Twende App | Tigo Tanzania

 Twende App

Chaguo #1 kwa usafiri wa Tanzania..

Twende inakupa usafiri wa haraka, salama na bei nafuu. Pia tunakaribisha maoni yako kwa kila safari kutusaidia kuwapanga madereva kwa maksi zao.

Huduma kwa wateja ya uhakika 24/7

Njia Za Usafiri Tulizonazo

Bajaji

Omba usafiri upate bajaj ndani ya dakika chache kupitia Twende. Safiri kwa usalama na madereva waliopatiwa mafunzo na kuhakikiwa.

Taxi

Omba usafiri upate taxi ndani ya dakika chache kupitia Twende. Safiri kwa style na usafiri unaokidhi vigezo vyako.

Boda boda

Omba usafiri upate bodaboda ndani ya dakika chache kupitia Twende. Wahi katika shughuli zako na Twende

 

 

Abiria

Faida ya kutumia Twende App 

● Malipo nafuu ya nauli 

● Fanya malipo kwa Tigopesa 

● Ni rahisi kupata usafiri

● Madereva waliohakikiwa na wenye mafunzo sahihi

● Ni rahisi kuitumia

 

Jinsi ya kutumia Twende App ya Abiria

● Kupakua App - Pakua Twende App katika Play Store.

● Kujiunga - Weka namba yako ya Tigo iliyosajiliwa.

● Ita usafiri - Chagua Taxi, Bajaj au Bodaboda. 

● Wasiliana na dereva kwa kupiga simu- Fahamu dereva alipo na pata mawasiliano yote.

● Taarifa za safari - Utapata taarifa dereva akifika sehemu ulipo.

● Jua mahali ulipo - Anza safari na jua mahali ulipofika.

● Lipa nauli - Lipa kwa Tigo pesa au fedha taslimu

● Thaminisha na toa maoni yako kuhusu dereva na safari yako. 

 

Dereva

Faida za kutumia Twende App

● Ni rahisi kupata abiria, 

● Kipato chako kitaongezeka

● Pokea malipo ya nauli kwa Tigopesa 

● Abiria wamesajiliwa na wanaotambulika 

● Ni rahisi kuitumia

 

Jinsi ya Kutumia Twende App ya dereva

● Kupakua App - Pakua Twende App katika Play Store.

● Kujiunga - Bonyeza "Jiunge" na hakikisha unakamilisha hatua zote za usajili.

● Kuingia - Bonyeza "ingia" baada ya kujaza namba yako ya simu na weka neno siri.

● Kuhakikiwa - Bonyeza "ndio" baada ya kuhakikiwa na TWENDE.

● Kufungua - Bonyeza "fungua" na kisha subiri ili kupata abiria.

● Kubali safari- Abiria atatuma ombi la usafiri

● Mpigie simu abiria kujua mahari alipo

● Mfuate abiria - Mjulishe abiria kuwa unafuata mahali alipo.

● Anza safari - Bonyeza "Safari Imeanza" abiria akiingia kwenye chombo chako na safari kuanza. 

● Safari imekamilika - Bonyeza "Safari Imekamilika" ukimfikisha abiria anapo kwenda.

● Malipo - abiria atalipa nauli kwa Tigopesa au  fedha taslimu kulingana na ankra atakayopewa.

● Thaminisha na toa maoni kuhusu abiria na safari yako.

 

Vigezo na Masharti

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo