Nyaka Nyaka Bonus | Tigo Tanzania

 Nyaka Nyaka Bonus

Nyaka Nyaka Bonus inamuwezesha mteja kupata mpaka bando la GB1 ambalo anaweza kutumia kwenye mitandao ya kijamii (Instagram, Twitter, Facebook na Whatsapp) baada ya kununua kifurushi cha intaneti kuanzia Tsh 1000 na zaidi kupitia *147*00#. Na pia mteja anaingia mojamoja kwenye droo inayomuwezesha kushinda simu ya 4G kila lisaa (Saa 3 asubuhi mpaka saa 9 jioni).  

BONASI:

Bonus za Nyaka Nyaka ni : 

  • Mpaka GB 1 za MB za bure

Pia kuingia moja kwa moja kwenye droo ambayo unaweza kujishindia simu ya Tecno R6 kila baada ya saa, kila siku.

MASWALI YA MARA KWA MARA

  Nyaka Nyaka Bonus ni nini?

Nyaka Nyaka Bonus ni Promosheni mpya kutoka Tigo inayomuwezesha mteja kupata Bonus za hapo kwa hapo mpaka GB1 za Social bando (Instagram, Twitter, Facebook na WhatsApp) pale mteja anaponunua vifurushi vya Intaneti kuanzia Tsh1000 au zaidi. Mteja anaingia moja kwa moja kwenye DROO ya kushinda SIMU JANJA kila saa (9am – 9pm)

  Ni vifurushi vinavyomuwezesha mteja kuingia kwenye?

Ni vifurushi vyote vya Intaneti kwenye Menyu ya *147*00# kuanzia Tsh1,000 au zaidi (vya Siku, Wiki au Mwezi) – vifurushi vyote vya intaneti vilivyopo sasa au vipya vitakavyotengenezwa vitakuwa kwenye promosheni.

  Ni Simu gani naweza kushinda?

Simu Janja ya Tecno R6 - 4G . Simu hii ni simu ya laini mbili na inakuwa imefungwa kwenye mtandao wa Tigo. Mteja anatakiwa kuweka laini yake kwenye SIM 1 ili aweze kutumia simu hiyo.

  Je ni faida gani nitapata nitakapojiunga na kifurushi cha intaneti?

Utapata BONUS za uhakika hapo hapo, utapata Bonus mpaka GB1 za Social Bundo (Instagram, WhatsApp, Facebook na Twitter). Katika Promosheni hii kila mteja ni mshindi.

  Je Bonus za Nyaka Nyaka ni za kutumia Muda gani?

Muda wa kutumia unaweza kuwa Siku, Wiki, au Mwezi kutokana na muda wa kifurushi chako ulichonunua na muda huu wa bonus utajulishwa unapopata bonus yako kwenye ujumbe.

  Je naweza kujiunga zaidi ya mara moja kupata Bonus?

Ndio, Unaweza kujiunga mara nyingi zaidi upendavyo. Kwa kila kifurushi utakachojiunga uta pata Bonus papo kwa hapo mpaka GB1 za social (WhatsApp, facebook , Twitter and Instagram)

  Je naweza pata Nyaka Nyaka Bonus kutoka kwenye menyu *148*00# au*148*01#?

Bonus zinapatika kwenye Menyu ya *147*00# Pekee. Hii ni Menyu iliyorahisishwa na inayotoa OFA nyingi.

  Je ni mara ngapi naweza ingia kwenye droo ya kushinda simu?

Utaingai kwenye droo kila saa unapojiunga na kifurushi cha intaneti kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 3 usiku. Na unaingia droo kila saa kutokana na muda ulionunua kifurushi.  

  Je naweza pata Nyaka Nyaka Bonus ninapongeza salio?

unaweza pata Bonus pale tu unaponunua kifurushi au vufurushi vya intaneti kuanzia Tsh1000 au zaidi kutoka kwenye Menyu ya *147*00#.

  Sijapata Bonus yangu baada ya kununua kifurushi

Kupata Bonus ni lazima ununue kifurushi cha intaneti kuanzaia 1,000 Tsh au zaidi kutoka kwenye Menyu ya *147*00#. Hutopata bonus ukinunua vufurushi vingine au mahali pengine au unapoongeza salio pekee. 

  Je nawezaje kuangalia salio langu la Bonus?

unaweza kuangalia salio kwa kupiga *147*102 # na utapokea ujumbe wenye salio lako la kawaida, salio la vifurushi vy intaneti, vifurushi vya dakika, SMS na hata Bonus zako.

  Je kuna tofauti gani kati ya Tumekusoma Bonus and Nyaka Nyaka Bonus

Nyaka nyaka Bonus inakuwezesha kufurahia MB BURE mpaka GB1 za Instagram, Facebook, WhatsApp na Twitter kuwasiliana na ndugu na marafiki unaponunua kifurushi cha intaneti kuanzaia 1,000 Tsh au zaidi. Zaidi ya hapo pia unapata nafasi ya Kushinda Simu Janja ya 4G.

 

 

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo