Tigo Pesa Cash In | Tigo Tanzania

 Tigo Pesa Cash In

Tigo inakuongezea Pesa zaidi kwenye simu yako ukiweka pesa kwa wakala au ukihamisha pesa kutoka benki kuingia kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa kuanzia TSh 10,000 na zaidi.

Tigo itakuzawadia kulingana na kiasi ulichoweka kwenye Tigo Pesa yako, ukiweka kiwango kikubwa zaidi utaongezewa Pesa Zaidi kwenye akaunti yako.

Unaweza kuhamisha pesa kutoka benki zaidi ya 50 kuingia kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa kama zilivyo orodheshwa hapa; CRDB, NMB, NBCTPB, BOA, ACB, ACCESS BANK, STANBIC BANK, FNB, BARCLAYS, KCB, EXIM, STANDARD CHARTERED, AMANA, I&M, MKOMBOZI BANK, ABC, EQUITY, UMOJASWITCH, ECO BANK, FINCA, PBZ, MAENDELEO BANK, YETU BANK

Fuata haya maelekezo kuhamisha pesa kutoka Benki kuingia kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa; Piga*150*01# kisha chagua 7 Huduma za kifedha, kisha chagua 2 Benki kwenda Tigo Pesa, kisha chagua benki yako.

Pesa utakayoongezewa unaweza kuitumia vyovyote, kama vile kununua muda wa maongezi au vifurushi, kulipia bidhaa kwenye duka lolote lenye alama ya Lipa hapa, kulipa bili, kuituma au unaweza kuitoa kwa wakala yeyote.

Ofa hii ni kwa mikoa ya Kagera, Kigoma, Mara, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Manyara, Singida, Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma. Ofa hii ni ya muda mfupi. Wahi sasa, usiikose!

Vigezo na masharti kuzingatiwa.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo