Jigiftishe Promo | Tigo Tanzania

 Jigiftishe Promo

Jigiftishe Promo

‘JIGIFTISHE’ ni promosheni mpya ya kutoka Tigo kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu, ambapo Tigo itatoa mamilionea Zaidi ya 450 katika msimu huu wa sikukuu. Mamilionea hawa watapatikana kwa kutumia huduma za tigo za kawaida, bila masharti ya ziada.

Unachotakiwa kufanya ni kuendelea kutumia huduma za Tigo ambazo ni pamoja na; Kuongeza salio, kununua kifurushi, kununua simu katika duka lolote la Tigo, kutumia huduma za Tigopesa, na hapo hapo utapata nafasi ya kuingizwa katika droo itakayokuwezesha kupata nafasi ya kushinda Shilingi Milioni 1 kila siku, Shilingi Milioni 10 kila wiki au hadi Shilingi Milioni 50 katika droo ya mwisho ya promosheni ya Jigiftishe.

Kila huduma utakayotumia itakupa nafasi kuingia katika droo (**Vigezo na Masharti kuzingatiwa). Unaweza kuangalia nafasi zako za kuingizwa katika droo kwa kupiga *149*22#. Huduma au Miamala mingi Zaidi unayofanya ndio itakupa nafasi zaidi za kuingia kwenye droo ya ushindi.

Promosheni hii ni kwa wateja wote wa Tigo.Tuzo za Jigiftishe

PRIZES


TUZO ZA SIKU
TSH MILIONI 1
Washindi 10 kila siku
TUZO YA WIKI
TSH MILIONI 10
Mhindi mmoja kila wiki
TUZO KUU
TSH MILIONI 15
TSH MILIONI 25
TSH MILIONI 50

1. Droo ya Siku

 • Namba za simu zitazofanya miamala au kununua vifurushi vya Tigo ndani ya Siku husika, zitaingizwa katika droo itakayochezeshwa siku inayofuata, ili kupata washindi 10 wa Shilingi Milioni 1 kila mmoja
 • Huduma zitakazokuwezesha kuingia katika droo ni pamoja na;
  • Kuongeza salio (kwa njia yoyote)
  • Kununua kifurushi
  • Kufanya miamala ya TigoPesa
  • Kulipia bili kwa TigoPesa

2. Droo ya Wiki

 • Namba za simu zitakazofanya miamala ndani ya wiki husika (Jumatatu hadi Jumapili) zitaingizwa katika droo itakayochezeshwa ili kupata mshindi 1 wa Shilingi Milioni 10.
 • Unavyozidi kufanya miamala na kutumia huduma za Tigo ndipo unapojiongezea nafasi za kushinda

3. Droo Kubwa

 • Namba za simu zitakazofanya miamala ndani ya kipindi kizima cha promosheni zitaingizwa katika droo ya kushinda Shilingi Milioni 15, Milioni 25 na Milioni 50.
 • Unavyozidi kufanya miamala na kutumia huduma za Tigo ndipo unapojiongezea nafasi za kushinda

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo