Kibubu FAQs | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..


Kibubu FAQs

TigoPesa Kibubu ni huduma inayokuwezesha kuweka akiba binafsi kwa kuunganisha akaunti kuu ya TigoPesa na akaunti ya Tigo Pesa Kibubu.

TigoPesa Kibubu inaunganisha akaunti kuu wa TigoPesa na akaunti yaTigoPesa Kibubu inayomwezesha mteja kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti moja kwenda nyingine.

Piga * 150 * 01 #, Chagua Huduma za Kifedha (7), >> Akiba (8) >> TigoPesa Kibubu (Akiba ya Binafsi) (1), kisha fuate maelekezo.

Mteja anaweza kuweka kiasi kuanzia TZS 1  hadi kiwango chochote kwenye TigoPesa Kibubu ilimradi tu kiasi hicho kipo kwenye akaunti kuu ya TigoPesa.

Mteja anaweza kutoa kiasi chochote cha chaguo na TigoPesa Kibubu hadi kiwango cha juu kabisa kinachopatikana katika akaunti yake ya TigoPesa Kibubu.

Ndio, Mteja anaweza kuangalia salio la akaunti yake ya TigoPesa Kibubu kupitia njia ya USSD kwa kupiga *150*01# kisha chagua 6 (Jihudumie- akaunti na Salio) kisha chagua 3 kuangalia salio kisha chagua namba 2 Salio la Tigo Pesa Kibubu.

Mteja atapata gawio kwenye akaunti kuu ya Tigo Pesa kila mwisho wa mwezi.

Gawio litalipwa kwenye akaunti kuu ya Tigo Pesa katika siku chache za kazi mwanzoni wa mwezi mpya.

Mteja anaweza kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yake TigoPesa Kibubu hadi kiwango cha juu kinachopatikana katika akaunti hiyo muda wowote atakapohitaji kufanya hivyo.

Tafadhali, Piga 100 kuwasiliana na Huduma Kwa Wateja kwa msaada zaidi.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo