Kuhusu Tigo | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

Tigo ilianzishwa mwaka 1994 ikiwa mtandao wa kwanza Tanzania wa simu za mkononi. Ni kampuni ya mawasiliano yenye ubunifu mkubwa nchini na ambayo inatoa huduma zinazolenga kuleta mageuzi ya kidijitali katika maisha ya watanzania. Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha za kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music (Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika

 Intaneti ya Tigo ya 4G na 3G zinatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima. Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya maeneo mapya 500 yenye mtandao wa Tigo na kufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya mtandao na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongeza uwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini. Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 9 waliosajiliwa, Tigo imeajiri zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.

Tigo ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni la Millicom, kampuni ya kimataifa inayoendeleza maisha ya kidijitali katika nchi 12 pamoja na shughuli za kibiashara katika Afrika na Amerika ya Kusini na ina ofisi Ulaya na Marekani. Pamoja na ujuzi wakibunifu iliyonayo, Millicom imeendelea kujenga thamani kubwa kwa wanahisa wake kwa kutumia dhana yao ya "hitaji zaidi" jambo ambalo limeiwezesha kampuni kujikita kileleni katika nafasi ya uongozi ya kuendeleza maisha ya kidijitali katika masoko inakoendesha shughuli zake

 

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo