Tumia MasterCard QR | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Tumia MasterCard QR

Tigo Pesa MasterCard QR inaondoa ulazima wa kubeba pesa taslim au kadi ya benki. Kwa hiyo hata ukisahau pochi lako nyumbani, bado unaweza kufanya malipo kupitia MasterCard QR. Mfumo huu unakuhakikishia usalama wa kulipia bidhaa na huduma mbali mbali kwa kuscani nembo ya QR inayopatikana katika kaunta ya malipo dukani ukitumia simu janja (smartphone) au  kwa kuingiza tarakimu nane (8) za wakala/muuzaji husika ikiwa unatumia simu ya kawaida.

Kwa kupakua mfumo mpya zaidi ya Tigo Pesa App, Watanzania wataweza kufanya malipo kwa njia ya MasterCard QR kwa kufuata hatua rahisi zifuatazo;

1.       Fungua App yako ya TigoPesa kisha chagua Pay Merchant MasterCard (Lipa Wakala wa MasterCard).

2.       Tumia App yako ya Tigo Pesa kuscani nembo ya QR iliyopo kwenye kaunta ya kufanyia malipo (au ingiza herufi nane (8) za wakala zilizoainishwa chini ya nembo ya QR).

3.       Ingiza kiasi cha muamala.

4.       Ingiza namba yako ya siri (PIN) kuthibitisha malipo.

 Wale wasiokuwa na simu janja/smartphone au wanaotaka kutumia menu ya USSD wanaweza kufanya malipo kwa kufuata hatua hizi sita rahisi:

1.       Piga *150*01#

2.       Chagua 5 – Pay Merchant   Lipa Wakala)

3.       Chagua 2 – Pay MasterCard QR merchant (Lipa Wakala wa MasterCard QR)

4.       Ingiza tarakimu  8 za wakala

5.       Ingiza kiasi cha muamala

6.       Ingiza namba yako ya siri (PIN) kuthibitisha malipo

 


 

Maswali ya Mara kwa Mara:

  Ni Huduma gani hii?

Ni huduma inayowawezesha wateja wa Tigo Pesa kufanya manunuzi ya bidhaa au malipo ya huduma kwa wafanya biashara wanaokubali malipo kupitia Mastepass, kwa njia rahisi ya kuskani picha ya QR na kulipa

  Masterpass ni nini

Masterpass ni huduma inayotolewa na Mastercard kumuwezesha mteja kufanya malipo kwa ya kidigitali ambayo ni ya haraka, salama na rahisi.
Huduma hii kwasasa inaweza kutumiwa na wateja wa Tigo Pesa kwa simu janja na simu za kawaida kupitia menyu ya *150*01#

  Ni wapi naweza kulipia na Masterpass kwa kutumia Tigo Pesa?

Unaweza kutumia akaunti ya Tigo Pesa kununua bidhaa au kulipa huduma popote unapoona Lipa hapa na Masterpass

  Ni Jinsi gani ya kulipia na Masterpass kutumia Tigo Pesa?

Wateja wa Tigo Pesa wanaweza kununua bidhaa au kulipa huduma kwa wafanyabiashara wote ambao wanakubali malipo ya Masterpass
Malipo yanaweza kufanyika kwa njia mbili tofauti:

1) Kwa kupiga *150*01#
Chagua 5 - Lipa bidhaa
Chagua 2 - Lipa na Masterpass QR
Ingiza tarakimu nane(8) za mfanya biashara na kiasi
Thibitisha malipo na namba ya siri

2) Kwa kutupia Tigo Pesa App
Chagua "Lipia bidhaa"

Skani kodi ya QR na fuata malekezo
Au
Ingiza tarakimu nane(8) za mfanyabiashara kisha fuata maelekezo

  Kuna makato ya ziada unapofanya malipo kwenye huduma hii?

Hapana, hakuna makato yoyote ya ziada

   Je napata risiti/ Napataje risiti kwa manunuzi nifanyayo?

Wafanyabiashara wengi wataweza kutoa risiti, lakini zaidi kila mteja atapata risiti kwenye simu yake katika mfumo wa SMS (ujumbe mfupi)

Vigezo na Masharti:

  • Mteja anatakiwa kuwa amesajili na Tigo Pesa
  • Mteja anatakiwa kuwa na salio la pesa kwenye akaunti yake Pamoja na pesa ya kutuma
  • Mteja ataweza kutuma pesa ambayo ipo kwenye viwango vilivyowekwa

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo