Pata App ya Tigo Pesa | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Pata App ya Tigo Pesa

App ya Tigo Pesa inafanya muamala wa simu wa pesa uwe wa haraka na rahisi zaidi. Kama hujapakua App hiyo bado basi hujui unachokosa! Angalia salio, tuma pesa, jaza salio kwenye simu yako, lipa bili, tuma pesa kwenye akaunti yako ya benki, toa pesa na vingine zaidi

Pakua na Sajili App ya Tigo Pesa kwa Hatua Rahisi  

A. Watumiaji wa Android

 1. Hakikisha una intaneti ya Tigo na umezima Wi-Fi kwa ajili ya kufanya usajili
 2. Nenda “Google play store”
 3. Tafuta Tigo Pesa App ”
 4. Chagua Tigo Pesa Tanzania App
 5. Chagua lugha Kiswahili/English
 6. App itatambua namba yako ya simu, bonyeza endelea
 7. Utapokea ujumbe mfupi wenye namba ya uthibitisho itakayojazwa moja kwa moja, endapo haijajazwa tafadhali weka namba hio kutoka kwenye ujumbe uliopokea.
 8. Ingiza namba ya Siri ya Tigo Pesa na utiki boksi chini yake kukubaliana na Vigezo na Masharti, kisha bofya Sajili

B. Mtumiaji wa IOS

 1. Hakikisha una intaneti ya Tigo na umezima Wi-Fi kwa ajili ya kufanya usajili
 2. Nenda “Apple Store”
 3. Tafuta Tigo Pesa App ”
 4. Chagua Tigo Pesa Tanzania App
 5. Chagua lugha Kiswahili/English
 6. App itatambua namba yako ya simu, bonyeza endelea
 7. Ingiza namba ya uthibitisho uliyopokea kwenye ujumbe mfupi wa simu.
 8. Ingiza namba ya Siri ya Tigo Pesa na utiki boksi chini yake kukubaliana na Vigezo na Masharti, kisha bofya Sajili

Pakua App ya Tigo Pesa Sasa! 

 

 

Maswali yanayoulizwa kuhusu App ya Tigo Pesa

  Je huduma zote za Tigo Pesa zinapatikana katika app ya Tigo Pesa?

Ndio, huduma zote muhimu za Tigo Pesa zinapatikana kama ilivyo kwenye Tigo Pesa ya kawaida. Kama vile

 • Kutuma pesa kwenda mitandao yote
 • Kutuma pesa kama vocha
 • Kutoa Pesa
 • Kulipia Bili
 • Kununua muda wa maongezi n vifurushi
 • Kupata taarifa fupi
 • Kutuma Pesa Benki
 • Kuangalia salio
 • Kuweka kumbukumbu
  Je natumia namba ya siri ile ile?

Ndio, utatumia namba ya siri ile ile unayotumiaga ukipiga *150*01#.

  Je naweza kutumia hatakama nipo mtandao mwingine?

Ndio,unaweza kutumia ukiwa mtandao wowote, unahitaji tu kuhakikisha namba yako ya Tigo ipo kwenye simu yako wakati wa usajili. Baada ya hapo unaweza kutumia Tigo Pesa App ukiwa mtandao wowote. 

  Nawezaje Kupakua Tigo Pesa App?

Mteja ataweza kupata App hiyo kwenye App store au tembele tovuti yetu ya Tigo kupata jinsi ya kupakua.

  Napata wapi LINK ya kupakua App

Link inapatika kwenye meseji tunazotumia wateja au kwenye tovuti yetu ya Tigo. Au tembelea App Store yako kupakua App ya Tigo Pesa. 

  Inachukua muda gani kupakua App?

Inachukua dakika chache na pia inategemea na Intaneti yako.

  Je, makato ni makubwa zaidi nikitumia App?

Hapana makato ni yale yale kama ya kawaida ya Tigo Pesa.

  Je, kuna makato yoyote ukipakua App?

Makato ni ya kawaida kama ya kudownload App nyingine.

  Inakuwaje kama App itaniletea ERROR?

Kama itatokea unapata tatizo angalia kama umeunganishwa na Intaneti  au wasiliana na huduma kwa wateja kwa msaada zaidi.

  Nahitaji nini kuweza kuipata?

Unahitaji Intaneti na simu ya yenye IOS au Android namba yako ya Tigo iliyosajiliwa Tigo Pesa

  Je, nikipoteza simu yangu?

Wasiliana na huduma kwa wateja kwa msaada zaidi na utaweza kuendelea kuitumia huduma kwenye simu nyingine kama kawaida na pesa zako zitakuwa salama maana kila muamala unahitaji namba ya siri.

  Hela zangu zinaweza ibiwa kama ntaibiwa simu yangu?

Hapana, pesa zako zitakuwa salama, mtu atahitaji namba yako ya siri kutumia Tigo Pesa yako. Ndio maana ni muhimu kutomwambia mtu yoyote namba yako ya siri.

  Najuaje kama simu yangu inaweza kukubali Application hii?

Unaweza kutembele tovuti yetu ya Tigo na kuangalia ni simu gani zinaweza kukubali APP hii.

  Inakuwaje kama nimesahau namba yangu ya siri?

Unaweza kureseti PIN yako kwa kupiga simu Huduma kwa wateja au kutembelea ofisi zetu za Tigo.

  Hii APP inaweza kufanya kazi hata nje ya Tanzania?

Ndio,unaweza kutumia App hii kokote Tanzania, unahitaji tu kuwa na Internet, WiFi/Data na vile vile unaweza kutumia mahali popote ulimwenguni , kama kawaida unahitaji internet kuweza kutumia APP hii.

  Je APP hii ipo katika lugha gani?

Application ipo katika lugha mbili, English na Kiswahili kumwezesha mteja kuweza kutumia huduma hii kwa lugha ambayo yuko vizuri nayo.

  Je naweza kuhifadhi kumbukumbu namba ya malipo yangu?

Ndio, inawezekana kuzihifadhi kumbukumbu namba kila mwisho wa muamala wako

  Usalama wa App

App hii ina usalama wa kisasa kukulinda wewe kama mteja, lakini tunapenda kukumbusha  umuhimu wa kutompa mtu PIN yako ya Tigo Pesa  na kujua kuwa Wafanyakazi wa Tigo hawatohitaji namba yako ya Siri kwa matumizi yoyote.

  Namba yangu itaweza kufanya kazi katika Tigo Pesa ya kawaida?(*150*01#)

Ndio utaweza tumia Tigo Pesa ya zamani na Application.

  Je naweza kuweka App hii kwenye simu tofauti

Ndio unaweza kuweka hii application kwenye simu nyingi na utaweza kuitumia kwenye zote kwa wakati mmoja, na utaweza kuangalia simu zote ambazo umesijali kwenye Application, na vile vile unaweza kuzitoa na kubaki na moja. Hakikisha tu namba yako ya Tigo unayotaka kutumia ipo ndani ya simu yako wakati wa usajili

  Jinsi ya Kupakua Tigo Pesa App

A.     Watumiaji wa Android 

 • Nenda “Google play store”
 • Tafuta Tigo Pesa  App ”
 • Chagua Tigo Pesa Tanzania App
 • Halafu “Unganisha”
 • Halafu “fungua”
 • Chagua Lugha Kiingereza/ Kiswahili
 • Sajili simu yako kwa kuingiza namba ya simu
 • Ingiza namba ya utambulisho uliyopokea kwenye ujumbe mfupi wa simu.

B.Mtumiaji wa IOS 

 • Nenda “Apple Store”
 • Tafuta Tigo Pesa App ”
 • Chagua Tigo Pesa Tanzania App
 • Halafu “Unganisha”
 • Halafu “fungua”
 • Chagua Lugha Kiingereza/ Kiswahili
 • Sajili simu yako kwa kuingiza namba ya simu
 • Ingiza namba ya utambulisho uliyopokea kwenye ujumbe mfupi wa simu.

 

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo