Tigo Pesa Kibubu | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Tigo Pesa Kibubu

TIGO PESA KIBUBU:

Tigo Pesa Kibubu ni huduma ya kuweka akiba ambayo inawawezesha wateja wetu kujenga mfumo wa kujiwekea akiba kwa njia ya kidigitali wakiwa na laini ile ile ya Tigo. Kwa kushirikiana na Bank of Afrika (BOA), huduma hii inawawezesha wateja wetu kuweka akiba ya hadi milioni 10 za kitanzania kwenye akaunti zao za Kibubu.

Hii itawaruhusu wateja wote waliosajiliwa na Tigo Pesa kuweka akiba kiurahisi kutoka kwenye akaunti zao kuu za Tigo Pesa kwenda kwenye akaunti za akiba bure na kupata gawio kila mwisho wa mwezi.


Muongozo wa Utumiaji kwa USSD:

Weka akiba na Tigo Pesa Kibubu:

 • Piga *150*01#
 • Chagua 7 – Huduma za kifedha
 • Chagua 8 – Akiba
 • Chagua 1- Tigo Pesa Kibubu (Akiba)
 • Chagua 1 - Weka kwenye Kibubu
 • Ingiza namba ya siri ya Tigo Pesa Kuthibitisha
 • Utapokea ujumbe wenye kumbumbuku za akiba yako

Hamisha Kutoka akaunti ya Kibubu:

 • Piga *150*01#
 • Chagua 7 – Huduma za Kifedha
 • Chagua 8 – Akiba
 • Chagua 1- Tigo Pesa (Kibubu)
 • Chagua 2 - Kuhamisha kutoka Kibubu.
 • Enter your Tigo Pesa PIN to confirm
 • Utapokea ujumbe wenye kumbukumbu za hamisho lako.

Angalia salio la Kibubu:

 • Piga *150*01#
 • Chagua 7 – Huduma za Kifedha
 • Chagua 8 – Akiba
 • Chagua 1- Tigo Pesa (Kibubu)
 • Chagua 3 – Salio la Tigo Pesa Kibubu.
 • Ingiza namba ya siri kuthibitisha
 • Utapokea ujumbe wenye kumbukumbu za hamisho lako.

Muongozo wa Utumiaji kwa APP:

Weka akiba na Tigo Pesa Kibubu:

 • Fungua App ya Tigo Pesa
 • Chagua Huduma za Kifedha
 • Chagua Akiba
 • Chagua Weka kwenye Kibubu kuweka kiasi unachotaka kuweka akiba.
 • Ingiza namba ya siri kuthibitisha
 • Utapokea ujumbe wenye kumbumbuku za akiba yako

Hamisha Kutoka akaunti ya Kibubu:

 • Fungua App ya Tigo Pesa
 • Chagua Huduma za Kifedha
 • Chagua Akiba
 • Chagua Hamisha kutoka Kibubu kuingiza kiasi unachotaka kuhamisha kutoka Tigo Pesa Kibubu.
 • Ingiza namba ya siri kuthibitisha
 • Utapokea ujumbe wenye kumbukumbu za hamisho lako.

Angalia salio la Kibubu:

 • Fungua App ya Tigo Pesa
 • Chagua Huduma za Kifedha
 • Chagua Akiba
 • Chagua Angalia salio
 • Ingiza namba ya siri kuthibitisha
 • Utapokea ujumbe wenye salio lako la Kibubu.


Maswali na Majibu:

  TigoPesa Kibubu ni nini?

TigoPesa Kibubu ni huduma inayokuwezesha kuweka akiba binafsi kwa kuunganisha akaunti kuu ya TigoPesa na akaunti ya Tigo Pesa Kibubu.

  Je! TigoPesa Kibubu inafanyaje kazi?

TigoPesa Kibubu inaunganisha akaunti kuu wa TigoPesa na akaunti yaTigoPesa Kibubu inayomwezesha mteja kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti moja kwenda nyingine.

  Je! Kuna ada yoyote inayotumika kwa mteja wakati anatumia huduma za Kibubu?

Hakuna ada itakayotumika wakati wa kutumia huduma.

  Ninawezaje kufikia huduma ya TigoPesa Kibubu kwenye USSD?

Piga * 150 * 01 #, Chagua Huduma za Kifedha (7), >> Akiba (8) >> TigoPesa Kibubu (Akiba ya Binafsi) (1), kisha fuate maelekezo.

  Ni kiwango gani cha chini ambacho mteja anaweza kuweka kwenye akaunti ya TigoPesa Kibubu?

Mteja anaweza kuweka kiasi kuanzia TZS 1  hadi kiwango chochote kwenye TigoPesa Kibubu ilimradi tu kiasi hicho kipo kwenye akaunti kuu ya TigoPesa.

  Je! Ni kiwango gani cha chini ambacho mteja anaweza kutoa kutoka kwa akaunti yake ya TigoPesa Kibubu?

Mteja anaweza kutoa kiasi chochote cha chaguo na TigoPesa Kibubu hadi kiwango cha juu kabisa kinachopatikana katika akaunti yake ya TigoPesa Kibubu.

  Je! Mteja anaweza kuangalia salio la kwenye TigoPesa Kibubu?

Ndio, Mteja anaweza kuangalia salio la akaunti yake ya TigoPesa Kibubu kupitia njia ya USSD kwa kupiga *150*01# kisha chagua 6 (Jihudumie- akaunti na Salio) kisha chagua 3 kuangalia salio kisha chagua namba 2 Salio la Tigo Pesa Kibubu.

  Je! Mteja atapata nini kwa kuweka akiba na TigoPesa Kibubu?

Mteja atapata gawio kwenye akaunti kuu ya Tigo Pesa kila mwisho wa mwezi.

  Gawio hilo litalipwa lini na kwa njia gani?

Gawio litalipwa kwenye akaunti kuu ya Tigo Pesa katika siku chache za kazi mwanzoni wa mwezi mpya.

  Ni lini mteja anaweza kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yake ya TigoPesa Kibubu?

Mteja anaweza kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yake TigoPesa Kibubu hadi kiwango cha juu kinachopatikana katika akaunti hiyo muda wowote atakapohitaji kufanya hivyo.

  Je! Ni vipi naweza kupata msaada?

Tafadhali, Piga 100 kuwasiliana na Huduma Kwa Wateja kwa msaada zaidi.

Vigezo na Masharti:

 

 1. Kila mteja kwenye namba ya simu ileile, atakuwa na akaunti ya pili mbali na ile ya awali ambayo inatumika kufanya miamala ya kawaida bila gharama yoyote..
 2. Akaunti ya sasa itabaki kuwa akaunti KUU ambayo itatumika kwaajili ya miamala ya kawaida kama ilivyo sasa.Hakuna mabadiliko yoyote kwenye matumizi katika akaunti ya KUU.
 3. Akaunti ya pili itakuwa akaunti ya Tigo Pesa Kibubu
 4. Tigo Pesa Kibubu itatumika tu kuhifadhi pesa kwa matumzi ya baadae. Pia, haitawezekana kufanya miamala ya kawaida kwenye akaunti hii isipokuwa kuweka na kutoa pesa pekee.
 5. Pesa zitawekwa kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu kwa kuzitoa kwenye akaunti KUU na pia pesa zitatolewa kutoka kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu kwa kuziingiza kwenye akaunti KUU.
 6. Kiasi kile kile na Kiwango cha mwisho cha kufanya miamala kinachotumika kwenye akaunti Kuu ndicho kitatumika kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu (Hii inategemea na aina ya mteja)
 7. Pesa zilizopo kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu zitaweza kupata gawio kulingana na kiasi na muda ambao zimehifadhiwa na pia gawio hilo litajulishwa kwa mteja.
 8. Wateja wataweza kutunza pesa kiasi chochote cha pesa kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu na pia wataweza kutoa kiasi chote au kiasi fulani kutoka akaunti ya Tigo Pesa Kibubu na kwenye akaunti kuu vilevile kama sheria za matumizi ya miamala zisemavyo.
 9. Tigo itatoza gharama ya huduma ya kawaida kwenye akaunti ya kawaida ya Tigo Pesa huku huduma kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu itakuwa BURE. Endapo kutakuwa na gharama zozote zitakazojitokeza zitaoneshwa kwa mteja kabla ya kutumia huduma na gharama hizo zitawasilishwa Benki Kuu baada ya kuzindua au kabla ya kufanya mabadiliko kwenye huduma.
 10. Gawio atakayopata mteja italipwa moja kwa moja kwenye akaunti KUU ya mteja ya Tigo Pesa kila mwezi i kulingana na kiwango cha gawio kitakachokua kimepangwa na Bank na Tigo Pesa.
 11. Gawio la mpaka 7% kwa mwaka linalojumuishwa kila siku na kulipwa kila mwisho wa mwezi.
 12. Kiwango cha gawio cha kila siku kinapatikana kwa kugawanya kiwango cha gawio cha kila mwaka na siku 365. Hesabu yako ya gawio inategemea kiwango cha pesa ulichonacho kwenye akaunti yako Tigo Pesa Kibubu kila mwisho wa siku.
 13. Gawio itakayolipwa kila mwezi ni mjumuisho wa gawio ya kila siku ya mwezi husika . Gawio hii italipwa italipwa kwenye akanti KUU ya Tigo Pesa.
 14. Pesa zitakazo hifadhiwa kwenye Tigo Pesa Kibubu zitaanza kupata gawio siku hiyo hiyo endapo zitahidhifadhiwa kabla ya muda wa kufnga biashara. Pesa zitakazo hifadhiwa baada ya muda wa kufunga biashara zitaanza kupata gawio siku inayofuata (Muda wa kufunga biashara ni saa nane kamili mchana <08:00> na muda huu unaweza kubadilika kulingana na masharti ya uendeshaji biashara). Pesa iliyopo kwenye kibubu haitopata gawio siku itakayo tolewa kwenye kibubu. Gawio ya pesa zilizohifadhiwa siku za mwisho wa wiki (Jumamosi na Jumapili) na siku za sikukuu itahesabiwa siku za kazi zinazofuata.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo