Kibubu Vigezo na Masharti | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

Tigo Pesa Kibubu Vigezo na Masharti

 

 1. Kila mteja kwenye namba ya simu ileile, atakuwa na akaunti ya pili mbali na ile ya awali ambayo inatumika kufanya miamala ya kawaida bila gharama yoyote..
 2. Akaunti ya sasa itabaki kuwa akaunti KUU ambayo itatumika kwaajili ya miamala ya kawaida kama ilivyo sasa.Hakuna mabadiliko yoyote kwenye matumizi katika akaunti ya KUU.
 3. Akaunti ya pili itakuwa akaunti ya Tigo Pesa Kibubu
 4. Tigo Pesa Kibubu itatumika tu kuhifadhi pesa kwa matumzi ya baadae. Pia, haitawezekana kufanya miamala ya kawaida kwenye akaunti hii isipokuwa kuweka na kutoa pesa pekee.
 5. Pesa zitawekwa kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu kwa kuzitoa kwenye akaunti KUU na pia pesa zitatolewa kutoka kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu kwa kuziingiza kwenye akaunti KUU.
 6. Kiasi kile kile na Kiwango cha mwisho cha kufanya miamala kinachotumika kwenye akaunti Kuu ndicho kitatumika kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu (Hii inategemea na aina ya mteja)
 7. Pesa zilizopo kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu zitaweza kupata gawio kulingana na kiasi na muda ambao zimehifadhiwa na pia gawio hilo litajulishwa kwa mteja.
 8. Wateja wataweza kutunza pesa kiasi chochote cha pesa kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu na pia wataweza kutoa kiasi chote au kiasi fulani kutoka akaunti ya Tigo Pesa Kibubu na kwenye akaunti kuu vilevile kama sheria za matumizi ya miamala zisemavyo.
 9. Tigo itatoza gharama ya huduma ya kawaida kwenye akaunti ya kawaida ya Tigo Pesa huku huduma kwenye akaunti ya Tigo Pesa Kibubu itakuwa BURE. Endapo kutakuwa na gharama zozote zitakazojitokeza zitaoneshwa kwa mteja kabla ya kutumia huduma na gharama hizo zitawasilishwa Benki Kuu baada ya kuzindua au kabla ya kufanya mabadiliko kwenye huduma.
 10. Gawio atakayopata mteja italipwa moja kwa moja kwenye akaunti KUU ya mteja ya Tigo Pesa kila mwezi i kulingana na kiwango cha gawio kitakachokua kimepangwa na Bank na Tigo Pesa.
 11. Gawio la mpaka 7% kwa mwaka linalojumuishwa kila siku na kulipwa kila mwisho wa mwezi.
 12. Kiwango cha gawio cha kila siku kinapatikana kwa kugawanya kiwango cha gawio cha kila mwaka na siku 365. Hesabu yako ya gawio inategemea kiwango cha pesa ulichonacho kwenye akaunti yako Tigo Pesa Kibubu kila mwisho wa siku.
 13. Gawio itakayolipwa kila mwezi ni mjumuisho wa gawio ya kila siku ya mwezi husika . Gawio hii italipwa italipwa kwenye akanti KUU ya Tigo Pesa.
 14. Pesa zitakazo hifadhiwa kwenye Tigo Pesa Kibubu zitaanza kupata gawio siku hiyo hiyo endapo zitahidhifadhiwa kabla ya muda wa kufnga biashara. Pesa zitakazo hifadhiwa baada ya muda wa kufunga biashara zitaanza kupata gawio siku inayofuata (Muda wa kufunga biashara ni saa nane kamili mchana <08:00> na muda huu unaweza kubadilika kulingana na masharti ya uendeshaji biashara). Pesa iliyopo kwenye kibubu haitopata gawio siku itakayo tolewa kwenye kibubu. Gawio ya pesa zilizohifadhiwa siku za mwisho wa wiki (Jumamosi na Jumapili) na siku za sikukuu itahesabiwa siku za kazi zinazofuata.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo