Kutuma Pesa Kimataifa | Tigo Tanzania

 Kutuma Pesa Kimataifa

WorldRemit | Pata Bonus, kila unapopokea pesa kwenye akaunti ya Tigo Pesa! 

Wateja wa Tigo wataweza kupata bonus ya hadi TSh 10,000 papo hapo mara baada ya kupokea pesa kutoka nje ya nchi kupitia huduma ya WorldRemit kwa miamala yenye thamani ya zaidi ya Tsh 100,000 kila siku. 

Vigezo na Masharti:

 • Promosheni hii ipo wazi kwa ajili ya wateja wote wa Tigo Pesa wanaopokea pesa kupitia huduma ya kifedha ya WorldRemit.
 • Bonus itatolewa mara moja tu kwa siku kwa muamala mmojawapo unaozidi kiasi cha Tsh 100,000.
 • Bonus italipwa papo hapo kwenda kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa  
 • Ili kuweza kupokea Bonus, namba yako ya Tigo Pesa inatakiwa kuwa imesajiliwa kikamilifu.
 • Promosheni hii itadumu hadi Novemba 30, 2019.
 • Kiwango chochote cha fedha kilicho chini ya Tsh100, 000 kitakachopokelewa kutoka WorldRemit kwenda Tigo Pesa hakitaweza kupata bonasi.
 • Kwa maelezo zaidi piga namba 100 huduma kwa wateja.

Kutuma Pesa kwenda kwa wateja wa Tigo Pesa nchini Tanzania Kupitia huduma ya WorldRemit

Kupitia huduma ya WorldRemit, unaweza kutuma pesa kutoka nchi yoyote duniani kwenda kwa wateja wa Tigo Pesa.Kama unahitaji kutuma Pesa kwa mteja wa Tigo Pesa aliyeko nchini Tanzania, fuata hatua zilizoainishwa kwenye link hii hapa chini:

https://www.worldremit.com/en/tanzania/tigo-mobile-wallet 

Kupitia huduma ya WorldRemit, wateja wa Tigo Pesa wanaweza kupokea pesa moja kwa moja kwenda kwenye simu zao kutoka kwa marafiki na ndugu wanaofanya kazi au kuishi nje ya nchi.Huduma hii ni ya haraka, rahisi, salama na nafuu ya kutuma au kukuwezesha kifedha.

Kutuma na Kupokea Pesa  Afrika Mashariki  

Kupitia  Tigo Pesa, unaweza kutuma na kupokea  pesa  kupitia  Airtel-Tigo Rwanda, MTN Rwanda na  MTN Uganda.

Jinsi ya kutuma Pesa kwenda nchi nyingine  

 • Piga *150*01#
 • Fanya chaguo  1 – Kutuma Pesa
 • Fanya chaguo  4 – Kwenda nchi nyingine
 • Alafu Chagua nchi na mtandao wa simu ya mkononi unaotaka kuutumia  kutuma pesa  
 • Ingiza namba uliyopokea  (+256xxxxxxx au +254xxxxxxx or +260xxxxxxxor +255xxxxxxx)
 • Ingiza kiasi unachotaka kutuma kwa pesa ya Tanzania
 • Utapokea ujumbe ukikuonesha kuthibitisha jina la mpokeaji , Kiasi , Taarifa za ubadilishaji wa pesa na gharama zake
 • Kuhakikisha, Ingiza PIN ya Tigo Pesa
 • Utapata ujumbe wa kuthibitisha kukamilika vyema kwa muamala
 • Na Mpokeaji atapokea kiasi kwa uthibitisho wa ujumbe

Viwango na gharama vinavyotumika wakati unatuma pesa kwenda  MTN Uganda na MTN Rwanda

Tigo Pesa

Kiwango cha chini

Kiwango cha juu

Gharamaza IMT (50% zaidi ya P2P)

               100

               999

                                                     23

           1,000

           1,999

                                                     38

           2,000

           2,999

                                                     53

           3,000

           3,999

                                                     75

           4,000

           4,999

                                                     98

           5,000

           6,999

                                                   188

           7,000

           9,999

                                                   195

         10,000

         19,999

                                                   480

         20,000

         29,999

                                                   548

         30,000

         39,999

                                                   555

         40,000

         49,999

                                                   600

         50,000

         99,999

                                               1,080

      100,000

      199,999

                                               1,500

      200,000

      299,999

                                               1,800

      300,000

      399,999

                                               2,250

      400,000

      499,999

                                               2,250

      500,000

      599,999

                                               3,300

      600,000

      799,999

                                               4,950

      800,000

   1,000,000

                                               5,250

   1,000,001

   3,000,000

                                               7,200

Viwango vya  Dunia | Kutuma kwa wateja wa Tigo Pesa  Tanzania

Unaweza kupokea pesa kutoka sehemu yoyote duniani  kupitia viwango vya Dunia . Kama unatarajia kutuma pesa kwa mtu nchini Tanzania , fuata utaratibu uliopo kwenye anwani ifuatayo ya URL:

https://www.worldremit.com/en/tanzania/tigo-mobile-wallet

Kupitia vigezo vya Dunia , Wateja wa Tigo Pesa wanapokea pesa moja kwa moja kwenye simu zao za mkononi kutoka kwa marafiki na familia , wakiwa kazini au safarini nje ya nchi . Ni mojawapo ya huduma rafiki , rahisi, isiyo na bei , salama ,  ya haraka na njia nyepesi ya kusaidia kupeana msaada wa kifedha.

 

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo