saizi yako | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 saizi yako

Kuhusu Saizi Yako:

Saizi Yako! Ofa maalum kwa bei nafuu zinazopatikana sehemu moja ndani ya menyu ya Saizi Yako.

Saizi Yako hizi ni ofa maalum na za kipekee zinazopatikana kwa wateja wote wa Tigo wa malipo ya kabla, zimetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa kila mteja kutokana na umri wa mteja katika Mtandao, matumizi ya mteja na eneo alilopo mteja.

Ofa zinapatika kwa bei nafuu na hivyo kutoa thamani ya pesa kwa wateja wetu wote

Faida za Saizi Yako:

 1. Ofa za Saizi Yako ni maalum na za kipekee zilizo tengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa kila mteja
 2. Ofa hizi zinapatikana sehemu moja maalum kupitia Menyu ya Saizi Yako katika Menu yetu kuu ya *147*00#
 3. Ofa za Saizi Yako zinapatikana kwa bei nafuu.
 4. Menyu ya Saizi Yako ni rahisi kutumia na kupatikana kwa urahisi

Jinsi ya kupata ofa za Saizi Yako:

Mteja anatakiwa kupiga *147*00# au *148*00# kisha chagua Saizi Yako na uchague kifurushi ukipendacho cha Saizi Yako.

Vigezio na Masharti vya Saizi Yako

Ustahiki na Upatikanaji wa Ofa za Saizi Yako:

 • Ofa hizi hupatikana kwa wateja wote wa Tigo wa malipo ya kabla nchini.
 • Mteja anatakiwa awe amesajiliwa katika mtandao wa Tigo.
 • Ofa za Saizi Yako zinapatikana kwa wateja wetu wote kuanzia tarehe 28 Mei, 2019
 • Ofa za Saizi Yako kwa wateja wapya wa Tigo hupatikana kwa kipindi cha siku 90 tangu kusajiliwa kwa Laini ya simu ya mteja.
 • Ofa za Saizi Yako zinaweza kubalidika kila baada ya siku 30. Mawasiliano yote ya ujumbe kwa wateja wetu kuhusu ofa za Saizi Yako huwekwa tarehe ya muda wa ofa wa kuanza na kuisha, hii humuwezesha mteja kujua muda wa ofa hiyo.

Jinsi ya kujiunga na Ofa za Saizi Yako:

Mteja anatakiwa kupiga *147*00# → Chagua Saizi Yako → kisha chagua kifurushi ukipendacho cha Saizi Yako.

Njia za malipo kwa Ofa za Saizi Yako:

Kuna njia mbili za malipo ambazo mteja anaweza kuchagua kutumia wakati wa kununua vifurushi vya Saizi Yako.

  1. Salio kuu la muda wa mongezi
  2. kupitia Tigo Pesa.

Njia hizi hupatiwa mteja pindi anapokuwa ananunua kifurushi

Ununuzi wa vifurushi zaidi ya mara moja:

Mteja anaweza kununua vifurushi zaidi ya mara moja kwa siku.

Kumnunulia rafiki:

Mteja hawezi kumnunulia rafiki kifurushi chochote cha Saizi Yako.

Kupitia menyu yetu ya *147*00# mteja anaweza akachagua vifurushi vingine vilivyopo nje ya Saizi yako kumnunulia Rafiki kifurushi wakati wowote kwa siku na anaweza kumnunulia kifurushi zaidi ya kimoja

Kugawa salio la kifurushi kwa mtu mwingine:

Kwa sasa Mteja hawezi kumgawia mtu mwingine salio la kifurushi alichonunua. Kumnunulia rafiki kifurushi, Mteja anatakiwa kununua kifurushi kingine kilicho nje ya Saizi Yako. Mteja anaweza kuchagua kifurushi chochote kupitia menyu yetu ya *147*00# na kuchagua namba 7 Mnunulie Rafiki.

Muda wa Kifurushi:

Kila kifurushi cha Saizi Yako kina muda wake wa kudumu. Salio la kifurushi kilichonunuliwa hudumu katika muda huo uliowekwa. Hii imewekwa wazi kwa kila kifurushi katika Menyu zetu za huduma na huwekwa bayana pia kabla mteja hajafanya manunuzi au kulipia

Kubeba salio la Kifurushi:

Mteja hawezi kubeba salio la kirufushi alichonunua. Hivyo Mteja anashauriwa kutumia salio la kifurushi chake alichonunua ndani muda wa kifurushi uliowekwa. Hii tumeiweka wazi kwa kila kifurushi katika Menyu zetu za huduma na huwekwa bayana pia kabla mteja hajafanya manunuzi au kulipia

Jinsi ya kuangalia salio la vifurushi vya Saizi Yako:

Piga *102*00# kisha utapokea ujumbe wenye salio la kifurushi

Matumizi ya salio la vifurushi vya Saizi Yako ndani na Nje ya Mtandao au Roaming:

Mteja anaweza kutumia salio lililopo kwenye kifurushi cha Saizi Yako ndani ya mtandao au mitandao mingine Tanzania na si kwa matumizi ya Roaming.

Kwa vifurushi vya kimataifa mteja anaweza kutumia kifurushi hicho kupiga simu nje ya nchi kulingana na aina ya kifurushi alichonunua na pia anaweza kutuma ujumbe mfupi nje ya nchi katika nchi zilizotajwa katika kifurushi hicho ikiwa kifurushi alichonunua kina salio la ujumbe mfupi. Mteja anaweza kujua kama kifurushi chake kina dakika na SMS pindi anapokuwa akinunua kifurushi katika menyu zetu za huduma.

Matumizi ya huduma nyingine:

 • Mteja hazuiliwi kutumia au kujiunga na huduma nyingine anapokua amejiunga na ofa za Saizi Yako.
 • Mteja anayenunua vifurushi vya Saizi Yako atafahamika kuwa amesoma, ameelewa na kukubali vigezo na masharti yaliyopo

Saizi Yako Maswali na Majibu

  Saizi Yako ni nini?

Saizi Yako hizi ni ofa maalum na za kipekee zinazopatikana kwa wateja wote wa Tigo wa malipo ya kabla, zimetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa kila mteja kutokana na umri wa mteja katika Mtandao, matumizi ya mteja na eneo alilopo mteja.

Ofa zinapatika kwa bei nafuu na hivyo kutoa thamani ya pesa kwa wateja wetu wote

  Zipi ni faida za Saizi Yako?
 1. Ofa za Saizi Yako ni maalum na za kipekee zilizo tengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa kila mteja
 2. Ofa hizi zinapatikana sehemu moja maalum kupitia Menyu ya Saizi Yako katika Menu yetu kuu ya *147*00#
 3. Ofa za Saizi Yako zinapatikana kwa bei nafuu.
 4. Menyu ya SAIZI YAKO ni rahisi kutumia na kupatikana kwa urahisi
  Jinsi gani naweza kupata ofa za Saizi Yako?

Mteja anatakiwa kupiga *147*00# au *148*00# kisha chagua Saizi Yako na uchague kifurushi ukipendacho cha Saizi Yako.

  Nani anaweza kupata ofa za Saizi Yako?
 • Ofa hizi hupatikana kwa wateja wote wa Tigo wa malipo ya kabla nchini.
 • Mteja anatakiwa awe amesajiliwa katika mtandao wa Tigo.
 • Ofa za Saizi Yako zinapatikana kwa wateja wetu wote kuanzia tarehe 28 Mei, 2019
 • Ofa za Saizi Yako kwa wateja wapya wa Tigo hupatikana kwa kipindi cha siku 90 tangu kusajiliwa kwa Laini ya simu ya mteja.
 • Ofa za Saizi Yako zinaweza kubalidika kila baada ya siku 30. Mawasiliano yote ya ujumbe kwa wateja wetu kuhusu ofa za Saizi Yako huwekwa tarehe ya muda wa ofa wa kuanza na kuisha, hii humuwezesha mteja kujua muda wa ofa hiyo.
  Jinsi gani naweza kujiunga na Ofa za Saizi Yako?

Mteja anatakiwa kupiga *147*00# → Chagua Saizi Yako → kisha chagua kifurushi ukipendacho cha Saizi Yako .

  Kuna njia zipi za malipo ninazoweza kutumia kununua Ofa za Saizi Yako?

Kuna njia mbili za malipo ambazo mteja anaweza kuchagua kutumia wakati wa kununua vifurushi vya Saizi Yako.

 1. Salio kuu la muda wa mongezi
 2. kupitia Tigo Pesa.

Njia hizi hupatiwa mteja pindi anapokuwa ananunua kifurushi

  Je, naweza kununua vifurushi vya Saizi Yako zaidi ya mara moja?

Mteja anaweza kununua vifurushi zaidi ya mara moja kwa siku.

  Je, naweza kumnunulia rafiki vifurushi vya Saizi Yako?

Mteja hawezi kumnunulia rafiki kifurushi chochote cha Saizi Yako.

Kupitia menyu yetu ya *147*00# mteja anaweza akachagua vifurushi vingine vilivyopo nje ya Saizi yako kumnunulia Rafiki kifurushi wakati wowote kwa siku na anaweza kumnunulia kifurushi zaidi ya kimoja

  Je, naweza kugawa salio la kifurushi kwa mtu mwingine kupitia kifurushi changu cha Saizi Yako nilichonunua?

Kwa sasa Mteja hawezi kumgawia mtu mwingine salio la kifurushi alichonunua. Kumnunulia rafiki kifurushi, Mteja anatakiwa kununua kifurushi kingine kilicho nje ya Saizi Yako. Mteja anaweza kuchagua kifurushi chochote kupitia menyu yetu ya *147*00# na kuchagua namba 7 Mnunulie Rafiki.

  Je vifurushi vya Saizi Yako vinadumu kwa muda gani?

Kila kifurushi cha Saizi Yako kina muda wake wa kudumu. Salio la kifurushi kilichonunuliwa hudumu katika muda huo uliowekwa. Hii imewekwa wazi kwa kila kifurushi katika Menyu zetu za huduma na huwekwa bayana pia kabla mteja hajafanya manunuzi au kulipia

  Je, naweza kubeba salio la Kifurushi changu cha Saizi Yako baada ya kununua kifurushi kingine?

Mteja hawezi kubeba salio la kirufushi alichonunua. Hivyo Mteja anashauriwa kutumia salio la kifurushi chake alichonunua ndani muda wa kifurushi uliowekwa. Hii tumeiweka wazi kwa kila kifurushi katika Menyu zetu za huduma na huwekwa bayana pia kabla mteja hajafanya manunuzi au kulipia

  Jinsi gani naweza kuangalia salio la vifurushi vya Saizi Yako?

Piga *102*00# kisha utapokea ujumbe wenye salio la kifurushi

  Je, naweza kutumia salio la vifurushi vya Saizi Yako ndani na Nje ya Mtandao au Roaming?

Mteja anaweza kutumia salio lililopo kwenye kifurushi cha Saizi Yako ndani ya mtandao au mitandao mingine Tanzania na si kwa matumizi ya Roaming.

Kwa vifurushi vya kimataifa mteja anaweza kutumia kifurushi hicho kupiga simu nje ya nchi kulingana na aina ya kifurushi alichonunua na pia anaweza kutuma ujumbe mfupi nje ya nchi katika nchi zilizotajwa katika kifurushi hicho ikiwa kifurushi alichonunua kina salio la ujumbe mfupi. Mteja anaweza kujua kama kifurushi chake kina dakika na SMS pindi anapokuwa akinunua kifurushi katika menyu zetu za huduma.

  Je, naweza kutumia huduma nyingine ninapokuwa numejiunga na kifurushi cha Saizi Yako?
 • Mteja hazuiliwi kutumia au kujiunga na huduma nyingine anapokua amejiunga na ofa za Saizi Yako.
 • Mteja anayenunua vifurushi vya Saizi Yako atafahamika kuwa amesoma, ameelewa na kukubali vigezo na masharti yaliyopo

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo