Soka | Tigo Tanzania

 Soka

Vigezo na Masharti vya promosheni ya “SOKA”

1. Vigezo na Masharti

a. Promosheni ya SOKA ni kwa wateja wa Tigo wa malipo ya awali tu

b. Muda wa promosheni: 1 Agosti 2018 hadi 31 Oktoba2018.

c. Kujiunga Mteja anatakiwa kutuma neon SOKA kwenda 15670. Kila swali analojibu anapata pointi. Kujibu maswali mengi ndio kujiongeze pointi nyingi na nafasi ya ushindi. Kila swali atakalotumiwa mteja atakatwa Sh 70/SMS.

d. Jinsi washindi watakavyo patikana:

Hakutakua na droo za bahati kwenye shindano hili. Ushindi utatokana na pointi za mchezaji au mteja. Mteja mwenye pointi nyingi ndiye mshindi.

Uchaguzi na upatikanaji wa washindi utafanyika chini ya usimamizi wa Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania (Gaming Board of Tanzania).

Washindi wote wa promosheni ya SOKA watapatikana kutokana na wingi wa pointi walizojikuSanyia. Mteja mwenye pointi nyingi Zaidi ya wenzake ndiye mshindi wa kipindi husika.

Mteja atakayeshiriki zaidi kwa kujibu maswali mengi atajiongezea nafasi za kuibuka mshindi kwa kujikusanyia pointi nyingi Zaidi.

ZAWADI ZITAKAZOTOLEWA

I. ZAWADI KUU: Mteja mmoja (1) atakayekuwa na pointi nyingi Zaidi ya washiriki Wengine atajishindia zawadi kuu ya PESA TASLIMU shilingi Milioni 10 (10,000,000/=). Mshindi huyu atapatikana mwisho wa promosheni hii.

Mshindi huyu atatangazwa ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupatikana.

II. WASHINDI WA WIKI: Kila wiki washindi WAWILI (2) watakao kuwa vinara wa pointi kwa wiki husika watajishindia zawadi za pesa taslimu Shilingi milioni Moja (1,000,000) kwa mshindi namba moja (1), na mshindi wa pili atajishindia Simujanja moja (1) yenye uwezo wa 4G. Washindi hawa watapatikana Tarehe 09/8/2018, 16/8/2018, 23/7/2018, 30/8/2018, 06/9/2018, 13/9/2018, 20/8/2018, 27/9/2018, 04/10/2018, 11/10/2018, 18/10/2018, 25/10/2018.

111.WASHINDI WA KILA MWEZI: Kila Mwezi mshindi Mmoja (1) atakaekua kinara wa pointi wa mwezi husika atajishindia zawadi ya Runinga (TV). Washindi hawa wa kila mwezi watapatikana tarehe 06/9/2018, 04/10/2018, 01/11/2018.

e. Washiriki ni lazime wawe na umri wa miaka 18 au Zaidi

f. Kujiunga Mteja anatakiwa kutuma neno SOKA kwenda 15670. Kujiunga na huduma hii ni BURE. Baada ya kujiunga Mteja atapokea maswali kuhusu kandanda. Kila swali atakalojibu anapata pointi. Kujibu maswali mengi ndio kujiongeze pointi nyingi na nafasi ya ushindi. Kila swali atakalotumiwa mteja atakatwa Sh70/SMS.

g. Mteja akituma neno au jibu lisilo sahihi kwenda namba 15670, ujumbe huu utachukuliwa kama jibu lisilo sahihi. Atapokea ujumbe wa kumfahamisha kuwa jibu lake sio sahihi na jinsi ya kujibu kwa usahihi kisha kumtumia swali jipya endapo ana salio la kutosha. Kila swali atakalotumiwa mteja atakatwa Sh70/SMS.

h. Kila jibu sahihi mteja atapata pointi 100 (mia moja) na jibu lisilo sahihi atapata pointi 25 (ishirini na tano).

i. Shindano hili litahusisha maswali ya kuhusu mpira wa miguu yanayolenga kuburudisha, kuelimisha na kumpatia nafasi Mteja kuwa kati ya mmoja wa washindi wa Runinga za Kisasa (LED TV), pesa taslimu shilingi Milioni Moja (1,000,000), Laki moja (100,000), Simu Janja na zawadi kuu ya Pesa Taslimu Shilingi Milioni 10 (10,000,000) mwishoni mwa promosheni hii.

j. Kujitoa kwenye huduma hii Mteja anatakiwa kutuma maneno ONDOA SOKA kwenda namba 15670.

k. Hakuna gharama za kujitoa.

l. Kama mteja akijishindia zawadi na wakati wa kumpigia simu ili kumtaarifu, simu ya mteja huyo aliyeshinda ikawa haipatikani au mteja huyo akipigiwa simu mara tatu pasipo kupokelewa, mteja huyo atapoteza haki yake ya ushindi wa zawadi husika. Mteja anayefuatia kwa pointi atateuliwa kuwa mshindi mpya.

m. Mshindi yeyote aliyepigiwa kutaarifiwa kuwa mshindi na hakupokea simu mara tatu (3) au simu haipatikana hatokuwa na haki ya kudai zawadi.

n. Zawadi zote zitakabidhiwa katika ofisi za Tigo baaada ya mshindi kuthibitisha kwa kitambulisho kama yeye ndio mshindi halali.

o. Mshindi anaweza kushinda aina moja ya zawadi mara moja tu. Yaani Mteja akishinda zawadi ya wiki hatoruhusiwa kushinda tena zawadi ya wiki kwa wiki zinazofuatia.

p. Tigo itabakia na zawadi za washindi wote amboa wakati wa ushindi wao hawakuweza kufika katika ofisi za Tigo kwa wakati mpaka watakapokuja kuzichukua.

q. Tigo itabakia na zawadi ya mshindi ambayo haijachukuliwa kwa kipindi cha miezi 3, baada ya hapo mshindi atakua amepoteza haki ya ushindi wa zawadi hiyo.

r. Majina ya washind, picha na video za washindi wa zawadi kupitia promosheni ya “SOKA” watakuwa wakitangazwa kupitia vyombo vya habari.

s. Kwa kushiriki, mshindi anaipatia kampuni ya Tigo haki ya kumtangaza na kutumia jina, picha na video ya mhusika kama mshiriki na mshindi kwenye vyombo vya habari kwa kipindi chote cha promosheni hii.

t. Wafanyakazi wa kampuni za Tigo na Green Telecom na familia zao hawaruhusiwi kushiriki kwenye promosheni hii.

u. Promosheni hii ni kwa ajili ya watanzania na wageni wenye vibali vya ukazi (residence permits) Tu.

v. Majina ya washindi yatatangazwa kwenye vyombo vya habari vitakavyochaguliwa.

w. Namba na idadi za wateja walioshiriki promosheni hii yatakuwa katika taarifa na kumbukumbu za kampuni za Tigo na Green Telecom.

x. Zawadi zote za PESA TASLIMU zitakatwa kodi kwa niaba ya TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania ya 10%

y. Kampuni ya Tigo itabaki na haki ya kubadili vigezo na masharti vya promosheni hii wakati wowote kwa kutoa taarifa kwa Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania (Gaming Board of Tanzania).

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo