Tigo Pesa FAQs | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..Tigo Pesa FAQs

Huduma hii inawasaidia wateja wenye mita za zamani za Tanesco kuliopa bili kutumia Tigo Pesa.

  • Piga *150*01#
  • Chagua namba 4 “malipo”
  • Chagua namba 3 "kupata kumbukumbu namba "
  • Chagua namba 3 "chagua kampuni"
  • Kwenye orodha utapata chaguo la kulipa BILI 

Hatushauri wafanyabiashara kutoa pesa kwasababu wanaweza kufanya shughuli mbali mbali na hela iliopo kwenye akaunti, unaweza fanya ifuatavyo.

  • Unaweza kuongeza bidhaa zako kwakulipa wasambazaji waliojisajili.
  • Unaweza kuhamisha salio la hela kwenda kwenye akaunti ya benki.
  • Unaweza kulipia bili tofauti zilizopo kwenye menyu ya Tigo Pesa.
  • Unaweza hamisha hela kutoka akaunti ya Tigo Pesa kwenda kwa akaunti zingine.

Tumia akaunti yako kuokoa pesa ili upate gawio la Tigo Pesa kila baada ya miezi mitatu.

Tuna ushirikiano mzuri na vituo vyetu vya simu, tunawashirkisha habari zote kuhusu wafanyabiashara na hamna mabadiliko yanayofanyika bila idhini ya mfanyabiashara.

Ndio, pesa ilioko kwa akaunti ya Tigo Pesa inaweza patikana kwa ndugu pale mfanyabiashara akifariki, kwakkuwasilisha nyaraka zitakazotakiwa na kufuata utaratibu wa kawaida, kama cheti cha kifo nk.

Mteja anaweza pakua app kwa kutembelea App Store au kwa kubofya kiungo itakayotumwa kwa SMS au tembelea tovuti yetu ya Tigo kupakua App.

Ndio, haijalishi mtandao gani unatumia. Hakikisha wakati unajisajili na app ya Tigo Pesa laini yako ya Tigo iko kwenye simu unayotumia na unatumia intaneti ya Tigo na sio mtandao mwingine, baada ya kujisajili ndo unapoweza kutumia mtandao mwingine.

Ndio, utatumia namba ya siri ile ile unayotumiaga ukipiga *150*01#. 

Huduma zote za muhimu ambazo zipo kwenye Tigo Pesa zinapatikana katika app ya Tigo Pesa.

Mara nyingi meseji ya kukamilika kwa muamala huingia baada ya muda mfupi lakini kuna muda mwingine mtandao unaweza kusumbua.

Kama umesubiri zaidi ya dakika 10 na hujapata meseji ya kukamilika kwa muamala, angalia salio au piga simu kwa kituo vyetu vya simu kwa kupiga 100.

Tigo Pesa inategema mtandao wa Tigo. Kwa bahtai mbaya ambapo mtandao wa Tigo utakua uko chini, epuka kufanya muamala wa aina wowote mpaka pale mtandao utakapo rudi hewani na ukiona simu yako ina mtandao.

Cha kwanza  ni kupiga simu kituo cha simu cha Tigo Pesa kwa kupiga 100 au tembelea duka lolote la Tigo Pesa na toa taarifa ya kupotea kwa laini au simu.

Mhudumu atakuuliza maswali ili aweze kuthibitisha uhalisia wa mteja na ndipo kuweza kufunga hiyo akaunti, utaratibu mwingine wa kupata laini nyingine utafuata.

Muamala wa kimakosa utatokea lakini ni muhimu kutoa ripoti mara moja kwa kupiga huduma kwa wateja kwa namba 100. Kama pesa bado haijatolewa bado, Tigo watweza kubadilisha huo muamala na kurudi kwa mteja. Kama pesa imeshatolewa na mpokeaji, mteja atoe taarifa kituo cha polisi na Tigo wataendelea na utaratibu mwingine wa kurudisha pesa.

TigoPesa Jihudumie ni huduma inayowawezesha watumiaji wenyewe kutatua masuala yanayohusu Tigo Pesa bila ulazima wa kuwasiliana na Huduma kwa Wateja.

Kuzuia Muamala ni kitendo cha kuomba pesa ambazo zimetumwa kimakosa kwa mtumiaji mwingine zirudishwe kwa aliyetuma. Sasa unaweza Kuzuia Muamala bila kuwasiliana na Huduma kwa Wateja.

Huduma ya Kuzuia Miamala. Tigo inawezesha watumiaji Kuzuia Miamala ambayo imetumwa kimakosa kwa wateja wengine wa Tigo bila ulazima wa kuwasiliana na Huduma kwa Wateja.

Mara tu unapogundua kuwa umekosea kutuma pesa kwa mteja wa Tigo Pesa, piga *150*01#, Chagua namba 6, Jihudumie (Akaunti yangu) na kisha fuata maelekezo.

Kwa sasa unaweza Kuzuia Miamala ya pesa zilizotumwa kimakosa kwa mteja wa Tigo, ila ndani ya kipindi kifupi utaweza Kuzuia Miamala ya kutuma hela ya aina zote (kwa pesa zilizotumwa kwenda mitandao mingine).

Ili uweze Kuzuia Muamala, unahitaji tu kupiga *150*01#, Chagua namba 6, Jihudumie (Akaunti Yangu) na fuata maelekezo. Unahitaji kuwa na kiasi cha Tsh 50 kwenye akaunti yako ambayo ndio gharama ya huduma hii.

Unaweza Kuzuia Muamala mara tatu (3) kwa siku. Ili kitendo cha kuzuia kifanikiwe inabidi kifanyike ndani ya muda wa dakika 30 baada ya kufanya muamala wa awali. Ikiwa hujazuia muamala ndani ya dakika 30 baada ya kutuma pesa, unashauriwa kuomba msaada kutoka kitengo cha Huduma kwa Wateja kwa kupiga namba 100.

Ndio, unaweza Kuzuia Muamala popote ulipo Tanzania.

Sasa wewe mwenyewe unaweza Kuzuia Muamala. Hauhitaji kuwasiliana na Huduma kwa Wateja. Mara tu unapogundua kuwa umekosea kutuma pesa, piga *150*01#, halafu chagua namba 6, Jihudumie na fuata maelekezo.

Unaweza Kuzuia Miamala ya kiasi chochote hadi kufikia Tsh3,000,000 ambacho ni kiwango cha juu zaidi cha muamala kinachoruhusiwa kwa siku.

? Usiwe na shaka lolote kuhusu mtu uliyemtumia pesa kikamosa kukataa ombi lako la Kuzuia Muamala. Pesa zako zitabaki kuwa salama hata ikitokea kuwa uliyemtumia kimakosa amekataa kuidhinisha ombi lako. Wasiliana na kitengo cha Huduma kwa Wateja kwa kupiga namba 100 kwa msaada zaidi.

Hautapoteza pesa zako. Ikiwa pesa halali zitazuiliwa, tafadhali wasiliana na Huduma kwa Wateja kwa kupiga namba 100 kwa msaada zaidi.

Huduma hii inapatikana kwa wateja pekee. Wakala hawawezi Kuzuia Muamala. Ikiwa Wakala atajaribu Kuzuia Muamala atapokea ujumbe utakaomtaarifu kuwa haruhusiwi kutumia huduma hii. Hali kadhlika, huwezi Kuzuia Muamala kwa namba ya mfanyabiashara aliyesajiliwa.

Huduma hii inapatikana tu kwa miamala ya kutuma pesa. Miamala ya Epin Pesa haiwezi kuzuiliwa.

Kwa sasa huduma hii inapatikana tu kwenye menu yetu ya USSD, ila hivi karibuni itapatikana kwenye TigoPesa App.

Unaweza tu Kuzuia Muamala uliofanyika ndani ya nusu saa. Baada ya nusu saa tafadhali wasiliana na kitengo cha Huduma kwa Wateja kwa kupiga namba 100 ili upate msaada.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo