Jihudumie | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Jihudumie

Tigo Pesa Jihudumie

Tigo Pesa imezindua huduma ya kipekee ya ‘Jihudumie’ inayokuwezesha kuzuia miamala iliyokosewa ya kutuma pesa Tigo kwenda Tigo Ni rahisi sana na sasa hauhitaji kuwa na wasiwasi tena kuhusu kupoteza pesa zako.

Jinsi ya kufuatilia malipo ya luku yaliyokosewa

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua namba 6, Ufuatiliaji binafsi (Akaunti yangu)
 3. Chagua namba 7, LUKU Tokens

Jinsi ya kurudisha muamala ulitumwa kimakosa

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua namba 6, Jihudumie (Akaunti yangu)
 3. Chagua namba 1, rudisha muamala
 4. Chagua muamala unaotaka kurudisha
 5. Ingiza namba yako siri kukubali

Utapokea ujumbe mfupi unaokufahamisha muamala umezuiwa na pesa yako iko salama. Pesa uliokosea kutuma itarudi kwenye akaunti yako pindi mpokeaji atakapo ruhusu


Jinsi ya kuthibitisha muamala uliotumwa kimakosa

 1. Piga *150*01#
 2. Chagua namba 6, Jihudumie (Akaunti yangu)
 3. Chagua namba 2, kukubali au kukataa kurudisha
 4. Chagua muamala unaotaka kukubali au kukataa kurudisha
 5. Ingiza namba yako siri kukubali au kukataa

Utapokea ujumbe mfupi kukufahamisha kwamba muamala umefanikiwa


Angalizo

Tigo inashauri kuwa makini unapofanya muhamala ili kuondoa usumbufu na upotezaji wa pesa. Tigo itatuma ujumbe mfupi kwa mpokeaji na mtumaji wa pesa kuhabarisha kuwa muhamala umekosewa na pesa zitarudishwa kwa mtumaji. Kama mpokeaji wa pesa anawasiwasi na kurudishwa kwa pesa, anashauriwa kupiga 100 na maelezo na muhamala husika ili kupata msaada Ikiwa muhamala umekosewa, unashauriwa kupiga 100 mapema iwezekanavyo kupata msaada kutoka kwa watoa huduma kwa wateja wetu, Tigo haitahusika ikitokea muhamala uliokosewa utatumiwa na mpokeaji.

Muda wa mrejesho kwa muhamala uliokosewa

 • Kutuma Pesa : Tigo kwenda Tigo – Masaa 12
 • Kutuma pesa : Tigo kwenda mitandao mingine MNO’s (Voda, Airtel & Zantel) – Masaa 72
 • Kutoa pesa : Masaa 24
 • Kuweka pesa : Masaa 12
 • Kulipia bili : Masaa 72
 • Kuweka pesa kwenye akaunti ya benki: Masaa 72
 • Kutoa pesa kutoka akaunti ya benki : Masaa 72

Angalizo:

Masaa yaliyo orodheshwa hapo juu ni muda wa mihamala ya kawaida. Kwa mazingira yasiyo ya kawaida muda unaweza kuongezeka kutokana na muhamala husika.

Kwa msaada zaidi

Endapo utapata tatizo linalohusiana na utoaji wa huduma za Tigo Pesa, fuata hatua hizi:

 1. Piga Huduma kwa Wateja, namba 100 muda wowote au tembelea duka lolote la Tigo muda wa kazi
 2. Endapo utashindwa kupata msaada kutoka Huduma kwa Wateja au maduka ya Tigo, tafadhali tuma barua pepe kwenda: Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. ukieleza tatizo lako kwa undani
 3. Endapo hutaridhishwa na matokeo kwa njia za awali hapo juu, unaweza kulipeleka suala hilo kwa TCRA kwa msaada zaidi

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo