Tigo Pesa Nivushe FAQs | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..Tigo Pesa Nivushe FAQs

Tigo inatoa mikopo kwa wateja waliochaguliwa ambao wanatumia huduma za muda wa maongezi, intaneti, meseji, malipo ya bili na huduma mbalimbali za Tigo Pesa. Utapokea meseji pindi utakapokidhi vigezo vya kupata mkopo. Ili kukidhi vigezo vya mkopo, endelea kutumia huduma za Tigo na Tigo Pesa mara kwa mara. 

Piga *150*01# chagua 7 Huduma za kifedha kisha chagua 4 Tigo Nivushe kwenye laini yako ya Tigo kisha chagua 1. Itakupasa kuchagua muda unaohitaji kurejesha mkopo na kiasi cha mkopo unachohitaji, Kisha utaingiza namba ya siri. Kama utapata meseji kuwa haujakidhi vigezo, basi utakuwa hauwezi kupata mkopo bado. Ili kukidhi vigezo vya mkopo, endelea kutumia huduma za Tigo na Tigo Pesa mara kwa mara. 

Nivushe inatoa mikopo kuanzia Tsh1,000 kwa wateja ambao hawajawahi kuchukua mkopo. Kiasi unachopata kinategemea na matumizi yako ya akaunti ya Tigo Pesa na huduma zingine za Tigo kama muda wa maongezi, intaneti na meseji.

Unaweza kupata mikopo ya siku 7, 14, 21 na 30. Marejesho yatakatwa kutoka kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa mwisho wa muda wa marejesho uliochagua.

Ada ziko tofauti kwa kila mteja. Ada itaonyeshwa kabla haujachukua mkopo.  Wateja wenye historia nzuri (kama  kulipia bili na kutuma  pesa kwa akaunti zao za Tigo Pesa na pia kurejesha mikopo kwa wakati) watapata ada nafuu zaidi.

Unaweza kuchukua mkopo mmoja tu kwa wakati, lakini pindi utakapomaliza marejesho unaweza kupata mkopo mwingine. Mkopo unaofuata unaweza kuwa mkubwa, kama utarejesha kwa wakati na kutumia akaunti yako ya Tigo Pesa na huduma zingine za Tigo kama muda wa maongezi, intaneti na meseji.

Piga *150*01# chagua 7 kwa ajili ya Huduma za kifedha na chagua  4 Tigo Nivushe kisha chagua 3 "Angalia Salio la mkopo", ili kuangalia salio la mkopo

Kurejesha mkopo wako wa Nivushe hakikisha unapesa ya kutosha kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa siku ya marejesho ikifika, na Nivushe itakata pesa kutoka kwenye akaunti yako. Na kama unataka kurejesha kabla au baada ya wakati, Piga *150*01# chagua 7 Huduma za kifedha kisha chagua 4 Tigo Nivushe, kisha chagua 2 "Rejesha Mkopo". Unaweza kuchagua kurejesha kiasi chote cha mkopo au sehemu ya kiasi cha mkopo kisha utaingiza namba yako ya siri kuthibitisha marejesho.

Kurejesha mkopo kabla ya siku ya marejesho, Piga *150*01# chagua 7 Huduma za kifedha kisha chagua 4 Tigo Nivushe kisha chagua 2 "Rejesha Mkopo". Unaweza kuchagua kurejesha mkopo wote, au sehemu ya mkopo kisha unaingiza namba ya siri kuthibitisha ombi lako.

Ndio, unaweza. Ni vizuri na rahisi zaidi kurejesha hata sehemu ndogo ya mkopo kama utaweza, kwasababu itakusaidia kupunguza kiasi cha ada ya ziada, kama utachelewa kurejesha mkopo wako.

Kama hautorejesha mkopo wako kwa wakati utatozwa mpaka 10% ya kiasi ambacho hakijarejeshwa kama ada ya kuchelewesha marejesho. Utapokea ujumbe mfupi kabla ya siku ya marejesho, ili kukukumbusha kuwa unatakiwa kurejesha mkopo. Ukichelewesha marejesho mkopo wako unaofuata unaweza kushuka, na kama utaendelea kuchelewesha marejesho mara kwa mara unaweza kuondolewa kweye huduma ya mkopo.

Tumia akaunti yako ya Tigo Pesa kufanya malipo na kuhamisha pesa mara kwa mara, hakikisha unarejesha mikopo yako kwa wakati. Kiasi cha mkopo unachopata kinategemea matumizi yako ya huduma za Tigo kama muda wa maongezi, intaneti, meseji, malipo ya bili mbali mbali na miamala ya Tigo Pesa na pia kwa kuangalia kama unarejesha mikopo yako kwa wakati, kila mara.

Kama umechelewesha marejesho ya mkopo wako mmoja, au matumizi yako ya Tigo Pesa na huduma zingine za Tigo yameshuka kuliko mwanzo. Kiasi cha mkopo unachopata kinategemea matumizi yako ya huduma za Tigo kama muda wa maongezi, intaneti, meseji, malipo ya bili mbali mbali na miamala ya Tigo Pesa na pia kwa kuangalia kama unarejesha mikopo yako kwa wakati, kila mara.

Angalia ujumbe unaoupata unasema nini, kama ni "hauna vigezo" au ni "umefikia kiwango cha mwisho cha siku". Kama umefikia kiwango chako cha mwisho, jaribu tena baada ya siku chache. Kama hauna vigezo, kumbuka kwamba ili uweze kupata mkopo inakupasa kulipia bili na kufanya miamala mbali mbali kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa mara kwa mara na pia kurejesha mikopo yako kwa wakati kila mara.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo