Tuma na Kupokea Pesa | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Tuma na Kupokea Pesa

Tigo Pesa inatoa fursa kwa watumiaji kutuma na kupokea pesa kati ya watoa huduma za kifedha, kuliko mwendeshaji mwingine yeyote. Mialama ya Tigo Pesa kwenda kwa watumiaji wa MPesa, AirtelMoney, TPesa,Halopesa NA EzyPesa inakuwa rahisi sana kupitia watumiaji wengine wa Tigo Pesa.

Jinsi ya Kutuma na Kupokea Pesa kwa Tigo Pesa

1.       Piga *150*01#

2.       Chagua “1” to kutuma pesa, alafu

3.       Chagua “1” kutuma kwa mteja wa Tigo, au “3” kutuma kwa mitandao mingine.


Jinsi ya kutuma pesa kwa kutumia Tigo Pesa App

1.       Fungua App ya Tigo Pesa

2.      Chagua Kutuma Pesa

3.      Unaweza kuchagua unayetaka kumtumia kutoka kwenye orodha ya watu walioko katika simu yako kwa kuandika kwenye chagua au kuingiza namba ya muhusika.

4.      Ingiza kiasi na gusa kwenye endelea

5.     Utaona ukurasa wenye jina la mpokeaji na ingiza nywila kukamilisha muamala

Pata App ya Tigo Pesa ufanye miamala ya Tigo Pesa kwa urahisi, upesi na kuaminika zaidi.

 


 

Maswali ya Mara kwa Mara:

  Ni hatua zipi natakiwa kufuata ili kutuma pesa?
 • Piga*150*01#
 • Chagua 1 Kutuma Pesa
 • Chagua 1 kuingiza namba ya mpokeaji
 • Ingiza namba ya mppokaeaji
 • Ingiza Kiasi
 • Ingiza PIN/namba uya siri kuthibitisha muamala
  Kuna faida zipi kutuma pesa kwa kutuma Tigo Pesa?
 • Ni ya Uhakika: Hakuna haja ya kutembea umbali mrefu kwenda benki au kwa Wakala ili kutuma pesa.Unaweza kutumia simu yako kutuma pesa kwa urahisi zaidi mahali popote na wakati wowote.
 • Ni Nafuu:Ada za kutuma pes ani nafuu zaidi kulinganisha na mitandao mingine
 • Moja kwa Moja:Pesa inaingia kwenye akaunti ya mpokeaji moja kwa moja
 • Ni Salama: Hakuna athari au wizi wakati wa kutuma pes ana Tigo Pesa
 • Papokwa papo:Tofauti na njia zingine, mteja anapokea pesa mara baada tu ya muamala kuthibitishwa.
  Nitatozwa kiasi gani kutuma pesa?
 • Tigo Pesa ina gharama nafuu zaidi za kutuma pesa kwenda Tigo Pesa au mitandao mingine ya simu.
 • Gharama zetu zinazingatia ushindani zaidi na zinapatikana kwenye tovuti yetu.
  Nitatozwa kiasi gani kupokea pesa?
 • Hakuna gharama zozote za kupokea pesa, ni bure.
  Itakuwa endapo nimetuma pea kwa mtu kimakosa?
 • Unaweza kupiga simu kwa huduma kwa wateja namba 100.
 • Wakala atathibitisha kama muamala ulitumwa kikamilifu au La!
 • Pia, Wakala atakusanya taarifa muhiu kutoka kwako na atafuata taratibu za kurudisha muamala uliokosewa.

Vigezo na Masharti:

 • Mteja anatakiwa kuwa amesajili na Tigo Pesa
 • Mteja anatakiwa kuwa na salio la pesa kwenye akaunti yake Pamoja na pesa ya kutuma
 • Mteja ataweza kutuma pesa ambayo ipo kwenye viwango vilivyowekwa

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo