Appanachezea | Tigo Tanzania

 Appanachezea

Appana Chezea Tigo Pesa App

Pakua na Tumia Tigo Pesa app. Ni rahisi, salama na haitumii MB zako! Tuma pesa, ongeza salio na nunua kifurushi kwa Tigo Pesa App urudishiwe pesa au upate dakika na MB bure
Rahisi

Ni rahisi kutuma mihamala, kulipia billi, kununua vifurushi na kununua salio kupitia Tigo Pesa app
Haitumii MB

Tigo Pesa App haitumii MB zako hata kidogo!
Salama

Tigo Pesa App ni salama kutumia. Usimpe mtu yeyote namba yako ya siri.

Tuma Pesa

Tuma pesa kwa mtandao wa Tigo na mitandao mingine. Ingiza namba ya simu au changua kutoka kwenye orodha ya simu kisha uingize kiasi cha kutuma

Tuma kwenda Benki

Hamisha pesa kwenda kwenye akaunti yako ya Benki ndani ya sekunde chache. Unachohitaji ni jina la bank na namba ya akaunti.

Nunua Salio

Nunua salio la kwako ama la mtu mwingine kwa kutumia Tigo Pesa app

Nunua Vifurushi

Buy or gift bundles using Tigo Pesa App, any time, any where. Click "Airtime" to check your airtime and bundle balance easily.

Kulipia Bili

Lipia billi zako za kila siku kama vile umeme, maji na kadhalika kwa urahisi kwa kutumia Tigo Pesa app

Kutoa Pesa

Tembelea wakala wa Tigo Pesa ili kutoa pesa kwa kutumia Tigo Pesa app

Masterpass QR

Scani Masterpass QR code kulipia bidhaa ama huduma kwa wakala yoyote mwenye code ya Masterpass QR

Malipo ya serikali

Lipia malipo kadha wa kadha ya serikali kirahisi kwa kutumia Tigo Pesa app

Maswali ya mara kwa mara Appana Chezea Tigo pesa App

  Ninayo App ya Tigo Pesa; je ninahitaji kuifuta kupakua nyingine?

Hapana, unaweza kuiboresha App yako bila ya kuifuta kwa kitufe cha kuboresha (Update).

  Je ninahitaji kuwasiliana na wahudumu wa Tigo kutumia App?

Hapana, mteja ataweza kupakua na kuwezesha App bila ya kuhitaji maelezo. App imetengezwa kwa njia rahisi inayoweza kufanywa na mteja.

  Ninaweza kupata bonasi zaidi ya mara mbili?

Mteja atapata bonasi kwa kila muamala ambao umetajwa kuwa na bonus atakaoufanya kwa App ya Tigo Pesa.

  Nani anapata bonasi wakati mteja akimnunulia Kifurushi Rafiki?

Mteja aliye mnunulia Rafiki kifurushi ndio atapata bonasi.

  Je App ina usalama gani?

App hii ina usalama wa kisasa kukulinda wewe kama mteja, lakini tunapenda kukumbusha umuhimu wa kutompa mtu PIN yako ya Tigo Pesa na kujua kuwa Wafanyakazi wa Tigo hawatohitaji namba yako ya Siri kwa matumizi yoyote. Pia hakikisha unasajili App kwenye simu/kifaa chako binafsi, usiruhusu mtu yeyote awezeshe App kwenye simu isiyoyako.

  OTP ni nini?

OTP ni PIN ya mara moja unayotumiwa kusajili App ya TigoPesa endapo huitumii kwenye mtandao wa Tigo, au laini yako haipo kwenye simu/kifaa chako. Kwa mfumo wa Android, App itakujazia namba hiyo. Lakini kwa mfumo wa iOS tafadhali nakili namba uweke kwenye simu.

  Je App inatumia vocha au kifurushi changu?

Hapana, App ya Tigo Pesa haitumii kifurushi cha bando, wala vocha yako endapo unatumia mtandao wa Tigo. Zingatia kuwasha intaneti ya Tigo kuwezesha mtandao, ila haitotumia kifurushi wala vocha yako.

  Je naweza kuitumia kwenye mtandao wowote au WiFi

Ndio, App inaweza kutumika na mtandao wowote, lakini gharama za Intaneti za mtandao husika zitahusika. Pia unaweza kupata OTP(PIN ya mara moja) endapo utatumia App nje ya mtandao wa Tigo au utakapohitaji kutumia App bila laini ya Tigo kuwa kwenye kifaa chako.

  Je napataje Ofa hizi?

>Pindi unapopakua na kujiunga kikamilifu kwenye App kwa mara ya kwanza, unapata kifurushi mahususi cha kukukaribisha
>Pindi ufanyapo muamala kwenda Tigo kwa kutumia App ya Tigo Pesa, utarudishiwa gharama za muamalo/makato.
>Pindi ununuapo kifurushi kwa kutumia App ya Tigo Pesa, utazawadiwa bonasi ya Dakika na MB
>Pindi uongezapo salio kwa kutumia App ya Tigo Pesa, utazawadiwa bonasi ya Dakika na MB

  Je napata ofa hizi nitumiapo *150*01#?

Hii ni maalumu kwa watumiaji wa App ya Tigo Pesa. Jiunge sasa kwa kupakua na ufanye miamala kidijitali. Pakua App kutoka App Store au Play Store leo.

  Ni bei gani au gharama yake ikoje?

Hakuna gharama ya ziada kufanya miamala kwa kutumia App ya Tigo Pesa na zaidi unaweza kuokoa gharama kwani kuangalia salio ni bure, na pia App haitumii kifurushi cha intaneti wala salio kuu, ukiwa kwenye mtandao wa intaneti ya Tigo.

  Nafanyaje kupata huduma hii?

Ni rahisi, unahitaji kuwa na laini ya Tigo iliyosajiliwa na Tigo Pesa. Utatembelea eneo husika la kupakua app tafuta Tigo Pesa upakue kwenye simu yako na kuiwezesha kwa kutumia Namba yako ya Siri ya Tigo Pesa, uanze kufanya miamala kidijitali na ufurahie huduma hii bora.

  Ni huduma gani hii?

Tigo tukiwa vinara wa maisha ya kidijitali tunawazawadia wateja wetu watumiao App ya Tigo Pesa kufanya miamala kidijitali kuendana na kauli mbiu yetu inayohimiza maisha ya kidijitali. Tunarudisha gharama ya muamala pindi mteja ufanyapo muamala kwa kutuma kwenda mtandao wa Tigo kwa kutumia App. Vilevile tunawazawadia wateja Muda wa Maongezi na MB pindi wanunuapo vifurushi na kuongeza salio kwa App ya Tigo Pesa


Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo