Masterpass QR | Tigo Tanzania

 Masterpass QR

Tigo Pesa Masterpass QR inaondoa ulazima wa kubeba pesa taslim au kadi ya benki. Kwa hiyo hata ukisahau pochi lako nyumbani, bado unaweza kufanya malipo kupitia Masterpass QR. Mfumo huu unakuhakikishia usalama wa kulipia bidhaa na huduma mbali mbali kwa kuscani nembo ya QR inayopatikana katika kaunta ya malipo dukani ukitumia simu janja (smartphone) au  kwa kuingiza tarakimu nane (8) za wakala/muuzaji husika ikiwa unatumia simu ya kawaida.

 

Kwa kupakua mfumo mpya zaidi ya Tigo Pesa App, Watanzania wataweza kufanya malipo kwa njia ya Masterpass QR kwa kufuata hatua rahisi zifuatazo;

1.       Fungua App yako ya TigoPesa kisha chagua Pay Merchant Masterpass (Lipa Wakala wa Masterpass).

2.       Tumia App yako ya Tigo Pesa kuscani nembo ya QR iliyopo kwenye kaunta ya kufanyia malipo (au ingiza herufi nane (8) za wakala zilizoainishwa chini ya nembo ya QR).

3.       Ingiza kiasi cha muamala.

4.       Ingiza namba yako ya siri (PIN) kuthibitisha malipo.

 Wale wasiokuwa na simu janja/smartphone au wanaotaka kutumia menu ya USSD wanaweza kufanya malipo kwa kufuata hatua hizi sita rahisi:

1.       Piga *150*01#

2.       Chagua 5 – Pay Merchant   Lipa Wakala)

3.       Chagua 2 – Pay Masterpass QR merchant (Lipa Wakala wa Masterpass QR)

4.       Ingiza tarakimu  8 za wakala

5.       Ingiza kiasi cha muamala

6.       Ingiza namba yako ya siri (PIN) kuthibitisha malipo

 

 

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo