Intaneti ya 4G Tanzania | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..


 Intaneti ya 4G Tanzania

Lipa Kidogo Kidogo:

Hii ni huduma inayomuwezesha mteja wa malipo ya kabla kudunduliza fedha kidogo kidogo kupitia Tigo pesa kwa muda wa miezi mitatu au sita. Mteja analipia kiasi ambacho ni sawa na bei ya simu halisi kidogo kidogo bila riba.

 

Namna ya kupata huduma:

 1.    Piga *147*00# kisha chagua Huduma nyingine kisha chagua Duka la simu
 2.    Unaweza pia kufika dula lolote la Tigo au Mawakala wa Tigo nchi nzima

 

Vigezo na Masharti:

 1. Huduma hii ni kwa wateja wa Tigo tuu wa malipo ya kable
 2. Mteja atatakiwa kusoma vizuri vigezo na masharti kabla ya kuanza kutumia huduma hii
 3. Mteja atatakiwa kujisajili na huduma kabla ya kuanza kudunduliza
 4. Mteja anatakiwa kuanzia na kiwango cha kudunduliza kisichopungua asilimia 20 ya bei ya simu kwa awamu ya kwanza.
 5. Mteja anaweza kuwekeza kiwango chochote baada ya kiwango cha kwanza hadi atakapomaliza malipo yake
 6. Endapo mteja hataweza kumalizia kiasi cha kudunduliza fedha tasilimu kufikia bei ya simu kwa muda aliochagua, pesa iliyokwisha dundulizwa itarudishwa kwa mteja.
 7. Mteja anaweza kukatisha kudunduliza na akafika duka lolote la Tigo kurudishiwa pesa yake
 8. Mteja akishamaliza kudunduliza, atatakiwa kufika duka la Tigo akiwa na kitambulisho chake (NIDA, Passport au Leseni ya udereva) kuchukua simu yake
 9. Mteja hataweza kumhamishia mteja mwingine salio lililodundulizwa.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo