Alhamis, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ya wiki iliyopita wakati Kila siku ya Alhamisi zitafanyika droo kwa jili ya washindi wa siku za Jumatatu, Jumanne na Jumatano.

Droo zote zitachezeshwa Makao Makuu ya Tigo kwa kusimamiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ambapo washindi wapya14 watachaguliwa kwa kila siku.

Washindi waliochaguliwa watapigiwa simu mpaka mshindi atakapopokea simu na kukubali Zawadi. Ikitokea simu haijapokelewa, hapatikani, hakidhi na kukubali vigezo na masharti na taratibu za promosheni, ushindi wake utahesabika ni batili na namba ninayofuata kwenye droo itapigiwa simu mpaka ataapopatikana mshindi atakaye kubali Zawadi na amekidhi vigezo na masharti.

Muhimu: Droo ya Mwisho itafanyika tarehe 25 Janauri 2021.

Bahati Nasibu awamu ya 2 itakuwa kwa Zawadi za aina ya 2 ambayo ni simu janja ya Samsung Note 20.

 • Ni kwa wateja watakaonunua vifurushi vya wiki na mwezi tu.
 • Kila Kifrushi kitatoa nafasi 1(moja) ya kuingia kwenye bahati nasibu. Kujiunga kwa wingi kutaongeza nafasi Zaidi za kuingia kwenye droo na ushindi.
 • Kutakuwa na jumla ya washindi 3 (Tatu) kwa kila wiki.

Mteja atajishindia Zawadi mara moja tu kwa wiki husika LAKINI atakuwa na nafasi ya ksuhiriki tena droo ya wiki inayofuata kama atanunua kifurushi kwa wiki hiyo. Hivyo mteja atajishindia Zawadi kwa wiki ya kwanza na ya pili lakini hawezi shinda Zaidi ya zawadi moja katika wiki hiyo hiyo.

Muhimu:

Wateja wote watakaonunua vifurushi vya siku, wiki au mwezi wataweza kuingia kwenye droo ya kundi la 1 (kwanza) LAKINI wateja watakaonunua vifurshi vya wiki au mwezi wataingia kwenye droo zote za KUNDI 1 na la 2. Hivyo vifurshi vya wiki au mwezi vilivyonunuliwa kwa siku husika vitaingia kwenye KUNDI la 1 (Zawadi ya siku) kwa siku husika na pia KUNDI la 2 (Zawadi za wiki) kwa wiki husika.

Droo ya 2 kwa KUNDI la 2 zawadi zitatolewa kila Jumatatu na zitahusisha wiki iliyopita. Hivyo wiki itahusisha siku kuanzia Jumanne hadi Jumapili.

Kutakuwa na jumla ya simu 39 zitakazotolewa kama Zawadi za KUNDI la 2. Ambapo ni simu 3 kila wiki kwa wiki 13.

Droo za bahati nasibu zote zitafanyika Makao Makuu ya Tigo chini ya usimamizi wa Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.

Washindi waliochaguliwa watapigiwa simu kwa awamu mpaka mshindi wa kwanza atakapopokea simu na kukubali Zawadi. Ikitokea simu haijapokelewa, mpigiwaji hapatikani au hakidhi na kukubali vigezo na masharti na taratibu za promosheni, ushindi wake utahesabika ni batili nan amba ninayofuata kwenye droo itapigiwa simu mpaka ataapopatikana mshindi atakaye kubali Zawadi na amekidhi vigezo na masharti.

Muhimu: Droo ya mwisho itafanyika tarehe 25 Januari 2021 lakini haitahusisha wiki ya tarehe 11 hadi 18 Januari 2021.


 

Frequently Asked Questions:

  What is Jaza Tukujaze Tena promotions?

This is a New promotion launched by Tigo where every Tigo subscriber is a winner. This promotion was launched on 23rd October 2020 and will run for a period of 90 Days. Through this campaign, Tigo customers who subscribers to any daily, weekly or monthly package will be rewarded with nstant bonus of minutes, SMS or MBs and will automatically get FREE entry into a raffle draw where over 1200 4G capable devices stand to be won.

  What packages are eligible for this promotion?

Any package/bundle (Data, Voice, SMS or Combo) of any validity (Day, Week or Month) will be considered as one free ticket to the raffle draw where a subscriber stands a chance of winning a 4G capable mobile device.

This excludes the purchase of ILD, International, Roaming, Niwezeshe packages and segmented packages

  Who is eligible to participate in the Jaza Tukujaze Tena promotion?
 • All Registered Tigo prepaid individual customers across the country.
 • The promotion is open for Tanzania residents only
 • Participants must be 18 (Eighteen) years of age to be able to participate
 • Tigo staff, their agencies and immediate family members may buy packages BUT will not be eligible for prizes from the raffle draws.
 • B2B and Postpaid contracts are specifically excluded from the Buy and Win promotion.
  Can I do multiple subscriptions for bundles/packages and enter into the draw?

Yes, Multiple subscriptions will yield multiple entry tickets to the raffle draw and thus increasing the chances of winning. Terms and conditions and FUP (Fair Usage Policy) to apply.

  Where can I buy the Tigo bundles/Packages to enter into the raffle draw?

Prepaid customers can buy bundles/packages via all our product channels

 • Our USSD menu *147*00#
 • Our portal or website at www.tigo.co.tz
 • Through Tigopesa USSD *150*01# or Tigopesa APP which can be downloaded from Google Play Store and APP Store
 • Through our Agents selling Tigo Rusha
  What are the 4G mobile phones given out in this promotion?

Samsung Galaxy Note 20 as weekly prize and Kitochi 4G Smart, Itel T20 as daily prizes.

  Can I win the same prize more than once?

No, subscriber will not be eligible to win more than 1 (One) daily or weekly prize for that particular day or week. However you are eligible to participate and win in the next/subsequent daily or weekly draws.

  If I win, can I participate in the next raffle draw?

Yes, previous winners are eligible to participate in the draws of following days

  How would I know that I have a won a prize?

If a customer wins a phone, a representative from Tigo will contact the winner about the prize and all details for picking up the prize.

  How can I opt out from the raffle draw if I don’t want to participate?

Since the promotion requires no subscription there is No opt out, but if a customer wishes not to be part of Buy and Win promotion then he/she needs to contact our call center number 100 or visit any of our Tigo Shops

Jaza Tukujaze Tena Vigezo na Masharti:

 • Promosheni hii ni kwa Wateja wa Tigo wa malipo ya kabla tu/pekee
 • Promosheni hii ni kwa Raia wa Wakazi halali wa Tanzania
 • Wafanyakazi wa Tigo ndugu zao na watu wa karibu hawatakua sehemu ya promosheni hii.Lakini wataweza kununua vifurushi
 • Mshiriki lazima awe na umri wa miaka 18 na kuendelea
 • Ushiriki katika promosheni hii ni Bure,Hakuna gharama za ziada
 • Kila ununuapo kifurushi chochote kiwe cha (Intaneti, SMS au Dakika) au cha Siku wiki au mwezi itachukuliwa kama tiketi moja kuingia kwenye droo ya bahati. Hii haitahusisha vifurushi vya kimataifa na Tigo Niwezeshe
 • Kadri ununuavyo vifurushi mara nyingi ndivyo unavyojiongezea nafasi kubwa ya ushindi kwenye droo ya bahati.
 • Tigo ina haki ya kusitisha huduma hii kama ikigudulika kua kifaa kinachotumika ni Batiri kulingana na Mwongozo wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania.
 • Tigo inahaki ya kurekebisha/Kuboresha vigezo na mashariti vya promosheni hii kwa kutoa taarifa na kuizinishwa na Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania
 • Promosheni hii ni kwa wateja wa malipo ya kabla (prepaid)wateja wa malipo ya baada na makampuni hawataruhusiwa kushiriki.
 • Kila kifurushi kitakua na nafasi sawa za ushindi kwenye droo ya bahati
 • Kutakua na Jumla ya siku za droo 26. Hii ina maanisha kwa siku ya Droo kutafanyika droo za siku Zaidi ya moja. Yaani Mfano Droo zitakazofanyika siku ya Jumatatu zitahusisha droo za bahati kwa siku za jumapili, jumamosi, ijumaa na alhamisi.
 • Kutakua na jumla ya simu janja 1200 ambazo zitatolewa kama Zawadi kwa wateja.kupitia promosheni hii.
 • Kutakua na jumla ya washindi 14 kila siku,washindi 7 watapata simu aina ya Kitochi 4G Smart na wengine 7 watapata Itel T20, zote zikiwa na uwezo wa 4G.
 • Ushindi ni Mara moja tu kwa siku/Mshiriki hawezi shinda Zaidi ya mara moja kwa siku.
 • Wateja ambao tayari wamewahi kushinda zawadi za siku au wanaruhusiwa kushiriki tena kwenye promosheni hii na wana nafasi ya kushinda tena kwa droo zinazofuatia..
 • Mteja atakae nunua kifurushi cha wiki/Mwezi ataingia kwenye droo ya Bahati Nasibu ya siku(katika siku husika) na droo ya wiki,katika wiki husika.
 • Mshiriki hawezi shinda Zaidi ya mara moja kwa wiki husika
 • Wateja ambao tayari wamewahi kushinda zawadi za wiki au wanaruhusiwa kushiriki tena kwenye promosheni hii na wana nafasi ya kushinda tena kwa droo zinazofuatia.. 
 • Jumla ya simu Janja 39 zitatolewa kwenye promosheni hii katika kipengere cha washindi wa wiki.Simu 3 kila wiki kwa siku 90.
 • Katika kipengere hiki (washindi wa wiki) Zawadi ni simu Janja aina Samsung Note 20
 • Kujitoa;Kwakua promosheni hii si ya kujiunga,hakutakua na namna ya mteja kujitoa,ila kama mteja atahitaji kujitoa,atatakiwa kupiga namba 100 huduma kwa wateja. 
 • Pamoja na namba ya Mteja kuchaguliwa kama mshindi, Mteja atahesabika mshindi kamili mara baada ya uhakiki wa taarifa zake kwa kufuata vigezo na Mashariti ya promosheni hii
 • Kwa kushiriki katika promosheni hii,Mteja anaipa Tigo haki ya kutangaza Jina/Jina na picha ya mshindi kwenye magazeti yaliyo chaguliwa katika kipindi chote cha promosheni.
 • Washindi watapigiwa simu na Mwakilishi kutoka Tigo mbele ya Mwakilishi kutoka Bodi ya Taifa ya Bahati Nasibu.Mshindi anatakiwa kupokea sim una kutoa taarifa za kumtambua. Kama Mteja hatapokea simu droo nyingine itafanyika hadi pale mshindi atakapopatikana na taarifa zake kuthibitishwa.
 • Washindi watatakiwa kuonyesha moja kati ya vitambulisho vinavyotambulika na kukubalika Kitaifa. Vitambulisho hivi ni Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha Uraia,Kitambulisho cha makzi Zanzibar au Pasi ya kusafilia wakati wa kukabidhiwa Zawadi.
 • Mshindi ataiidhinishia Tigo kutumia taarifa zake,Anwani ,picha na sauti kwa Matangazo au kwa matumizi mengine,Mteja hatakua na Haki ya kulipwa katika kipindi chote cha kampeni na siku 360 baada ya kampeni kumalizika.
 • Kama Mteja hatopatikana kwenye simu,au kuto kubaliana na vigezo na mashariti,au mshindi kushindwa kuchukua Zawadi yake ndani ya siku 90,Ushindi Utabatilishwa na Mshindi mbadala atapigiwa simu.
 • Washiriki wanahakikishiwa kua hakuna upande wa tatu wenye haki ya kuchapisha,kuonyesha,kusambaza au kudukua picha ya mshiriki.Tigo Hitausika na usambazaji huo,Na ikitokea,Mtu wa tatu atahusika.
 • Ushiriki katika promosheni hii kutamaanisha idhini na kukubaliana na vigezo na masharti , video, sauti au taarifa binafsi za mshindi kwa njia yeyote ile ya mawasiliano kama redio, magazeti, njia za satelite au runinga kwa dhumuni la kuitangaza promosheni hii wakati wote wa promosheni hii na kwa kipindi kisichozidi mwaka 1. Mshiriki hatokua na haki ya kudai au kufungua madai ya ujira / fedha kwa namna yeyote ile. 
 • Washiriki wanatambua kuwa kushiriki katika kampeni hii hakuleti uharibifu wowote wa mali, kwa hiyo, Hakutokua na madai yoyote ambayo yanaweza kutolewa dhidi ya MIC Tanzania Ltd, ama kwa kujisajili kwa huduma zilizoorodheshwa  au kwa kuhamisha haki miliki zozote. 

Kuwa sehemu ya kampeni hii kunamaanisha Mshiriki anafahamu na kukubaliana na sheria zote zilizowekwa katika Vigezo na masharti katika Promosheni ya  Jaza Tukujaze Tena. Kila Mshiriki atachukuliwa amekukubali kila moja ya mahitaji yaliyoelezwa,pamoja na kukubaliana na maamuzi yaliyopitishwa na Tigo juu ya maswala

ambayo yalitarajiwa au hayakutarajiwa katika ushiriki wake. 

Tigo itakuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu migogoro yoyote isipokuwa itakapoagizwa vingine na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania

 • Mawasaliano au taarifa zote kuhusu promosheni hii na mshiriki zitasimamiwa na sharia za Tanzania na mshiriki anakataa sheria zingine zozote ambazo zinazoweza kutumika. 

Vigezo na masharti ya Promosheni ya Jaza Tukujaze Tena vinapatikana kupitia tovuti ya www.tigo.co.tz Pamoja na vituo vya Huduma kwa wateja Tigo 

Promosheni hii itaendeshwa kwa siku 90 kutoka  Oktoba 23 2020 hadi  Januari  21-2021. 

Droo kwa wiki ya mwisho ya promosheni hii itafanyika 25 Januari 2021.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo