Nunua Muda wa Maongezi | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Nunua Muda wa Maongezi

Nunua Muda wa Maongezi na Tigo Pesa:

Fikiri urahisi wa kuongeza salio muda wowote kutoka sehemu yoyote. Tigo Pesa inafanya huduma ya kununua muda wa maongezi na vifurushi rahisi kwa kutumia Tigo Pesa.

Jinsi ya Kununua Muda wa Maongezi kwa Tigo Pesa

1.       Piga *150*01#

2.       Chagua “2” kununua Muda wa Maongezi kwajili yako, familia yako na marafiki

Pata App ya Tigo Pesa ufurahie hudua ya pesa kwa urahisi, upesi na kuaminika zaidi. 


Jinsi ya kununua Muda wa Maongezi kwa kutumia App ya Tigo Pesa

 1. Fungua App ya Tigo Pesa

 2. Chagua Kuongeza Salio

 3. Unaweza kuchagua kuongeza salio kwa Simu Yangu kununua vocha kwaajili yangu , fanya chaguo jingine kununua kwaajili ya familia yako au marafiki

Pata App ya Tigo Pesa ufurahie hudua ya pesa kwa urahisi, upesi na kuaminika zaidi.


 

Maswali ya Mara kwa Mara:

  Mchakato wa kununua muda wa maongezi ukoje?
 • Piga *150*01#
 • Chagua 2 Muda wa Maongezi & Vifurushi
 • Chagua 1 kununua muda wa maongezi
 • Chagua kama ni namba binafsi/ingiza namba/chagua kwenye majina
 • Ingiza kiasi
 • Ingiza Namba ya Siri kuthibitisha

 

AU

Nenda kwenye App ya Tigo Pesa kisha chagua Mobile Shop na chagua Top Up(Jaza muda wa maongezi)

  Ni kiwango gani cha chini na cha juu ambacho mteja anaweza kutumia kununua muda wa maongezi?

Kiwango cha Chini kabisa ni Sh100 na Kiwango cha juu ni Sh50,000.

  Ni kiasi gani kitachajiwa kwa kununua muda wa maongezi

Hakuna gharama wala makato yoyote ya kununua muda wa maongezi kwa Tigo Pesa

  Nawezaje kujua salio langu?

Wateja wanaweza kujua salio kwa kupiga *102*00# au kwa kuangalia kupitia App ya Tigo Pesa.

  Naweza kurudisha kiasi cha muda wa maongzi nilionunua kimakosa?

Muamala wa muda wa maongezi hauwezi kurudishwa baada ya kukamilika.Hivyo, ni muhimu kuhakikisha namba ya mpokeaji na kiasi cha pesa  kwa umakini kabla ya kutuma.

  Inachukua muda gani kupata muda wa maongezi mara baada ya kununua?

Ni papo hapo hakuna kuchelewa

  Je kuna faida gani za kununua muda wa maongezi kwa Tigo Pesa?
 • Ni ya Uhakika.Mteja anatumia njia ya kidigitali na hakuna haja ya kutembea umbali mrefu kutafuta vocha.
 • Ni Nafuu: Unaweza kununua muda wa maongezi kwa kiwango cha chini cha Sh100.
 • Matumizi maradufu: Muda wa maongezi unaweza kutumika kupiga mitandao yote, SMS, Intaneti au ILD.
 • Ni Salama zaidi: Hakuna athari ukinunua muda wa maongezi kwa Tigo Pesa
 • Haraka:Mpokeaji anapata muda wa maongezi papohapo, mara tu ya muamala kuthibitishwa.

Vigezo na Masharti:

 • Mteja lazima awe amesajisajili na Tigo Pesa
 • Mteja anatakiwa awe na salio kwenye akaunti yake ya Tigo Pesa
 • Mteja wa Tigo Pesa anaweza kutumia salio kununua vifurushi mbalimbali vya Tigo.
 • Muda wa maongezi unaweza kutumika Kupiga Mitandao yote, SMS, VAS, Data (intaneti) na ILD.
 • Wateja wote wanaotumia Tigo Pesa wataweza kupokea muda wa maongezi kutoka kwa wateja wengine halali wa Tigo Pesa.
 • Endapo akaunti ya tigo Pesa imefungiwa au kuzuiliwa mteja hataweza kuhamisha muda wa maongezi.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo