Personal Insurance - Bima Mkononi | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Personal Insurance - Bima Mkononi

TIGO GREEN FOR KILI:

Kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita tumeshuhudia kupungua kwa kasi kwa theluji katika kilele cha mlima Kilimanjaro.Mbali na ongezeko la joto la dunia, tatizo hili pia limechangiwa na ukataji wa miti uliokithiri ambao umesababisha mabadiliko ya hali ya hewa na kushuka kwa kiwango cha mvua katika eneo la mlima Kilimanjaro.

Tafiti zinaonesha kuwa hadi ifikapo mwaka 2033 kilele cha Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi Afrika kitapotea huku asilimia 85 ya theluji katika kilele cha mlima ikipungua kwa kipindi cha miaka 100 na kusababisha kupungua kwa futi 19,000 za urefu wa mlima.

Serikali na taasisi zisizo za kiserikali zimekuwa zikichukua hatua mbalimbali kutatua changamoto hizi na kwa kiasi kikubwa juhudi hizi zimeanza kuzaa matunda.

Aidha, shughuli za ukataji holela wa miti kwaajili ya kuni na magogo zimekithiri na zinahatarisha uhai wa misitu katika eneo la mlima huu.Endapo changamoto hizi zisipochukuliwa hatua ili kudhibiti zitasababisha upotevu wa viumbe hai ambavyo duniani vinapatikana katika eneo hili pekee.

Kama mdhamini wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka sita mfululizo, tunaanza mwaka 2021 kwa kusaidia utunzaji wa mazingira katika eneo la Kilimanjaro na kusaidia kurejesha theluji kwenye Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa cha utalii na fahari ya Afrika.

Katika kufanikisha hilo tumeanza kwa kuzindua kampeni ijulikanayo kama TIGO GREEN FOR KILI-ONE STEP ONE TREE. Lengo ni kupanda jumla ya miti 28,000 na Tigo imeanza kwa kupanda miti 10,000 Moshi mwezi Februari mwaka huu. Kauli mbiu yetu ni ‘Mti mmoja utapandwa katika kila hatua utakayopiga’.

Gharama ya mti mmoja ni Sh 5,000 na wateja wetu wanaweza kuchangia kupitia huduma ya LIPA KWA SIMU kwa namba 9867912.

Tigo inawakaribisha wadau na umma kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja kufanikisha azma hii ya kuhakikisha tunaifanya Kilimanjaro kuwa ya kijani tena.

TIGO GREEN FOR KILI- ONE STEP ONE TREE.


Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo