Lipa kwa Simu | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Lipa kwa Simu

Ufafanuzi wa Bidhaa:

Ni huduma mpya ya malipo ya kidigitali kutoka Tigo Pesa inayowezesha mteja yeyote kutoka kwa mtandao wowote nchini kufanya malipo ya bidhaa / huduma kwa njia rahisi, salama, na ya haraka.

Mfanyabiashara atakuwa na lipa namba na QR code ambazo zitaruhusu wateja kulipa kwa kuingiza lipa namba au kuskani picha ya QR.


Jinsi ya Kutumia:

MTEJA:

Kwenye USSD

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua 5 (Lipa kwa Simu)
 3. Chagua 1 (kwenda Tigo Pesa)
 4. Ingiza Lipa Namba
 5. Ingiza kiasi cha kulipa
 6. Ingiza namba ya siri kuthibitisha

Kwenye Tigo Pesa App

 1. Bonyeza kitufe cha Lipa Kwa Simu
 2. Chagua njia ya kufanya malipo kwa kuingiza lipa namba au kuskani picha ya QR
 3. Ingiza kiasi cha kulipa
 4. Ingiza namba ya siri kuthibitisha

MFANYABIASHARA:

Kwenye USSD

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua 5 (Lipa kwa Simu)
 3. Chagua namba 4 kuingia kwenye akaunti ya mfanyabiashara
 4. Chagua huduma ya Tigo Pesa unayotaka kutumia, kama; kutuma pesa, kutoa pesa, kuangalia salio na kadharika.

Kwenye Tigo Pesa App

 1. Bonyeza kitufe cha akaunti ya biashara
 2. Chagua akaunti ya Biashara
 3. Chagua huduma ya Tigo Pesa unayotaka kutumia, kama; kutuma pesa, kutoa pesa, kuangalia salio na kadharika.

Makato:


 

Maswali na Majibu:

  Lipa kwa Simu nini?

hili ni suluhisho jipya la malipo ya kidijitali kutoka Tigo, ambalo linaruhusu wateja kufanya malipo kwa kuskani QR au namba maalumu.

  Nawezaje kuunganishwa na huduma ya Lipa kwa simu?

Ili kuunganishwa utahitaji kuwa na hati zako halali za biashara kama cheti cha TIN, leseni ya Biashara na kwa Machinga utahitaji kitambulisho cha machinga tu.

  je kama mfanyabiashara ntapata faida gani kutumia huduma hii?

Zifuatazo ni faida anazopata mfanyabiashara kwa kutumia huduma hii.

 • Kutuma pesa benki kwa punguzo la asilimia 50 ya gharama za kawaida
 • Kutuma pesa kwa mfanyabiashara mwingine mwenye huduma hii kwa punguza la asilimia 50 ya gharama za kawaida
 • Usalama
 • Urahisi
 • Ongeza mauzo kwa kuwa na njia mbadala za kupokea malipo
 • Husaidia kuweka kumbukumbu za mauzo
  Je! Kuna ada zozote wakati mteja analipia bidhaa/huduma?

ndio, lakini ikiwa mteja analipa chini ya Elfu 20   hakutakuwa na makato lakini ikiwa malipo yapo juu ya Elfu 20 atatozwa nusu ya ada ya kawaida ya kutuma pesa.

  mnalindaje pesa zangu zisiweze kurudishwa na wateja wasio waaminifu pindi wanapofanya malipo?

Tuna ushirikiano mzuri na timu yetu ya huduma kwa wateja, hivyo hakuna muamala utakaorudishwa bila ya ridhaa ya mfanyabiashara.

  ninapofanya malipo kwa mfanyabiashara mwenye Lipa Hapa, je nahitaji kuongeza na ada ya kutolea kwa wakala?

hapana, atalipia kiasi kile kile.

  Naweza pokea malipo kutoka mitandao mingine na mabenki?

Ndio, unaweza kupokea malipo kutokea mitandao mingine hapa nchini.

  Je! ntatozwa kiasi gani kutoa pesa kutoka kwa akaunti yangu ya mfanyabiashara kwenda nambari yangu?

hakuna tozo zozote.

  Je! Ni kiwango gani cha juu ambacho akaunti yangu ya mfanyabiashara inaweza kushikilia/kutunza?

Akaunti ya mfanyabiashara inaweza kutunza mpaka TZS 50,000,000/-

  Je! Naweza kuwa na akaunti za mfanyabiashara zaidi ya moja?

Ndio, unaweza kuwa na akaunti zaidi ya kulingana na idadi ya biashara ulizonazo, na unaweza kufikia akaunti zote za biashara kwa kutumia nambari moja ya simu.

  ikiwa ninahitaji msaada kutoka kwenu, ninawezaje kuwasiliana nanyi?

ukihitaji msaada tafadhali piga 101 au tuma ujumbe mfupi kwenda WhatsApp 0677333100

Vigezo na Masharti:

 

 1. MTEJA:
  • Bidhaa hii inaweza kutumiwa na mteja yeyote kutoka kwenye mtandao wowote wa simu.
  • Ada za malipo kwa wateja wa mitandao mingine zitakua kama zilivyowekwa na mtandao husika.
  • Wateja wataweza kufanya malipo yasiozidi Milioni 5 za Kitanzania.
  • Tigo haitashiriki kwenye makubaliano yoyote kati ya mfanyabiashara na mteja.

 

 1. MFANYABIASHARA

  Nyaraka zinazohitajika ili kusajiliwa kwenye huduma:

  Kwa Wafanyabiashara wa kati

  • Cheti cha TIN
  • Leseni ya biashara
  • Namba ya Tigo iliyosajiliwa
  • Cheti cha Brela (Kama unataka kubadili jina lako na kuweka la biashara)

 

 1. Kwa Kampuni/Taasisi:
  • Cheti cha TIN
  • Leseni ya biashara
  • Namba ya Tigo iliyosajiliwa
  • memorandum and article of association
  • Barua ya utambulisho

 

 1. Kwa Machinga
  • Kitambulisho cha Machinga
  • Namba ya Tigo iliyosajiliwa

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo