TIGO LUCKY VIDEO QUIZ | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..


 TIGO LUCKY VIDEO QUIZ

Tigo Lucky Video Quiz:

Hii ni huduma inayomuwezesha mteja kujibu maswali ya video amabpo kila swali anapojibu anapata pointi zitazomuwezesha kushinda pesa taslimu.


Jinsi Ya Kujiunga:

 1. Kwa SMS-15724

  Mteja anaweza kujunga kwa kutuma neno QUIZ kwenda 15724 na atakatwa Tsh300 kwenye salio la muda wa maongezi.

  Mteja atakatwa Tsh300 kila siku na kupata sarafu 15 kwa ajili ya kujibu maswali.

 2. Kwa tovuti

  Mteja anaweza kujuinga kwa kubofya hapa https://theluckyquiz.com kwa Tsh300 kwenye salio la muda wa maongezi.

  Mteja atakatwa Tsh300 kila siku na kupata sarafu 15 kwa ajili ya kujibu maswali.

Endapo mteja atamaliza sarafu zake anaweza kununua sarafu nyinginev kupitia tovuti au kwa SMS.


Jinsi ya Kununua Sarafu:

1. Kununua kwa njia ya SMS:

Mteja anaweza kununua sarafu kwa kutuma Maneno yafuatayo kwenda 15724

 • QUIZ100 kupata sarafu 5(kwa 100Tsh)
 • QUIZ200 kupata sarafu 10(kwa 200Tsh)
 • QUIZ300 kupata sarafu 15(kwa 300Tsh)

2. Kununua kwa tovuti:

Mteja anaweza kununua sarafu kwa tovuti kwa kubonyeza Nunua Sarafu’ na kuchagua

 • Sarafu 5(kwa Tsh100T)
 • Sarafu 10(kwa Tsh200T)
 • Sarafu 15(kwa Tsh300T)

Jinsi invofanya kazi:

 • Mteja anatakiwa kutambua majina ya ppicha au video sitakazonekana wakati anacheza
 • Mteja atatumia sarafu zake zitakazomuwezesha kushiriki kwenye mchezo
 • Wateja kenye point nyingi watapata nafasi kushiriki kwenye droo ili kupata mshindi wa Siku,Wiki na droo kubwa.

Mteja anaweza kujiunga kwa njia ya sms au tovuti kwa Tsh300 and atapatiwa sarafu 15 za kuanzia lakini anaweza kununua sarafu nyingine zaidi kujibu maswali mengi zaidi na kupata nafasi ya kushinda.


Maswali na Majibu:

  Lucky Video Quiz ni nini?

Lucky Video Quiz ango ambalo hutoa maswali ya video kwa wateja wa Tigo kujibu na kukusanya alama. Wateja walio na alama za juu watachorwa, na mshindi atapewa tuzo kwa kipindi hicho (kila siku, kila wiki au robo).

  Je, nawezaje kushiriki kwenye hii promosheni?

Unaweza kushiriki kwa kutuma QUIZ kwenda 15724 au kutembelea https://theluckyquiz.com

  Je, kuna aina ngapi za zawadi zinazowaniwa?

Kuna aina tatu za zawadi nazo ni zawadi za kila siku, zawadi za kila wiki na zawadi kubwa ya mwisho wa mwezi.

  Je, nitaingia gharama za ziada kwa kushiriki katika promosheni hii?

Ndio. Itakugharimu Tsh300 kujiunga na huduma hii. Unaweza kununua sarafu 5 kwa Tsh100. Sarafu 10 kwa Tsh200 na sarafu 15 kwa Tsh300.

  Promosheni hii ni kwa ajili ya wateja wa aina gani?

Hii promosheni ni kwa ajili ya wateja wa malipo ya kabla na hybrid.

  Nitajuaje nimeshinda zawadi?

Tigo itawapigia washindi wote waliobahatika kuwataarifu juu ya ushindi wao na jinsi ya kukusanya zawadi zao.

  Bado sijafikisha miaka 18, naweza kushiriki?

Washiriki lazima wawe na umri wa miaka kumi na nane (18) na Zaidi.

  Mimi ni mteja wa malipo ya baada, je ninaweza kushiriki kwenye hii promosheni?

Hapana. : Hii promosheni ni kwa ajili ya wateja wa malipo ya kabla na hybrid.

  Je, Nikishinda zawadi yangu itatozwa kodi? Nani atalipa kodi?

Makato ya kodi kwa michezo ya bahati nasibu kwenye zawadi zote za fedha ni 20%. Hiki kiasi kitalipwa na mshindi wa zawadi.

  Je, nikishinda na ikawa sina nauli ya kuja kuchukua zawadi yangu, nini kitatokea kwa zawadi yangu?

Mwakilishi wa Tigo atakupigia simu na kuangalia uwezekano wa kukufikia na wawakilishi wetu waliopo karibu na wewe.

  Je, itakuwaje pale ambapo nitashinda na sitokuja kuchukua zawadi yangu?

Tigo itabakia na zawadi ya mshindi kwa muda wa miezi mitatu (3) endapo mshindi huyo hatojitokeza kuichukua zawadi yake. Baada ya muda huo mshindi hatokuwa na haki ya kuichukua zawadi.

  Ni wapi naweza kupata vigezo na masharti ya promosheni hii?

Maelezo kuhusu Vigezo na masharti ya pomosheni hii yanapatikana kwenye tovuti yetu. (www.tigo.co.tz)

  Je, nikishinda lakini nipo mkoani napataje zawadi yangu? Itabidi nije makao makuu ya Tigo Dar?

Kama upo mkoani, Tigo itapanga na mwakilishi wa mkoa ili kukufikia.

  Mimi sio Mtanzania, ninaweza kushiriki na kushinda tuzo?

Hapana, promosheni hii iko wazi kwa Watanzania tu.

  Ninaweza kupata msaada wapi / kutuma maswali yangu kuhusu hii promosheni?

Piga 100, tembelea duka lolote la Tigo au tembelea tovuti yetu (www.tigo.co.tz)

  Je, naweza kushinda kwenye droo na kuchagua nisitangazwe?

Hapana, majina ya washindi yatatangazwa au kuchapishwa katika vyombo vya habari vilivyochaguliwa na waendesha kampeni.

  Je, nikishinda, lakini sikuweza kupokea simu wakati wanapigia mshindi kwenye droo?

Mshindi yeyote ambaye alipigiwa simu na hakupatikana au hakujibu simu mara 3 hatokuwa na ruhusa ya kudai zawadi. Katika tukio kama hilo mtumiaji anayefatia kwa wingi wa pointi atapigiwa simu na akipatikana atatangazwa kuwa mshindi.

Vigezo na Masharti:

 

 1. Washiriki lazima wawe na umri wa miaka kumi na nane (18) na zaidi kushiriki.
 2. Kuanzia tarehe 1 Julai 2019 na kuendelea makato ya ushuru kwa michezo ya Bahati Nasibu kwenye zawadi zote za fedha ni 15%.
 3. Waajiriwa wa ZingAfric na Tigo pamoja na familia zao hawana ruhusa ya kushiriki kwenye kampeni hii.
 4. Mteja anatakiwa ajiunge kwa kutuma QUIZ kwenda 15724 au kutembelea https://theluckyquiz.com
 5. Mteja anaweza kununua sarafu 5 kwa Tsh100, sarafu 10 kwa Tsh200 na sarafu 15 kwa Tsh300.
 6. Kadiri mteja anavyojibu maswali zaidi ndivyo anavyozidi kujiongezea nafasi ya USHINDI kwa kujikusanyia pointi nyingi zaidi.
 7. Washindi wote watachaguliwa kulingana na pointi walizokusanya. Mteja atakayekuwa amekusanya pointi zaidi ya wengine ndani ya muda wa kutoa Zawadi ndiye atakayechaguliwa kuwa Mshindi
 8. Endapo kutakuwa na watu wawili au zaidi wana pointi sawa basi mtu aliyepata pointi nyingi ndani ya muda mfupi ndiye atakuwa mshindi.
 9. Baada ya kujiunga na huduma, mteja atakuwa ametoa idhini na kuanza kupokea ujumbe mfupi wa kushawishi wa huduma.
 10. Tigo inaweza kutumia baadhi ya taarifa kama picha, sauti au video za mshindi aliyeshinda zawadi ya kampeni hii kwa kipindi chote cha kampeni kwa ajili ya uhamasishaji wa kampeni
 11. Majina ya washindi yatatangazwa au kuchapishwa katika vyombo vya habari vilivyochaguliwa na waendesha kampeni.
 12. Zawadi zote zitakabidhiwa katika ofisi za Tigo.
 13. Mshindi yeyote ambaye alipigiwa simu na hakupatikana au hakujibu simu mara 3 hatokuwa na ruhusa ya kudai zawadi. Katika tukio kama hilo mtumiaji anayefatia kwa wingi wa pointi atapigiwa simu na akipatikana atatangazwa kuwa mshindi.
 14. Tigo itabakia na zawadi ya mshindi kwa muda wa miezi mitatu (3) endapo mshindi huyo hatojitokeza kuichukua zawadi yake. Baada ya muda huo mshindi hatokuwa na haki ya kuichukua zawadi.
 15. Namba ya mteja lazima iwe imesajiliwa kwa alama za vidole ili kufuzu kushiriki kwenye hii huduma.
 16. Promosheni hii iko wazi kwa wakazi wa Tanzania tu.
 17. Tigo inaweza wa kubadilisha vigezo na masharti muda wowote kwa kupeleka mapendekezo yao katika Taasisi ya Kuratibu Mashindano ya Bahati Nasibu (Gaming Board of Tanzania).

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo