Muhamala Uliokosewa | Tigo Tanzania

 Muhamala Uliokosewa

Tigo inashauri kuwa makini unapofanya muhamala ili kuondoa usumbufu na upotezaji wa pesa. Tigo itatuma meseji kwa mpokeaji na mtumaji wa pesa kuhabarisha kuwa muhamala umekosewa na pesa zitarudishwa kwa mtumaji.

Kama mpokeaji wa pesa anawasiwasi na kurudishwa kwa pesa, anashauriwa kupiga 100 na maelezo na muhamala husika ili kupata msaada

Ikiwa muhamala umekosewa, unashauriwa kupiga 100 mapema iwezekanavyo kupata msaada kutoka kwa watoa huduma kwa wateja wetu, Tigo haitahusika ikitokea muhamala uliokosewa utatumiwa na mpokeaji.

Muda wa mrejesho kwa muhamala uliokosewa

  • Kutuma Pesa : Tigo kwenda Tigo – Masaa 12 
  • Kutuma pesa :  Tigo kwenda mitandao mingine MNO’s (Voda, Airtel & Zantel) – Masaa 72 
  • Kutoa pesa      :  Masaa 24 
  • Kuweka pesa   :  Masaa 24
  • Kulipia bili  :  Masaa 72
  • Kuweka pesa kwenye akaunti ya benki: Masaa 72
  • Kutoa pesa kutoka akaunti ya benki : Masaa 72

Angalizo:

Masaa yaliyo orodheshwa hapo juu ni muda wa mihamala ya kawaida. Kwa mazingira yasiyo ya kawaida muda unaweza kuongezeka kutokana na muhamala husika

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo