Kuwa Mfanyabiashara atumiae Tigo Pesa | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Kuwa Mfanyabiashara atumiae Tigo Pesa

Kuwa mfanyabiashara atumiae Tigo Pesa alafu jiunge na zaidi ya biashara 70,000 zinazopokea malipo kutoka kwa zaidi ya watumiaji milioni 16 wanaotumia Tigo Pesa, Mpesa, Airtel Money au EzyPesa. Pia, ukiwa na Tigo Pesa, unaweza kupokea malipo kutoka kwa watumiaji wa MPesa, Airtel Money, TPesa, Halopesa na EzyPesa. Hii inakuwezesha kufanya miamala na wateja wengi zaidi kuliko mtandao wa simu nyingine.

Ukiwa mfanyabiashara atumiae Tigo Pesa, unaweza kuhamisha pesa yako kutoka akaunti yako ya Tigo Pesa kwenda kwenye akaunti yako ya benki, kulipia billi mbalimbali na pia kutoa pesa kutoka kwa wakala wa Tigo Pesa utakapohitaji.

Kama unataka kuwa mfanyabiashara atumiae Tigo Pesa, piga namba ifuatayo 150 au jaza fomu ya mawasiliano iliyopo hapo chini. Utahitaji yafuatay

1.       Leseni ya kufanya biashara 

2.       Kitambulisho

3.       Mkataba wa biashara

4.       TIN namba na malipo ya VAT

5.       Hati ya Usajili 

Terms and Conditions 

Mfanyabiashara anayetumia Lipa Hapa kwa Tigo Pesa: ni mfanyabiashara yoyote anayepokea/kubali malipo kwa njia ya Tigo Pesa

Mteja: Inamaanisha mtu  aliyesajiliwa kikamilifu anaweza kutumia Huduma yoyote ya Tigo Pesa kupitia njia yoyote. Neno "Mteja" litajumuisha wawakilishi wa kibinafsi wa mteja, waliofaulu kwa jina na wadhifa na vile vile watu wanaohusika na mamlaka ya Wateja kama mawakala, wafanyakazi.

Usajili:

Wakati wa usajili wa huduma hii mfanyabiashara anatakiwa kutoa maelezo yafuatayo ambayo yatakuepo kwenye kandarasi amayo itasainiwa na yeye mwenyewe: -

 •  Namba ya simu;
 •  Majina kamili;
 • Tarehe ya kuzaliwa;
 • jinsia
 • anwani ya makazi.
 • Aina ya biashara

Pia, utahitajika kutoa nakala ya hati zifuatazo;

 

Kwa wafanyabiashara wadogo

 • Nakala ya kitambulisho cha Machinga
 • Nakala ya kitambulisho cha NIDA

Kwa wafanyabiashara wa kati

 • Nakala ya TIN
 • Nakala ya leseni ya biashara
 • Nakala ya kitambulisho cha NIDA

 

 

 

 

Kwa wafanyabiashara wakubwa

 • Nakala ya TIN
 • Nakala ya leseni ya biashara
 • Nakala ya kitambulisho cha NIDA
 • Nakala ya memorandum of association
 • Nakala ya article of association
 • Barua ya utambulisho

Kwa mashirika isiyo ya faida

 • Barua ya utambulisho
 • Nakala ya barua ya idhini
 • Nakala ya kitambulisho cha NIDA

Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo